Nani waziri bora kwa mwaka 2012?

Nani waziri bora kwa mwaka 2012?

Waziri Wa Nishati na Madini - JOHN .J. MNYIKA

Mbunge Wa Wananchi Wa UBUNGO .

MUNGU Amzidishie yale yote yaliyo Mema Ayatakayo .
 
Wana JF, mwaka 2012 ndio unaishia ukingoni hivyo basi ningependa kila mmoja atoe maoni yake kuhusiana na utendaji kazi wa mawaziri wetu. Tufanye evaluation kwa kipindi chote cha mwaka 2012. Unafikiri ni nani anastahili kuwa waziri bora wa mwaka?. Si vibaya pia kama utamtaja na naibu waziri bora wa mwaka 2012. Karibuni.

Chema chajiuza kibaya chajitembeza; tuwajadili wabovu kwa kina ili wapate aibu!

Naanza hivi:
1: Lazarus Nyalandu kwa kuhujumu shirika la umma TANAPA
2: Sopspeter Muhongo kwa kuwa muongo na kukosa msimamo thabiti
3: Hawa Ghasia uswahili na kukosa impact katika serikali
4: Khamis Kagasheki kwa kukiuka sheria za nchi "kumchonga" Meya wa Bukoba mjini kwa maslahi binafsi.
5: Shukuru Kawambwa kwa viwango duni vya elimu nchini
6: Abdalah Kigoda kudanganya umma kuhusu uhai wa viwanda nchini
7: William Mgimwa kwa kuanguka thamani ya shilingi.
8: Mark Mwandosya kwa kupokea mshahara na marupurupu bila kufanya kazi
9: Aggrey Mwandri pure utopianist!

sasa endeleeni
 
  1. Dr.John Pombe Magufuri
  2. Prof.Anna Tibaijuka.
  3. Dr.Harson Mwakyembe.
  4. Steven Wassira.
  5. Dr.William Mgimwa.
  6. .January Makamba.
  7. Dr.Marry Nagu.
  8. Dr.Shukuru Kawambwa
  9. Bernad membe.
  10. Mohamed Abood.
Kwanini JPM? Sababu nyingi zinaonekana na miradi mingine bado inaendelea kwa kasi chini ya usimamizi wake imara.
 
Katiba pia inawatambua mawaziri vivuli!



  1. Freeman A Mbowe
  2. Zitto Kabwe
  3. John Mnyika
  4. Tundu Lissu
  5. Ezekia Wenje

6.Halima Mdee
7.Vicent Nyerere

Kwanini FAM? Sababu zipo ni nyingi,mojawapo ni kuwa mfano wa kuigwa katika hoja,mijadala na ni kiongozi mtulivu,asiyekurupuka wala kuwa na stress zisizo na maana juu ya uendeshwaji wa nchi.
 
Tuwekee VIGEZO na MASHARTI ili tuvizingatie wakati wa kuteua waziri bora mwaka huu.
 
1. mwakyembe waziri wa uchukuzi
2. balozi kaghasheki waziri wa maliasili na utalii
3 prof sospeter muhongo waziri wa nishati na madini


Vipi pembe za ndivu, kafanya nini huyo Kagasheki?
 
Weng wao bado wapo kwenye upembuz yakinifu na michakato mpaka June 2013 kipind cha bajet, Nadhan Mwakyembe anatajwa kwa sababu alifanya mambo kadhaa na kwa muda mfup, labda anastahil.
 
Mwakyembe kwa serikali kuu wengine vyenga tupu...
Lissu,zitto,mnyika wanafuata..kwa serikali kivuli wengine vyenga....
 
Mkuu mada yangu inawahusu mawaziri wa serikali iliyoko madarakani. Haiwahusu mawaziri vivuli.

Umenikumbusha tukiwa kidato cha 3 mwalimu wa history aliwahi kutuambia tujitungie maswali na tujibu na bado watu walifeli..ndicho kilichokutokea...hawa mawaziri vivuli, wapo madarakani na wanatambulika kikatiba na ndio wanaounda baraza kivuli la mawaziri, wana budget zao na huzisoma bungeni.. Sasa narudia kusema waziri bora kwa mwaka huu ni TUNDU LISSU kwisha
 
magufuli, mwakyembye, sospeter muhongo, kagasheki, mlugo na tibaijuka
 
hata wale kimvuli ni wa serikali kwani wote wanafanya kazi moja kwa niaba ya taifa letu
 
- Halima Mdee - Waziri kivuri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya Makazi
- Joseph Mbilinyi - Waziri kivuri wa Habari, Vijana na michezo.
 
Back
Top Bottom