Nani ni nani urais wa JMT 2025 kati ya Dr. Kalemani, Paul Makonda na Dr. Shein?

Hakuna hata mmoja hapo. Kilichopo Watanzania wote tusali sana kila mtu na imani yake. Yaani tusali sana.
 
Muondoe Dr Shein kwenye hiyo list
Umofia kwenu wadau wa JF siasa.

Tetesi zipo japo mnaweza kubisha ila mtanikumbuka 2025, kuwa wagombea urais ndani ya CCM watakaotikisa ni Dr Medard Kalemani waziri wa Nishati, RC Makonda na Dr shein Rais wa sasa wa Zanzibar.

Habari za udaku kutoka ktk medani ya siasa nchini inamtaja Dr shein kuwa mtu mwenye sura ya upole lakini anayeweza kuhimili siasa za JMT kwani ni Makini na mkali mno tofauti tumuonavyo.

Waziri Dr Kalemani anatajwa kubebwa na sifa ya usambazaji umeme kwa vijiji vyote hadi kwenye tembe huku Tanzania ikiwa nchi ya kwanza Africa kutoa huduma hiyo kwa wananchi wake.

RC Dar Paul Makonda anatajwa kuwa ni mtu mbunifu ktk uongozi wa kutatua shida za watu na mtu mwenye uvumilivu zaidi ya hata Lowassa kutokana na kuhimili kejeli na matusi kutoka kwa watu wanaomchukia waliotapakaa kote nchini. Inadaiwa Dar ama Mzizima haijawahi na haitakaa impate RC kama huyu.

Chanzo changu nyeti serikalini kimenijuza Rais yupo hapo juu miongoni mwa watatu na nasubiri Uzi huu kufukuliwa November 2025.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
2025 Huenda akawa Mgogo mmoja ambae Ni Prof wa Sheria

Huyo Mgogo ni mzalendo tu na yuko pale kwa sababu ya kuitikia wito wa kumsaidia majukumu ya uwaziri Mh. Rais. Mgogo siyo mwanasiasa as such, ni mzalendo tu. Mtu anayetakiwa kugombea 2025 ni yule ambaye ana qualities zote mbili, za uanasiasa na uzalendo pia, kama alivyo JPM mwenyewe.
 
Naona kuna ukweli kwa mbali, ila Dr. Shein atakwazwa na sheria mpya ya vyama vya siasa kuhusu umri, lkn hilo huenda lisiwepo kwani itakuwa imeshafanyiwa marekebisho kwani lengo la sheria hiyo, wakati huo, litakuwa limekamilika. Hii ndio Tanzania yetu.
 
Umofia kwenu wadau wa JF siasa.

Tetesi zipo japo mnaweza kubisha ila mtanikumbuka 2025, kuwa wagombea urais ndani ya CCM watakaotikisa ni Dr Medard Kalemani waziri wa Nishati, RC Makonda na Dr shein Rais wa sasa wa Zanzibar.

Habari za udaku kutoka ktk medani ya siasa nchini inamtaja Dr shein kuwa mtu mwenye sura ya upole lakini anayeweza kuhimili siasa za JMT kwani ni Makini na mkali mno tofauti tumuonavyo.

Waziri Dr Kalemani anatajwa kubebwa na sifa ya usambazaji umeme kwa vijiji vyote hadi kwenye tembe huku Tanzania ikiwa nchi ya kwanza Africa kutoa huduma hiyo kwa wananchi wake.

RC Dar Paul Makonda anatajwa kuwa ni mtu mbunifu ktk uongozi wa kutatua shida za watu na mtu mwenye uvumilivu zaidi ya hata Lowassa kutokana na kuhimili kejeli na matusi kutoka kwa watu wanaomchukia waliotapakaa kote nchini. Inadaiwa Dar ama Mzizima haijawahi na haitakaa impate RC kama huyu.

Chanzo changu nyeti serikalini kimenijuza Rais yupo hapo juu miongoni mwa watatu na nasubiri Uzi huu kufukuliwa November 2025.
Kwani Shein naye ni mtanganyika Hadi agombee urais wa jamuhuri au na yy km kina mzee mwinyi wanzanzibara

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom