Nani tunapendana

Nani tunapendana

Lumbi9

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2014
Posts
8,750
Reaction score
12,473
SIMULIZI: NANI TUNAPENDANA?
MTUNZI: RICHARD ERASTO ONYANGO
SIMU: 0719 879608
******PATA UHONDO****
?Katika kitu ambacho sikukitegemea katika maisha yangu ni kukutana
na changamato ambazo ziliitaji utulivu wa akili na mwili ili kuweza
Kupambana nazo.....
Naitwa Richard Erasto Onyango nikiwa mtoto wa kwanza katika uzao
wa mama yangu, baba tayari akiwa na watoto wengine wakubwa kwa
wake zake wengine waliotangulia kuolewa kabla ya mama
yangu.Nilikutana na kitu ambacho sikukitegemea nilipokuwa nasoma
shule ya sekondari Benjamini William Mkapa nikiwa kidato cha
nne.Aha mpaka leo nikikumbuka huwa nashindwa kupata majibu ya
maswali tata ninayojiuliza kutokana na huo mkasa ulionikuta.?
Ilikuwa ni mwaka 2010 mwezi wa nane nikisomea masomo ya sayansi
katika shule hiyo iliyopo jijini Dar es salaam.Masomo yalikuwa
yakipamba moto siku baada ya siku tukijiandaa kufanya mitihan ya
taifa mwezi wa kumi na moja.
?Wewe ni kwanini unadiriki kufanya ujinga katika hii shule??
?Ujinga!Ujinga upi??
?Pumbavu kabisa yaani nakuuliza swali na wewe unanijibu swali.Kuja
hapa .? Darasa zima lilishituka baada ya kusikia sauti ya mwalimu
Mlokozi akimfokea mtu kwa sababu kila mwanafunzi alikuwa bize
kujisomea na wengine wakifundishana na kuelekezana mambo
mbalimbali waliyokuwa yanawatatiza katika masomo.Mshituko huo
ukamfanya kila mwanafunzi ajiulize ni nani anayefokewa lakini
hatukupata majibu tukabaki tukitizamana sisi kwa sisi na viulizo
nyusoni mwetu.Lakini baada kama ya dakika moja mwalimu huyo
anayesifika kwa ukali kuzunguka zunguka mle darasani alikuja
kusimama mbele yangu na kunikazia macho.
Darasa zima likawa linaniangalia mimi na kujikuta najishtukia na
kujiuliza swali lile niliulizwa mimi au lah ,nami nilipomuona
akiemdelea kunikazia macho ndipo nikamuuliza swali pia
ujinga,ujinga gani.
Aha ni kama nilimchokoza na kumpandisha hasira zake alifoka na
kunikamata kwa nguvu katika mkanda wa suruali na kunichomoa
katika kiti nilichokuwa nimekaa na kuniinua juu juu kwa kunipiga
Tanganyika jeki huku akiendelea kufoka na kunitoa nje. Wanafunzi
wote mle darasani wakapigwa na mshangao na kujiuliza maswali
ambayo walikosa majibu yake na wakaanza kutoka nje wakimfuata
mwalimu aliyekuwa akinipeleka nisipopajua.
?Si niliwaambia huyu kenge anajifanya anajua sana kwa sababu yeye
ni kichwa hapa shuleni .Namuuliza swali na yeye ananijibu swali
.?Mwalimu Mlokozi alikuwa anawaambia walimu wenzake baada ya
kunisukuma nisimame pembeni aliponiingiza katika ofisi ya
walimu.Ofisini humo kulkuwa na walimu wengi na waliposikia
mwalimu Mlokozi akinikashfu wakakasirika sana.
Muda huo mwalimu Mlokozi akawa anafungua vifungo vya shati lake
lenye mikono mirefu na kuanza kukunja mikono huku akiniangalia
kwa chuki.
Wanafunzi wa darasani mwangu walikuwa wamejazana kwa nje
kwenye madirisha ya ofisi hiyo kubwa wakitaka kufahamu sababu ya
mimi kupelekwa pale.Na sababu ya mwalimu Mlokozi kuniita kichwa
si kwamba nina kichwa kikubwa bali uwezo wangu darasani ni wa juu
mno.
Katika wanafunzi wote wa kidato cha nne mimi ndiye nilikuwa
nawaongoza kila muhula na ninapenda sana kuuliza maswali hata
kama jibu nalijua, hali hiyo ikafanywa nibatizwe jina la kichwa
wakimaanisha nina akili sana.
?Yaani wanafunzi kama hawa wananikera sana ,wakishajiona
wanaongoza mitihani wanajIfanya wanajua kuliko hata walimu wao
hasa huyu anajidaiga kuuliza uliza maswali mpaka anaboa.Anatoaga
mifano ya mambo yanayofanyika chumbani eti aonyeshe jinsi sayansi
inavyotendeka kati nguvu ya msuguano ,anakwambia no friction force
no life mfano eti wakati wa kufanya ngono nguvu ya msuguano ndiyo
inayonogesha tendo na kusababisha mbegu kutoka na mwanamke
kupata mimba kisha mtoto kuzaliwa na maisha kuendelea.Anakw
ambia maisha bila watoto kuzaliwa hayatakuwepo hivyo nguvu ya
msuguano ndiyo nayosababisha maisha yawepo.
?Alisema mwalimu wa kike aitwae Mage anayefundisha somo la
physics.
?Te te te te .?Walijikuta walimu na wanafunzi waliokuwa
wanachungulia madirishani kuangua vicheko.
?Sasa hiyo kanuni yake ya no friction force no life leo ndiyo
atatueleza ni kwa nini amemjaza mimba mwanafunzi wa
Jitegemee.?Alisema mwalimu Mlokozi.
?Ahaa!?Nilitoa mshangao huo, mkubwa mno huku nikijiziba mdomo
wangu na mkono wa kulia.
?Ahaa nini?Aha dawa ya meno.We si unajifanya kidume tuambie kwa
nini umeidhalilisha shule yetu kwa kumpa mimba msichana wa watu
wa Jitegemee.?
?Mwalimu ni nani huyo msichana??Nilimuuliza swali.
?Boya kabisa wewe unaniuliza mimi ?Kwani wakati unakwenda kuvua
bukta yako na kufanya nae mi nilikuwepo nawaona au
namfahamu??Alikaripia mwalimu Mlokozi.Nilibaki nimepigwa na
butwaa nisijue la kuongea na lini nimefanya mapenzi na msichana?
Na ni msichana gani huyo?Nikawa najiuliza maswali pasipo kupata
majibu na kila nilipowafikiria wasichana ninaofahamiana nao na
kuwa pamoja nao karibu hakuna hata mmoja anaesoma
Jitegemee.Nikawa najiuliza ni nani sasa sikupata jibu.
?kooo?Nilishitushwa na kwenzi nililopigwa kichwani na mwalinu huyo
baada ya kuniona mimi nipo kimya na nimekumbwa na mawazo
mengi kichwani.Nilishituka na bila kujitambua nikataka kukimbia
nikijua watu wabaya wanataka kunidhuru kumbe nipo ofisini kwa
walimu.Mwalimu kuona nataka kukimbia aliniwai na kunikamata na
kunirudisha lisha kunikalisha chini kabisa ili nisiweze
kutoroka.Wanafunzi wenzangu waliokuwa nje madirishani waliangua
vicheko viambatanavyo na masikitiko.
?Unataka kukimbia ehe sasa umechokoza moto.Kaa hapa chini ,haya
tuambie unamfahamu Neema??Mwalimu Mlokozi alinikalisha chini na
yeye kukaa juu ya meza mguu mmoja uking?inia na mwingine ukiwa
umegusa chini na kuniuliza swali.Niliposikia jina Neema moyo
ukanipiga paaa.
?Aha Neem ndo kasema hivi ?Na mbona Neema hasomo Jitegemee
bali Airwing?Sasa Neema yupi hapo?Mhm Neema ninayemjua mimi
ndiye kafanya hivi kweli?Aha nimekumbukaaaaaaaaaaaaaa, ndiyo ni
Neema huyo huyo kanisingizia lakini hasomi Jitegemee bali kuna
mchezo mchafu amenichezea , ndiyo ni mchezo kwa sababu alisema
atanikomesha.?Nilikuwa najiuliza maswali na kujijibu mwenyewe juu
ya huyo Neema aliyetajwa nikiwa nimekaa pale chini ofisi ya walimu.
Neema ni msichana tunaesoma nae pale keko majira ya usiku akiwa
anasoma shule ya sekondari Airwing inayomilikiwa na jeshi .
Hapo keko kuna kituo cha wanafunzi wanaorudia mitihani ya kidato
cha nne pamoja na kuwepo pre-form one kipindi darasa la saba
wanapomaliza elimu ya msingi hivyo majira ya usiku madarasa
yanakuwa wazi na mmiliki akaamua kuwaruhusu wanafunzi
mbalimbali wajisomee hapo kwa kulipia mchango kila mwezi.Kituo
hicho kinajulikana sana kwa jina la mto wa mbu au camp mbu.
Kunakuwepo na wanafunzi wengi wanaosoma shule mbalimbali na
hata wa vyuo wakiljisomea hapo usiku na mimi nikiwa mmoja
wapo.Ifikapo saa nne usiku wanafunzi wengi urejea makwao lakini
kuna baadhi ambao ni wasongo kama mimi tunakesha mpaka
asubuhi.
Nilikuwa maarufu sana hapo camp mbu kutokana na ucheshi wangu
na moyo mzuri wa kuwasaidia wanafunzi wenzangu masomo
mbalimbali kutokana na uwezo wangu mkubwa kiakili kwani nilikuwa
nasoma masomo kumi kwa ujumla mojawapo likiwa somo la
additional mathematics,somo ambalo wanafunzi wengi hawaliwezi na
linafundishwa kidato cha tano na sita kama pure mathematics.
Kulingana na sifa hizo nilifahamiana na wafunzi wengi na mmoja
wapo ni Neema mtoto wa mkuu wa gereza la keko lililo jirani na
tunapo soma.
ITAENDELEA
 
Nilikuwa maarufu sana hapo camp mbu
kutokana na ucheshi wangu na moyo mzuri
wa kuwasaidia wanafunzi wenzangu masomo
mbalimbali kutokana na uwezo wangu
mkubwa kiakili kwani nilikuwa nasoma
masomo kumi kwa ujumla mojawapo likiwa
somo la additional mathematics,somo ambalo
wanafunzi wengi hawaliwezi na linafundishwa
kidato cha tano na sita kama pure
mathematics.Kulingana na sifa hizo
nilifahamiana na wafunzi wengi na mmoja
wapo ni Neema mtoto wa mkuu wa gereza la
keko lililo jirani na tunapo soma.
ENDELEA?..
Katika hali nisiyoitegemea ,siku moja majira
ya saa tano usiku tukiwa camp mbu
tunajisomea Neema aliniomba twende Fammy
cafe ambayo ipo mtaa wa pili tukapate
vinywaji ,kutokana na mimi sikuwa mambo
safi mfukoni nikamwambia kuwa mimi sina
fedha alinijibu ataripa yeye,tukaenda.
Tukiwa tunakula na kunywa nilishituka kuhisi
mguu wangu unatekenywa na mguu wa mtu
uvunguni mwa meza ,nilipotazama nikauona
mguu wa Neema ukinipapasa papasa na
nilipomtazama usoni aliniangalia kwa macho
ya kurembua na kutamanisha akionyesha
hisia fulani lakini anashindwa kuongea.Nilibak
i namshangaa na ndipo alipouchukua mkono
wangu wa kulia na kuuvuta kwake kisha
kuhukisi midomoni mwake na kuniambai .
?Nakupenda sana Richie ,naomba uzisikilize
hisia zangu,nilikuwa natamani nikueleze siku
nyingi lakini ulionekana kuwa bize mno na
masomo lakini leo nakutamkia, nakuhitaji uwe
mpenzi wangu na si urafiki kama tulionao.?
Ahaa nilishangaa sana na kubaki
namwangalia tu hata hamu ya kula na
kunywa ikanitoka,kilichonifanya niwe hivyo ni
kwamba Neema ana mahusiano ya kimapenzi
na Erick,mwanafunzi anayesoma shule ya
sekondari ya Dar es salaam na uhusiano wao
unajuikana kwa kila mtu iweje Neema
anitamkie kuwa ananipenda wakati tayari
anampenz wake na ni rafiki yangu pia, si vita
vitaanza,tena vita vya mapenzi.
Ni vita hatari sana hivi,baki kusimuliwa na
kuwa msikilizaji au msomaji tu kama mimi
ninavyokusimulia lakini usiombe uingie
kwenye hivi vita. ?Wewe si mpenzi wa Erick na
kila mtu anajua hilo?Iweje unipende
mimi??Nilimuuliza swali huku
nikimshangaa.Mtoto huyo wa kike bila ya
woga wala aibu akaniambia.?
Erick kashapitwa na wakati,ni toleo la zamani
name moyo wangu umekupenda wewe kwa
sababu ni t oleo jipya.Usinitese Richie
nimekupenda nawe nipende tupendane
tufuraie maisha. Ka huyu ana kichaa eti Erick
ni toleo la zamani na mimi toleo jipya ina
maana siku hizi katika mapenzi kuna matoleo
mpya kama yalivyo magari na vitabu?Na mimi
siku nikiwa toleo la zamani naachwa kama
alivyoachwa Erick aha aha.
?Nilijiwazia na kucheka moyoni huku
nikimwangalia kwa mshangao sana.Nikaona
hapo sipo na mtu bali kichaa tena kichaa wa
mapenzi ,ni ugonjwa mbaya sana na hatari
kuliko hata dengue nikaamua niinuke li
niondoke zangu.Nilikuwa nampenda Neema
kama rafiki tukishilikiana katika masomo na
nilimuheshimu kama shemeji yangu kwani
nilifahamu ni mpenzi wa mtu lakini sikuwa
nampenda kimapenzi kwa sababu tayari ana
mpenzi wake na Erick ni rafiki yangu huwa
tunakaaga wote na kupiga soga pamoja na
kwenda kunywa kahawa na tangawizi kwa
shuba,muuza kahawa mtu mzima mwenye
tumbo kubwa na maneno mengi mdomoni
kuwavutia wateja.
Nikiwa nainuka Neema aliniwahi na
kuukamata mkono wangu wa kulia na bila
hata y kutegemea alinishika shingo yangu na
kunivutia kwake na kunikisi midomoni
mwangu .Yesu wangu kipind akinikisi ghafla
aliingia Rose akiwa ameshika glasi ya juisi
pamoja na sahani yenye chips ndani ya
chumba hicho ambacho kipo mwishoni kwani
cafe hiyo ina vyumba vyumba kwa ajili ya
wateja kukaa wanapopataka wao.
Rose alishituka sana kutuona tunakisihana
kumbe nalazimishwa kukihi ,glasi ya juice na
sahani ya chips zikamponyoka bila ya yeye
kujitambua kutokana na mshituko alioupata
,nami moyo wangu ulilipuka paaaaa baada ya
kumuona yeye. Rose ni msichana mrembo na
mzuri anayesoma shule ya sekondari
St.Antony tukiwa tunasoma nae hapo camp
mbu lakini yeye huwa anaondokaga saa tano
kwani anakaa magorofa ya jeshi katika kituo
cha daladala cha bora ,magorofa hayo yana
rangi nyeupe,baba yake akiwa na cheo cha
luteni kanali jeshini ,alikuwa ni mkali sana
kwa bintie hataki achezewe kabisa.Rose ana
uwezo mkubwa kimasomo lakini katika somo
la physics lilikuwa linamshinda kidogoi hivyo
mara nyingi alikuwa ananiomba nimfundishe
sehemu ambazo hakuzielewa.Katika
kufundishana kwetu tukajikuwa tukiwa
marafika na watani sana kwa sababu yeye ni
mhaya na mimi ni mjaluo kwani makabila
hayo ni mtu na mtani wke.
Kuna siku moja nikiwa najisomea majira ya
saa tano usiku nilimuona Rose akija nilpo na
aliponifikia akanikabidhi kikaratasi na
akaniomba nikisome baada ya yeye kuondoka
name nikatii alivyoniagiza.Ilipohitimu saa sita
nilikichukua kile kikaratasi na kukisoma dah
nilichokutana nacho humo nikagwaya nisijue
la kufanya.
?Richie naomba leo nikueleze ukweli kilichopo
moyoni mwangu .Ushirikiano wetu ni mzuri na
najivunia kuwa na rafiki kama wewe lakini
ndani ya urafiki wetu kuna chembe chembe za
upendo ambazo zinanitesa sana .Natambua
tunao upendo wa kirafiki lakin huu ni upendo
wa kimapenzi.Nakupenda sana Richie
mwenzio, unanitesa rohoni na moyoni naomba
uwe wangu tuuboreshe urafiki wetu.?
Yaani nilichoka kabisa hata hamu ya kusoma
ikanitoka.Huyu Rose ingawaje ni mtoto wa
mwanajeshi na ana cheo kikubwa tu jeshini
lakini nae ni binti wa starehe sana kwa
sababu kila jumamosi na jumapili ni mtu wa
kwenda club kujirusha kwa kudanganya
anakwenda kuwasalimia ndugu zao au hata
kwa kutoroka ikibidi ingawaje baba yake
anamchunga sana.Nilipata taarifa kuwa ana
mahusiano ya kimapenzi na mtoto wa mkuu
wa kambi ya jeshi ya mgulani kwa maana
hata picha zao nilikuwa naziona facebook
wakiwa katika mikao ya kimahaba na tayari
kijana huyo amehitimu mafunzo ya jeshi
baada ya kumaliza chuo na anasubiri
kupangiwa kambi ya kwenda kufanya kazi na
huwa anakujaga hapo camp mbu namwona
nae .
Siku hiyo ananiandikia kuwa ananipenda
nilishindwa kumwelewa . ?Hizi anataka
nipigwe na wanajeshi mimi ,nivunjwe miguu
kwa sababu baba yeke ni mjeda na mpenzi
wake ni mjeda na ni mtoto wa mjeda tena
anacheo cha mkuu wa kambi.Mamaaha mhm
naingizwa choo cha kike mwanao .?Niliikuwa
nawaza na kuwazua bila ya kuelewa
chochote.Ingekuwa kwa mtu mwingine
angefurahi sana kupendwa na Rose lakini
ukija kutazama hali halisi ni lazima
uchangayikiwe kwani utajiingiza katika
matatizo huku ukiyaona.
Siku iliyofuata Rosealikuja mahali
ninapopenda kukaaga na kuniuliza kama
nilikisoma kile kikaratasi ilinibidi nimwinue na
kutoka nae nje kwani sikutaka watu wasikie
nitakachomwambia. ?Hivi we Rose unataka
kunisababishia matatizo ?Wewe si una mpenzi
wako tena mjeda na baba yake ni mkuu wa
kambi unataka waniue??
Nilimuuliza kwa hasira kwani niliona
ananiletea mabala kama sio matatizo.
?Sikiliza Richie kwani mimi sikuvutii au sina
urembo wa kukushawishi niwe nawe,embu
angalia figure hii namba nane we unaogopa
wajeda acha ushamba wewe usione hatari nzi
kufia kweye kidonda?Rose alinijibu hivyo bila
haya kama kabila lake la kihaya. ?Khaa huyu
hamnazo nini mimi naongerea vitu vya maana
yeye anaongerea figure yake hakika naletewa
matatizo.?Nilijiambia moyoni.
?Sitaki usumbufu na matatizo .?Nilimwambia
vile nami nikaondoka kurudi ndani niendelee
kusoma kwani nilimuona kama
amechanganyikiwa lakini hata nilipoendelea
kusoma sikuelewa kitu ikanibidi niwaage rafiki
zangu Andunje na Sere kinyani wa ze komedy
ninaokaa nao room moja na kurudi getoni
kulala.
?Ni lazima nitakupat a tuu Richie kwani
unautesa sana moyo wangu.?Ulikuwa I ujumbe
mfupi ulioandikwa kwenye kikaratasi niliopewa
na Sere kinyani wa ze komedy aliporudi getoni
kuchukua daftari ili akasome na kuniambia
kapewa na Rose aniletee.
