Nani wa kumrithi IGP - Simon Sirro?

Naona Mahundi na Mahita ndio walidumu muda mrefu kuliko wengine.
Sijui siri ni nini
 
Mkuu kwani kuna nini...mara nyingi si huwa anakwenda nae mpaka mwisho wa utawala wake ama kuna fununu ya mtu kutumbuliwa
 
Ni wakati Tanzania wafanye kama Kenya Uganda, Rwanda IGP atoke JWTZ huko wao waligundua IGP akiwa mjeshi huwa makini zaidi

Halafu akikosekana wa kumrithi CDF atachukuliwa kutokea taasisi gani???

Uganda,Kenya sheria yao iko tofauti kidogo na sisi.hata basic course wanafanya pamoja.
 
Nafasi ya IGP ni ngumu sana.
Anaweza kuteuliwa mtu muadilifu kabisa, anaweza kuteuliwa mtu mcha Mungu lakini nafasi ya IGP ina mambo ya ajabu ajabu, anapokea order za ajabu ajabu kutoka kwa maboss wake akiwemo rais, inamuwia vigumu sana kua muadilifu.

Kuna wakati hawa wazee wanapata tabu sana kutetea serikali zilizoko madarakani, wanapata tabu sana kuwalinda maboss wao mara nyingi hua na mambo mengi ya uovu
 
Back
Top Bottom