Nani wa kutoa majibu kati ya CAG na Wizara ya fedha?

Nani wa kutoa majibu kati ya CAG na Wizara ya fedha?

Kweli atusaidie Shark.

Yaani pamoja na yote haya hujagundua kuwa nahoji utimamu wa prof Assad? Tulichotofautiana baada ya kuusoma uk 34, maana kabla ya kuusoma nilikuwa upande wa hoja za zitto, ni kuwa wewe unaendeleza hoja ya zitto kutaka serikali ieleze ziliko 1.5, nao wamejibu kizembe sana.

Mimi nahoji kazi ya cag, mbona kuna mengi tu kahoji? Ilikuwaje hili akakaa kimya? Alidhani hatutaipata kazi yake?

Kwa maneno mengine, amekaa kimya kwa kuwa anajua si serikali wala sisi wenye serikali hatuna cha kumfanya. Ana kiburi tu. Ametumia mabilioni kutuletea kazi incomplete.

Why this?
Nadhani unamtafuta CAG ili kumuangushia jumba bovu
 
Alipotezea vipi?? Waliotumia ndio ilibidi wapeleke nyaraka kama risiti, ili yeye atoe kutoka katika hyo 1.5tr.
Yeye kazi yake ni kuandika makusanyo, expenditure(zilitumika wapi), na ambazo hazijatumika ni hizi. Sasa kwann uwe na bajeti ya elfu 10, ujibane ukatumia elfu 7, halafu elfu 3 hazipo na wala hujui zipo wapi, hii ni akili..??

Halafu ulitegemea CAG pale ikulu alipoulizwa ajibu kweli sijaziona wakati usoni ameshamuona mkuu ana jazba?? Si ungeanza ugomvi mwngn palepale?

Na yeye wala hajasema zimepotea au zimeibiwa. Amesema hajajua zimetumikaje, kwa sababu hana rekodi zake
 
Mzee naamini hujasoma lolote kuhusu hili. Kifupi ni kuwa CAG kaandika kuhusu makadirio, mapato halisi na matumizi.

Hajasema lolote kuhusu baki inayotokana na tofauti kati ya mapato halisi na matumizi.

Ndo mi nahoji sasa, kabla ya kuwauliza serikali, kwa nini tusimwulize CAG alifanyaje katika eneo hilo?

Ilikuwaje akatuonesha mapato halisi na matumizi yaliyochini ya mapato halisi akashindwa kutuambia au hata kuwauliza serikali ziliko change?
 
Mkumbuke serikali huaanza kupanga bajeti ikisha ndio hutafuta pesa kwa ajili ya kuzitumia ni tofauti na kwenye private budget ambayo hupangwa kwa mujibu wa fedha zilizopo na kujaliziwa kwa fedha za kukopa. Ikiwa serikali imekusanya 25 trilioni maana yake matumizi yake yatakuwa ni hiyo 25 trilioni ila kwa mujibu wa CAG kilichotumiwa ni 23.5 trilioni tu. Sasa hii 1.5trilioni iliyokusanywa iko wapi? I nahitaji mchanganuo. Kwa maelezo ya naibu waziri amesema kuwa kuna hati fungani zisizowiva kuna mapato ya zanzibar na kuna receivables lakini suali linakuja jee hizo zilikuwa disclosed kwenye notes za financial statements ili CAG azikague? . Jee wakati wa exit meeting CAG alipewa hayo maelezo na vielelezo ili ajiridhishe? Jee CAG akiwa professor kwenye uhasibu hajui tofauti ya cash basis na accrual basis accounting?
Wafundishe hawo ndugu. Issue iko wazi kabisa. Lakini kuna wengine wanavichwa vigumu sana kuelewa. Maelezo ya huyo naibu waziri ni upotoshaji, ni njia ga uongo ya kujarobu kujinasua. Lakini hawatoki Ng' o. Report inetoka na haibadilishiki.
 
Repoti inasema trilion 23 zimetumika kulipa mishahara,madeni ,matumizi na AMANA za serikali.

Hivi Amana ni kitu gani hasa?,au ndo hizo bond?
 
Repoti inasema trilion 23 zimetumika kulipa mishahara,madeni ,matumizi na AMANA za serikali.

Hivi Amana ni kitu gani hasa?,au ndo hizo bond?
 
Mzee naamini hujasoma lolote kuhusu hili. Kifupi ni kuwa CAG kaandika kuhusu makadirio, mapato halisi na matumizi.

Hajasema lolote kuhusu baki inayotokana na tofauti kati ya mapato halisi na matumizi.

Ndo mi nahoji sasa, kabla ya kuwauliza serikali, kwa nini tusimwulize CAG alifanyaje katika eneo hilo?

Ilikuwaje akatuonesha mapato halisi na matumizi yaliyochini ya mapato halisi akashindwa kutuambia au hata kuwauliza serikali ziliko change?
Sio kazi yake kuuliza zipo chenji

Sent from my D5322 using JamiiForums mobile app
 
Nimekuelewa. CAG anatakiwa kutoa ufafanuzi kwenye hili huenda wasaidizi wake walioverlook kitu kwa bahati mbaya au kwa makusudi. Sio rahisi kuwa CAG amesoma neno kwa neno report za ukaguzi wa Serikali nzima but kwa hapo naona kuna kitu anatakiwa kukifafanua
 
Mbona mengine kauliza, akapewa majibu akaandika taarifa? Mbona ametoa hati safi, chafu na isiyoridhisha? We unadhani hakuhoji?

Hoja za ukaguzi zinakosaje sasa?
Ukiona hivyo ujue hilo wameshindwa wamwambie nn na jamaa akaanika kila kitu nje. Na hizo za matibabu nje ya nchi badala ya kupungua, zikazidi. Sasa hatujui za matibabu zzilizozid zimejumlishwa na za yule binti msanii aliyeoneshwa na shilawadu halafu yeye akampeleka India au yeye alihudumiwa kutoka kwny hizi tr 1.5. Mi sijui.

Sent from my D5322 using JamiiForums mobile app
 
Ukiona hivyo ujue hilo wameshindwa wamwambie nn na jamaa akaanika kila kitu nje. Na hizo za matibabu nje ya nchi badala ya kupungua, zikazidi. Sasa hatujui za matibabu zzilizozid zimejumlishwa na za yule binti msanii aliyeoneshwa na shilawadu halafu yeye akampeleka India au yeye alihudumiwa kutoka kwny hizi tr 1.5. Mi sijui.

Sent from my D5322 using JamiiForums mobile app
Zote hizo kazungumza isipokuwa 1.5. Hajasema lolote
 
Kwa nini asihoji na kama hakuna majibu akaandika taarifa yake? Hivi wewe ukimtuma mwanao kununu sukari dukani, ukampa 5,000/-, halafu akakuletea sukari na maelezo kuwa, "umenipa 5,000/-, kilo moja ni 3,500/-, sukari hii hapa.." Halafu akakaa kimya, au akasepa, utakubali?

Hautamwuliza change?
Yeye anahoji kwa kudai nyaraka ,kama hukupeleka nyaraka hawezi kusikiliza poroho.Tatizo lako mtoa mada unadhan CAG anafanya ukaguzi wa duka .
 
Zote hizo kazungumza isipokuwa 1.5. Hajasema lolote
Mkuu, hebu VAA VIATU VYA SERIKALI, ungeulizwa hivi ungejibu nini..?? Hakuna anyeweza kumnyooshea kidole mkuu..!!!

Yeye CAG ni kama katupa jiwe gizani kwa sababu hakuna jibu la moja kwa moja la wapi zilienda. Ofa anazotoa mzee baba watendaji HAWAWEZI KUHOJI. Kwa mfano mdogo alipotoa milioni 100 kwa yule mzee wa Tanzanite, unaweza kujua zimetoka wapi..?? Kama ni hazina, zimeidhinishwa na bunge?? Au ni mfukoni mwake..??

Sent from my D5322 using JamiiForums mobile app
 
Nadhani mleta mada unalazimisha CAG afanye kazi zingine za ziada. Ni sawa lakini sio lazima.
Kazi ya CAG ni kukagua mahesabu na kutupa mchanganuo. Na mchanganuo kauweka. Mengine jiongeze mwenyewe.

Sasa CAG angeweza kwenda zaidi ya hapo lakini ukumbuke haya....
1/Katika mazingira haya ya sasa ya kisiasa hata CAG analinda ugali wake, lazima acheze kama Pele. Tafsiri au mapendekezo yoyote kuhusu hizo 1.5Trilioni katika ripoti yake kungemwingiza kwenye kile kitu kinaitwa 'Uchochezi'. Serikali hii ingetafuta jinsi ya kumfukuza na kuja kumwita mpotoshaji.

2/Ripoti ya CAG huenda sambamba na viambatanisho na hivyo ndio vimebeba tafsiri nzima ya ripoti yake. Muhtasari wa ripoti unapaswa uwe neutral(very raw) ili kuwapa nafasi washika dau kuweza kuisoma ripoti katika jicho la haki.
 
Back
Top Bottom