*****ITAENDELEA ****
 
?Ni lazima nitakupat a tuu Richie kwani
unautesa sana moyo wangu.?Ulikuwa I ujumbe
mfupi ulioandikwa kwenye kikaratasi niliopewa
na Sere kinyani wa ze komedy aliporudi getoni
kuchukua daftari ili akasome na kuniambia
kapewa na Rose aniletee.
ENDELEA?.
?Mpuuzi nini mimi nimempenda kirafiki lakini
si kimapenzi ,sasa anataka kunisababishia
vita na wajeda .?Niliongea kwa sauti huku
Sere kinyani wa ze komedy akiniangalia na
kunishangaa kisha kuondoka kurejea camp
mbu.
Nikiwa getoni nimejiegesha tu kwani hata
usingizi nilikuwa siupati ,nilishituka kuona
mlango ukifunguliwa na miguu ya msichana
ikiingia, alipoingiza uso wake nikamtambua ni
Nora . ?Pole Richie nimeambiwa unaumwa na
Andunje nikaamua nije kukuona.?Alisema
Nora kumbe Andunje alimdanganya kuwa
naumwa baada ya yeye kunitafuta camp mbu
na kutoniona akaenda kuniulizia kwa Andunje
na kuelekezwa nilipo.
Nora ni msichana anayesoma shule ya
sekondari ya Zanaki akiwa nae kidato cha nne
na pia anaishi nyumba hiyo hiyo hapo camp
mbu tunaposomea.Ni mtoto wa mama
mwenye nyumba na mjomba wake ndiye
anayefundisha hapo.
Nilizoeana nae na kuwa marafiki kutokana na
kaka zake wawii niliwahi kusoma nao tuition
moja kule Ilala na mda huo ninasoma na kaka
yake mkubwa Mark shule moja Benjamini
hivyo kujuana na kaka zake ikanifanya nijuane
nae na kuwa marafiki.
Kama kawaida mtu anapokuwa na akili sana
kimasomo basi marafiki huwa wengi na yeye
Nora akawa ananiletea maswali mbalimbali
nimfundishe lakini hata yeye anapenda kulala
saa tano hivyo huwa hakeshi. Siku moja
nilikuwa nimelala chumba cha mwisho usiku
wa saa tisa nikiwa peke yangu na mvua
inanyesha kwani wanafunzi waliondoka na
hata marafiki zangu walirudi getoni.Nilishit
uka mtu akinipapasa na kutaka kuninyonya
ndimi .
Nilikurupuka na kukuta taa zimezimwa,nikaj
ua nanyonywa ndimi na jinni mahaba na mtu
yule akinivuta kwake na kuniambia nitulie
nisipige kelele na nilipompapasa
nikamtambua ni msichana nikajiambia leo
nimevamiwa na jini la kike na kujikuta najuta
kubaki peke yangu eneo hilo lakini nikaamua
niwashe taa nimjue huyo msichana ni nani.
Aha nilipowasha taa nikamuona msichana
akiwa ndani ya kanga moja tu hata kufuri
hajavaa akinitaka nizime taa na nisipige
kelele nikawa nadhani ni mchawi alikuja
kuniroga na kutaka kupiga kelele kuwa kuna
mchawi ananiroga mle darasani.Kama yule
msichana aliyajua mawazo yangu nilipotaka
kufungua tu mdomo nipige kelele aliniwahi na
kunifunga kasha kuniambia nisipige
kelele.Lakini nilipomwangalia vizuri
nikamtambua ni Nora.
Nilipomuuliza mbona yupo vile akaniambia
alibanwa na haja ndogo na kutaka kutoka nje
kwenda chooni kujisaidia kwani choo cha
ndani kilikuwa kmeharibika na alipofika
mlango wa uwani wa nyumba yao akakuta
mlango umefungwa kwa kufuri na hakujua
funguo zilipo au anazo nani kwani nyumba
hiyo wanaishi watu wengi na kuamuakupitia
mlango wa mbele ambapo ni lazima apite
katika madarasa yaliyozunguka nyumba yao
na ndipo hapo alipojua kuwa mvua inanyesha
na pia hakukuwa na mwanafunzi yeyote.
Alipofika darasa la mwisho ili atokee uwani na
kwenda chooni alisikia mtu akikoloma na
akapatwa na shauku ya kumjua huyo mtu na
kuamua kuingia ndani ya hilo darasa na
kunikuta nimelala.Alifurahi sana kuniona
nimelala kwa haraka haraka akaenda kuzima
taa na kuja kunipapasa na kutaka kuninyonya
ndimi name nikashituka.
Mara tukasikia mtu akitembea akielekea
mlango wa kutokea uwani ambapo nilazima
apite karibu na hilo darasa tulimokuwa. Kwa
haraka sana nikazima taa na kwenda
kujibanza mwisho kabisa mwa ukuta huku
wote tukiwa tunatetemeka vibaya mno kwani
tulimsikia mtu huyoakikohoa na kuitambua
sauti yake ni ya mjomba wake kwani nae
anaishi hapo hapo.
Bahati mbaya mjomba wake alipofika darasa
hilo akielekea uwani na kushituka mbona
darasa hilo tu limezimwa taa na mengine yote
yamewashwa ikambidi aingie na kuwasha taa
ya darasa hilo huku akifoka ?Pumbavu kabisa
hawa wanafunzi wajinga kabisa hawajui kuwa
serikali za mitaa wameniambiia madarasa
yote yawe yanawashwa taa usiku kucha ili
kama kutatokea tatizo watu waone na
msaada utolewe kwa haraka?? Mlipuko moyoni
uliotupata ulikuwa si wa kawaida tulisikia
paaaaaaaaaa na tukitetemeka zaidi hata ya
mwanzo huku mimi nimefumba macho na
nikimuomba mungu kimoyo moyo mjomba
wake asituone wakati akiwasha taa.
Kweli Mungu ni mwema ndugu yangu
akayasikia mapombi yangu na mjomba wake
baada ya kuwasha taa akaondoka bila hata
ya kutuona na kuelekea uwani na baada kama
ya sekunde kuni tukasikia akifungua mlango
wa kuingilia chooni kwanii upo karibu na
darasa hilo na kisha kuufunga.Kwa haraka
sana nikabeba begi langu na kuondoka nae
Nora akatoka na kuingia ndani kwao hata ule
mkojo uliombana haukuwepo tena chezea
kufumaniwa wewe shauri yako utajikuta
umekuwa mdodgo kama punje ya mchanga.
Siku zikawa zinakwenda na Nora akwa
ananisumbua kunitaka kimapenzi akidai
ananipenda sana lakini mimi nikawa
namkwepa kwa sababu nilipata tetesi kuwa
Nora anatoka kimapenzi na mwalimu
mwingine anayefundisha hapo kisirisiri lakini
mimi mwenyewe siku moja niliwaona bila wao
kuniona wakiingia gesti iliyokuwepo jirani na
hapo camp mbu bila ya kuogopa kuwa
wataonwa kwani ilikuwa ni saa sita usiku na
mimi nilikuwa natoka kuchukua daftari kwa
rafiki yangu anayeishi katika magorofa ya
jeshi yaliyopo barabarani karibu na njia
panda ya kuelekea uwanja wa taifa na shule
ya msingi Mgulani.
Halafu ananitaka mimi tena ,nikajiambia
haitowezekana kwani kwa jinsi ninavyomjua
yule mwalimu ni mtu wa kubadilisha
wasichana kama gesti anazozibadilisha
anapokwenda kufanya nao ngono.
?Nimeshapoa.?Nikamjibu kwa mkato na
kugeuza uso wangu kuangaliaukutani kwani
nilimuona ni mchawi amekuja kuniroga.Bila
hata ya aibu wala soni akavua nguo zake zote
na kunifuata nilipolala na kuanza
kunitomasatomasa wakati ameshaambiwa
kuwa mimi ninaumwa.Nilishituka nikamkuta
ameshanikalia juu ya mwili wangu
akinipapasa papasa.Aha nilipotaka kumtoa
lakini akawa mbishi na nilipotaka kutumia
nguvu akanigandamiza kwa nguvu nikajikuta
sina ujanja lakini sikutaka kukubali kushindwa
kumtoa nikaamua kupambana nae.
Ikawa purukushani tukibiringishana hapo
kitandani mimi nikitaka nimtoe yeye akitaka
kunikumbatia ili tufanye ngono.Ghafla bin vuh
mlango wa chumba ukafunguliwa na akaingia
Rose na kutukuta tukibiringishana na Nora
akijua tunachezeana kwa ajili ya kujiandaa
tufanye ngono.Tulipigwa na butwaa kwa
mshituko tulioupata na Rosekuanza kufoka.
?Kumbe wewe Malaya ndiye mwizi ,unawaibia
watu wapenzi wao.?Nora kuambiwa yeye
mwizi alikasirika sana na kutaka kuinuka
akiwa uchi wa mnyama apambane na Rose
lakini Rose kama aliyasoma mawazo ya Nora
kwa haraka na bila ya kutegemea alichukua
stuli iliyopo humo getoni na kumpiga nayo
Nora kichwani na kumfanya apate
mshitukomkubwa sana na kudondoka chini k
\isha kupoteza fahamu.Nilishituka tena mara
mbili ya nwanzo nikijua Rose kaua. ?Rose
umeua?Nilimwambia Rose.
?Mwache afe mwizi mkubwa huyo.?Alijibu
Rose kwa hasira na kisha kufungua mlango
na kutoka.Ilikuwa ni kizaa zaa kweli kweli
nilipouona mwili wa Nora uchi wa mnyama
ukiwa chini umedondoka amepoteza
fahamu.Nilijiuliza nifanye ni ni niokoe maisha
ya Nora au nikimbie yaani nilichanganyiki
wa.Akili iliyonijia haraka haraka niufunike
mwili wa Nora kwa shuka na kisha kuchukua
ndoo yenye maji na kumwagia mwilimi mwake
ndipo akashituka na kurejewa na fahamu .Dah
nilimshukuru Mungu sana kwani nilijua Nora
ameshakufa na mimi ningeonekana
nimemuua.
*****ITAENDELEA*****
 
ENDELEA?.
Baada ya dakika kumi aliva nguo zake na
kuondoka nami nikaanza kazi ya kuondoa
maji niliyommwagia Nora ndani humo. Vita
vikaanza kati ya Rose na Nora ,mara kwa
mara wanapoonana walikuwa wanatupiana
maneno makali sna na hata matusi ya nguoni
na muda mwingine wakawa wanapigana
kabisa na kuumizana.
Kuliibuka migogoro mikubwa sana kati ya
baba yake na mpenzi wake Rose
wakiniandama mimi na mara kwa mara
walikuwa wanakuja hapo camp mbu tena na
magwanda na magari ya jeshi kunitisha kwani
Rose alibadilika mno kwa sababu yangu
baada ya kugundua kuwa mimi ndiye chanzo.
Hata mjomba wake na Nora nae akafahamu
kuwa Nora amekuwa mtu wa hasir hasira na
alipofanya uchunguzi akajua mimi ndiye
niliyesababisha hivyo na kunionya niachane
na mpwa wake ama sivyo atanifukuza na
kunipiga marufuku kusoma hapo camp mbu.
Na siku hiyo ndiyo Rose alitukuta mimi na
Neema mle fammy caf? na kulianzisha
varangati kubwa sana.Rose alianza kumpiga
Neema nae Neema hakukubali kupigwa
akaanza kumpiga Rose.Aise ugomvi ulikuwa
mkubwa sana na kila nilipojitahidi
kuwaachanisha ilishindikana huku
wakitupiana matusi mazito na kuwafanya
watu wakajaa na ndipo wahudumu wa kiume
wakaja kugombelezea lakini tayari walikuwa
wameshaumizana .
Habari za ugomvi huo zilienea eneo lote la
camp mbu mpaka Nora na Erick
wakajua.Kesho yake baba yake na Rose
alikuja hapo camp mbu akiwa na bastola
mkononi kutaka kunipiga risasi,wanafunzi
kuona bastola imeshikwa mkononi kila mmoja
akatoka nduki kuokoa maisha yake lakini
marafiki zangu wakanitonya na kukimbia kwa
sababu nilikuwa nimekaa darasa la mwisho
kwenye kona mwishoni kabisa mwa darasa
hilo.
Mpenzi wa Rose akawa ananisaka kwa udi na
uvumba na siku ya tatu yake alikuja getoni
mwetu usiku baada ya kuelekezwa ninapoishi
.Rafiki yangu alipomuona anapaki gari la
jeshi nje ya nyumba alikuja haraka na
kunijulisha kwani alishamwonaga akija pale
camp mbu kunitafuta na mim i
sikuchelewesha muda nitatoka nduki kwa
kupitia mlango wa nyuma.
Erick hakawa hatupatani tena ,akawa
ananichukia vibaya mno na kila tulipokuwa
tunaonana alitaka kuanzisha ugomvi lakini
nilijitahidi kutopigana na hata marafki
wengine wakawa wanagombelezea.Yule
mwalimu mpenzi wa Nora nae akashangaa
kuona mabadiliko ya mpenzi wake na
alipofanya upelelezi akagundua mimi
nimembadilisha mpenzi wake.
Akaanza kunipaka majungu na kashfa kwa
mjomba wa Nora anifukuze na anipige
marufuku mimi kusoma hapo kwani
ninawaalibu mabinti wanaosoma hapo na
kukipa kituo chao sifa mbaya ya umalaya
wakati yeye ndiye malaya wa kiume hana hata
haya.Yule mwalimu kila aliponiona akawa
ananitishia kunidhuru .
Baada ya wiki mbili wale wasichana wakawa
wananifuata kila mmoja na muda wake kwani
nilikuwa siendi tena kusoma camp mbu baada
ya mjomba wake na Nora kunifukuza kwani
Nora alikuwa amwelewi anampomkanya
kuhusu mimi lakini hakujua kuwa Nora
anatembea na mwalimu wake msaidizi
,angejua wala asingeangaika na mimi kwani
mbaya wake anayemwaribia mpwa wake ni
mwalimu mwenzie.
Wasichana hao walinibembeleza niwakubalie
lakini wapi nikawakatalia ,walikasirika sana
na kuahidi kunitenda vibaya hasa Neema .
?Wewe fisadi wa mapenzi unawaza nini wakati
tunataka utueleze Neema ni nani??Nilishitu
shwa na swali la mwalimu Mlokozi aliloliuliza
kwa ukali na kuniondoa katika kumbukumbu
niliyokuwa inapita ubongoni mwangu.Nilijiku
ta jasho linanitoka na kuwa na hofu moyoni .
Nikaanza kuwaangali watu waliokuwemo
humo ndani ofisini na kabla sijamamiliza
kuangalia. ?Unamwangalia nani ?Unazani
Neema atakuwa hapa?Neema yupo polisi
baba yake kampeleka kufungua kesi ili
upelekwe mahakamani kushitakiwa kwa
kumjaza mimba binti yake.?Aliuliza Mwalimu
Mlokozi na kufafanua. ?Paaaa .?Moyo
ulilipuka vibaya sana kusikia taarifa
hiyo.Nikajua sasa naingia matatizoni ikabidi
niwe muwazi na kuwaeleza kila kitu na
kuwafanya walimu wote washangae pamoja
na wanafunzi wenzangu.
?Ina maana kuwa huu ni mchezo
umechezwa??Mwalimu wa kike alimuuliza
mwalimu Mlokozi. ?Yaah itakuwa
hivyo.?Alijibu mwalimu Mlokozi na akionekana
ameguswa sana na nilichokielezea. ?Pole sana
nenda darasani tuachie sisi walimu wako
tutakusaidia.?Alisema mwalimu mwingine
nami nikaondoka kurejea darasani huku
wanafunzi wenzangu wakinipa pole na
kusikitika sana.
Baada ya wiki moja walimu watatu walileta
majibu ya uchunguzi wao na kugundulika
kuwa ni mchezo ulichezwa na wale wasichana
watatu kwani wote ni marafiki hata kabla
migogoro haijatokea na wakashirikiana na
wapenzi wao ili kunikomoa mimi nifungwe jera
ndipo wakaenda kwa daktari na kufoji vyeti
kuwa Neema ni mjamzito wa miezi miwili na
mimba hiyo nimempa mimi huku yule
mwalimu anayetembea na Nora akijidai ndiye
mzazi wa Neema na mpenzi wa Roseambae
nimjeda akitoa pesa kuuratibuhuo mchezo
mchafu bila ya wazazi wa hao wasichana
kujua kuwa kuna mchezo unachezwa juu
yangu.
Walipokamilisha kila kitu wakaenda katika
kampuni inayochapisha magazeti ya udaku na
kuwaonga wanichafulie jina langu na wao
wakakubali bila ya kufanya uchunguzi
wowote.
Gazeti lilipotoka lilikuwa na picha yangu
mbele ya gazeti huku picha ya mwanafunzi wa
kike ikiwa imefichwa sura yako kukiambatana
na maneno yaliyoandikwa kwa herufi kubwa
?GENEOUS AMJAZA MIMBA DENTI MWENZIE
NA KUIKATAA.?Kisha kufuatiwa na mandishi
madogo chini yake.?
Aliyejaza anasoma B.W.Mkapa high
school,ana akili balaa,eti alimshawishi denti
wa kike wafanye ngono kipractiacal ili waone
jinsi mimba inavyopatikana kama
wanavyofundishwa shuleni.?Kumbe gazeti hilo
lilisomwa na walimu na ndilo liliwashitua na
kumfanya mwalimu Mlokozi kuja kunifuata
siku ile darasani na kunipeleka ofisini.
Na wala Neema hakutaja gazetini shule halisi
aliyokuwa anasoma bali walitaja Jitegemee ili
asisababishe matatizo yuleni mwao
Nilisikitika sana kusikia hivo lakini
nikamwachia Mungu kila kitu.Wakuu wa shule
ya Benjamini na Jitegemee hawakukubali
kuchafuliwa jina la shule zao wakaamua
kufungua kesi mahakamani.Walikamatwa
wote wahusika pamoja na gazeti lililochapa
habari hiyo na daktari aliyefoji cheti cha
mimba ya Neema.
Neema,Rose na Nora walipohojiwa ni kwa nini
walinifanyia hivy ndipo wakasema kuwa wao
ni marafiki sana na kila mmoja ana mpenzi
wake,wakiwa wanapiga soga na kuongea
umbea kama kawaida ya wanawake
waliwasikia marafiki zangu Andunje na Sere
kinyani wa ze komedy wakiongea chumba cha
pili pale camp mbu kuwa mimi nina muhogo
mrefu balaa .
Kusikia hivyo wakawa wanatamani na kuwa
na hamu ya kukutana nami ili wauone ndipo
kila mmoja akawa ananiwinda kwa udi na
uvumba .Wakawa wakinionea wivu wakiniona
nikiwa na msichana kiasi kwamba hata wao
kwa wao marafiki wakajikuta wanaoneana
wivu na kujenga ushindani wa kunipata kwa
hali na mali.Mahakama ikatoa hukumu ya kila
mmoja alipe shilingi laki tano kama faini ya
kuchafua majina ya shule na langu la sivyo
wakatumikie kifungo jela kwa muda wa miezi
sita kila mmoja ikawabidi walipe.
Shule walizokuwa wanasoma zikawafukuza
ikawapasa wakae nyumbani wakisubiri mwaka
unaofuata warudie kidato cha nne katika shule
zingine za private mikoani.
Mpaka kesi inamalizika ilikuwa imebaki wiki
moja kuanza kwa mitihani ya taifa .Nilisoma
kwa haraka haraka na baada ya wiki
tukafanya mitihani na matokeo yalipotoka
nikawa wa kwanza Tanzania nzima na
kuchaguliwa kwenda kusoma shule ya
sekondari Mzumbe. Swali ninalojiuliza mpaka
sasa nani nilimpenda na yupi alinipenda?
*****MWISHO*****MWISHO****
 
Ni mwaka gani huo?
vp Matokeo ya kidato cha IV tayari?
maana si utani mkia uliutembeza sana
na wao walikumaliza
HONGERA kwa mtiririko wa uandishi maana imefuatana hadi mwisho tofauti na kina chau CHUNGU na kina Mzizi MKAVU
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom