Nani wa kulikomboa bara la Afrika?

Nani wa kulikomboa bara la Afrika?

Alloyce PR

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2020
Posts
590
Reaction score
706
Afrika buana! Hivi ni ugumu wa maisha au malezi magumu tuliyokuzwa nayo ndio umetufunga akili tusitambue jema? Bara hili pekee ndilo ambapo kiongozi anayeweka mbele maendeleo ya Taifa lake na kulinda maslahi ya wananchi wake huonekana adui, hupewa majina ya dikteta, mnywaji damu, mbaguzi, asiye na huruma, asiyetenda haki, hasa zile zinazohusiana na LGBTQ.

Ni kana kwamba kufanya yaliyo sahihi ni kosa. Je, Waafrika tumerogwa? Na kama kweli tumerogwa, aliyeiroga Afrika alishakufa au bado yupo hai, akicheka gizani?"
Alloyce, P.R.
 
Viongozi wa dini hakuna wengine.na hawa ndio vyanzo vya kuwakandamiza wengine.
Unakumbuka kipindi cha gadafi,amin na wengine
 
Umerudi tena? Khee!!! Ungeuliza viongozi wa Afrika nani kawaroga? Maana wana matumizi makubwa na utajiri uliotukuka kuliko hata hao viongozi wa nje wanaowakopesha na kuwapa misaada.

Wewe hakuna unachojua kuhusu hili bara, acha kuandika kwa mapenzi yako kwa mtu fulani. Siku familia yako ikiteketezwa utaandika haya? Hamna utu nyinyi watu wanapotea wana wazazi, ndugu, jamaa na marafiki. Hamuwafikirii, bora uuguze uzike. Kuliko mtu apotee kama hewa.

Acheni kudanganya watu, ongea ukweli. Mungu anachukia uongo. Wewe umeona viongozi wanavyoishi kama wafalme na malkia nenda kwa walipa kodi umeona watu walivyo? Mtu anashindia mlo mmoja nao kuupata ni sandakalawe.

Kuna umuhimu gani wa kununua magari ya gharama, posho kubwa, kutokatwa kodi, kupewa nyumba, mishahara mikubwa huku wananchi wengi wakihangaika kupata hata huo muhogo wa kuchemsha. Acheni hizi propaganda zenu hata Mungu hapendi acheni.
 
Ni kana kwamba kufanya yaliyo sahihi ni kosa. Je, Waafrika tumerogwa? Na kama kweli tumerogwa, aliyeiroga Afrika alishakufa au bado yupo hai, akicheka gizani?"
Waafrica ni WAJINGA, na kosa letu kubwa ni kuamini matatizo yetu yanasababishwa na watu wengine na tunaamini wakuyamaliza atatoka sehemu nyingine na kuja kututatulia matatizo yetu (TUNAMUACHIA MUNGU).

TUMEJIROGA WENYEWE.
 
TUTAKOMBOLEWA OOH OOH 🎶🎶

I KNOW YOU'RE HOPEFUL 🎶🎶

View: https://youtu.be/w9uBGWNiCQg?si=CsNpeLTpDBcoKJ-c

1080494.gif
 
Afrika buana! Hivi ni ugumu wa maisha au malezi magumu tuliyokuzwa nayo ndio umetufunga akili tusitambue jema? Bara hili pekee ndilo ambapo kiongozi anayeweka mbele maendeleo ya Taifa lake na kulinda maslahi ya wananchi wake huonekana adui, hupewa majina ya dikteta, mnywaji damu, mbaguzi, asiye na huruma, asiyetenda haki, hasa zile zinazohusiana na LGBTQ.

Ni kana kwamba kufanya yaliyo sahihi ni kosa. Je, Waafrika tumerogwa? Na kama kweli tumerogwa, aliyeiroga Afrika alishakufa au bado yupo hai, akicheka gizani?"
Alloyce, P.R.
kwa sababu unataka uishi mfumo wa wazungu ama?
 
Samia The Killer yuko kwenye hiyo list yako ya viongozi wazalendo? That’s all for now!
 
Umerudi tena? Khee!!! Ungeuliza viongozi wa Afrika nani kawaroga? Maana wana matumizi makubwa na utajiri uliotukuka kuliko hata hao viongozi wa nje wanaowakopesha na kuwapa misaada.

Wewe hakuna unachojua kuhusu hili bara, acha kuandika kwa mapenzi yako kwa mtu fulani. Siku familia yako ikiteketezwa utaandika haya? Hamna utu nyinyi watu wanapotea wana wazazi, ndugu, jamaa na marafiki. Hamuwafikirii, bora uuguze uzike. Kuliko mtu apotee kama hewa.

Acheni kudanganya watu, ongea ukweli. Mungu anachukia uongo. Wewe umeona viongozi wanavyoishi kama wafalme na malkia nenda kwa walipa kodi umeona watu walivyo? Mtu anashindia mlo mmoja nao kuupata ni sandakalawe.

Kuna umuhimu gani wa kununua magari ya gharama, posho kubwa, kutokatwa kodi, kupewa nyumba, mishahara mikubwa huku wananchi wengi wakihangaika kupata hata huo muhogo wa kuchemsha. Acheni hizi propaganda zenu hata Mungu hapendi acheni.
Bantu Lady kwa sasa umejitahidi ku comment kistaarabu na walau umejenga hoja. Endelea kujifunza zaidi kujenga hoja utakuwa bora sana.

Uliyonena sipingani nayo. Isipokua punguza kunituhumu au kuwatuhumu wasiohusika. 😂😂😂
 
Afrika buana! Hivi ni ugumu wa maisha au malezi magumu tuliyokuzwa nayo ndio umetufunga akili tusitambue jema? Bara hili pekee ndilo ambapo kiongozi anayeweka mbele maendeleo ya Taifa lake na kulinda maslahi ya wananchi wake huonekana adui, hupewa majina ya dikteta, mnywaji damu, mbaguzi, asiye na huruma, asiyetenda haki, hasa zile zinazohusiana na LGBTQ.

Ni kana kwamba kufanya yaliyo sahihi ni kosa. Je, Waafrika tumerogwa? Na kama kweli tumerogwa, aliyeiroga Afrika alishakufa au bado yupo hai, akicheka gizani?"
Alloyce, P.R.
waafrica wenyewe ndio wana wajibu muhimu, fursa na nafasi ya kulikomboa na kulijenga bara lao Africa na si vinginevyo 🐒
 
Bantu Lady kwa sasa umejitahidi ku comment kistaarabu na walau umejenga hoja. Endelea kujifunza zaidi kujenga hoja utakuwa bora sana.

Uliyonena sipingani nayo. Isipokua punguza kunituhumu au kuwatuhumu wasiohusika. 😂😂😂
Aisee wewe naona umenijua leo, pole. Unifundishe kujenga hoja wewe? Mimi nasimama kwenye Forums kubwa za ndani na nje na naongea. Hebu niache, mimi unavyokuja ndivyo navyokupokea. Wewe na huo ushamba wako nikutuhumu nini? Zaidi ya kukwambia acha kujipendekeza na uongo.
 
Afrika buana! Hivi ni ugumu wa maisha au malezi magumu tuliyokuzwa nayo ndio umetufunga akili tusitambue jema? Bara hili pekee ndilo ambapo kiongozi anayeweka mbele maendeleo ya Taifa lake na kulinda maslahi ya wananchi wake huonekana adui, hupewa majina ya dikteta, mnywaji damu, mbaguzi, asiye na huruma, asiyetenda haki, hasa zile zinazohusiana na LGBTQ.

Ni kana kwamba kufanya yaliyo sahihi ni kosa. Je, Waafrika tumerogwa? Na kama kweli tumerogwa, aliyeiroga Afrika alishakufa au bado yupo hai, akicheka gizani?"
Alloyce, P.R.
CCM itaikomboa Africa sio umeona askari wetu walivyo wema? Hata Mwangi alipakwa mafuta kabla ya kuingiziwa vitu huruma iliyoje. Nimemnukuu Mwangi mwenyewe
 
Punguza hukumu ambazo hauna nazo uhakika. Na wewe sio Mahakama kuhukumu watu. 😂😂😂
Anajihukumu mwenyewe, kwa matendo na maneno yake. Wewe unaishi sehemu gani ambayo imekutenga na yanayojiri Tanzania?
 
  • Thanks
Reactions: K11
Aisee wewe naona umenijua leo, pole. Unifundishe kujenga hoja wewe? Mimi nasimama kwenye Forums kubwa za ndani na nje na naongea. Hebu niache, mimi unavyokuja ndivyo navyokupokea. Wewe na huo ushamba wako nikutuhumu nini? Zaidi ya kukwambia acha kujipendekeza na uongo.
Sawa Bantu Lady, niishie hapo kwa leo kukujibu, ingawa sijakujibu ulivyotaka.
 
Aisee wewe naona umenijua leo, pole. Unifundishe kujenga hoja wewe? Mimi nasimama kwenye Forums kubwa za ndani na nje na naongea. Hebu niache, mimi unavyokuja ndivyo navyokupokea. Wewe na huo ushamba wako nikutuhumu nini? Zaidi ya kukwambia acha kujipendekeza na uongo.
Naomba unifundishe namna ya kusimama kwenye forum kubwa za nje huku nikiongea.

Pliz Niko chini ya miguu yako 🙏.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom