Nani wa kuchanganyikiwa? Mr a au mke wa mr b?

ANTA

Member
Nov 20, 2011
66
7
A na b ni marafiki, wote ni wanaume na wameoa. A kamtamani mke wa b. Kamtongoza, mke wa b kakubali kwa masharti ya kupewa tsh 100,000/=. Lakini a hana kitu cha kumhonga mke wa b. Kwa kuwa a na b ni marafiki. A anaamua kukopa tsh 100,000/= kutoka kwa rafiki yake b akimwambia anampeleka mtoto shule na atalipa baada ya siku 3. B alienda kuchukua hela alizomwachia mke wake atunze sh 100,000/= (note za 2000/= hamsini) ili akampe a amalize shida zake. A alipopewa hiyo hela, baada ya siku 3, a akaenda na kuzihonga kwa mke wa b na kupata mzigo. Wakati anaondoka b alimuona akiishia njiani akitoka nyumbani kwake. B alipofika akamuuliza mke wake, nani katoka hapa? Mke wake wakati akiwaza, mme wake akaendelea kumuuliza, mr a alishaleta hela yangu 100,000/=? Mke wake akashutuka sana, ikabidi aseme ndiyo. Akampatia mme wake hizo sh 100,000. Mr b akampigia a na kumwambia ahsante sana, taarifa zako nimezipata hapa home na hela nimeiona (akiimanisha salam na hela yake ameipata). Wakati mr b hajui chochote, mke wake yuko chumbani kachanganyikiwa akihisi mr a na b walimwekea mtego, na hela ni zile zile note 50 za buku mbili mbili. Mr a naye kachanganyikiwa akihisi mr b amemfahamu mchezo wake, na pengine anahisi mr b na mke wake walimwekea mtego. Huku mr b hajui lolote bali anafurahi kuona mr a karudisha hela zake kwa wakati. Je, mr a afanye nini, mke wa b aende wapi, na mr b akijua itakuwaje. Mke wa b na mr a wanaendelea kutumiana ujumbe wa matusi na wamekuwa maadui, kila mmoja anawaza kutoroka ili mr b asianzie kwake. Mh, itakuwaje?
 
Mr A na mke wa Mr B wote hawakupaswa kuchanganyikiwa kwasababu Mr B hawezi kwa njia yoyote akakubali kumtega mke wake au rafiki yake kwa kiwango cha kuacha wakafanya Mapenzi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom