Habari wanajamvi .
Naleta mada tajwa hapo juu tujadili pamoja kwa hoja.
Nikianza na Raisi wa awamu ya kwanza huyu alikuwa muhimu sana kwa kuwa tanzania ndo ilikuwa inajenga msingi.
Ukiangalia kiufundi msingi wa Tanzania ulijengwa kwa tope na kupakwa rangi.
Nasema hivo kwa sababu baada ya Uhuru bado mwalimu hakujibidiisha na kuwawezesha wananchii kujitawala kama ilivyokuwa lengo la kupigania Uhuru.
Na hata ukiangalia ishu ya muungano bado unaona wananchi hawajashirikishwa kikamilifu ndo maana mpaka sasa bado kuna utata mkubwa wa huu muungano. Kwa ufupi utawala wa awamu ya kwanza haukujenga misingi imara ya kidemokrasia na kuwapa mamlaka wananchi. Kwa hiyo unakosa vigezo vya kupata point.
Awamu ya pili napo hakuna jipya lilifanyika badala yake kila kitu kilibaki vilevile. Kwa hiyo nao wanakosa alama au points.
Awamu ya 3 walivunja misingi ya kidemokrasia kwa kuvuruga Chaguzi na tume nzima ya uchaguzi. Hapa tume nzima ya uchaguzi ikajaa makada wa chama kimoja. Wananchi hawakuwa na sauti kabisaa kwenye nchi Yao kwa hiyo awamu ya 3 nao wanakosa point.
Awamu ya 5 nao walivunja rekodi ya kutoheshimu wananchii na kuwachagulia viongozi waziwazi na mihimili mingine ya dola ikamezwa kabisa.
Awamu ya 6 bado tunawaangalia kwa jicho la mwewe ili tuone kama watabadilisha mwelekeo kwa Sababu mpaka sasa bado hawajafanya jipya tofauti na watangulizi wao tajwa hapo juu.
Mshindi wetu kwa alama 75%%ni jakaya mrisho kikwete kwa kuthubutu kutuletea rasimu ya jaji warioba. Watanzania wengi wamekuwa hawampongezi kikwete bali anapongezwa warioba.
Naomba vijana mpiganie rasimu ya Warioba iingie mezani ipitishwe kwa kura za ndio 💯 Kikwete ameshatupa hii zawadi sasa kazi yetu kuikamilisha.
Ahsanten sana.