Nani unahisi muuaji

Kizinga mpemba

Senior Member
Sep 23, 2018
178
250
#87
Ambiance kama mwezi hivi mjomba wangu alitoka sauzi akakutwa kafa ktk kiti na mlinzi mmasai asubuhi. Akiwa kaptula , Kaoshi na mguuni pekupeku.

Sisi hatuna habari kumbe akitoka sauzi kuna geust anafikia ila siku akakuta imejaa ,akachukua ya jirani na kwa Maelezo ya mwezake simu aliindondosha mpakani ktk kuitafuta mwenzie akamwambia achana nayo utanunua nyingine.

Maelezo mhudumu wa guest alipofika alimwomba simu haipigie demu wake maana hakuwa na simu. Mhudumu wa geust baada ya siku tatu hajarudi akabidi ampigie yule demu kwamwambia jamaa hana siku tatu hajarudi,na nguo kaacha naye akawajibu hata kwake hayupo ,baada ya siku kumi na name ndio anapiga simu sauzi mjomba(boyfriend wako) amuoni maana inasemekana alivyokuwa sauzi alimtumia milioni moja kabla ya kuja Dar ,hivyo alitumia hiyo namba kuwajulisha boyfriend wake amuoni ndio walioko sauzi wakatoa taarifa mjomba aonekani Dar.

Ndio jitihada za kumtafuta zikaanza bila mafanikio hospitali zote ndugu mmoja akapata wazo kwenda moja kwa mochwari mwananyamala mkamkuta naye akawa na wasiwasi labda sie ,akatafuta ndugu mwingene akathibitisha ndiye na Maelezo mhudumu wa mochwari aliletwa pale na polisi ipo pale siku ya kumi na name, toka wale ndugu wamuone ndio taratibu zikaanza za kumsafirisha ila, ikabidi ipelekwe muhimbili kwa uchunguzi kabla kuisafirisha.

Maana ilifika pale Muhimbili saa tatu asubuhi ila tulipewa SAA kumi na safari akaanzia hapo na SAA sita usiku tulifika home Tanga ,SAA NNE asubihi tulizika ila kifo chake mpaka Leo utata na polisi walichukua no ya demu wake ,rafiki yake waliotoka sauzi na Dada wa guest waliofikia na mmasai mlinzi ambiance alipofariki.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom