Nani ni mmiliki wa Channel 10?

Tabia ya kutetea ubaguzi kwa misingi ya rangi ikome kabisa hapa JF mmiliki wa vyombo habari ana haki ya kutangaza chochote na kuacha chochote kutegemeana na muda uliopo (air time) na maslahi yake ya kibiashara pamoja na ethics za uandishi! kutokutamgaza magazeti ya mengi kati ya magazeti yote nchini siyo big deal?? who is he? mengi naye fisadi tu tena nyangumi so sijaona unachotetea hapo

Tumain,

Umetumwa na nani????? Mbona unaonekana kama vile una agenda ya siri? Usiiaibishe JF please!!!!!!

Tiba
 
Wewe unayeuliza anayemiliki so what? kwa magazeti ya mengi yasipotajwa what is a deal?? (magazeti ya mengi yana umuhimu kwako kanunue) kwa chanel 10 siyo muhimu???
Utawajua walionunuliwa na watu mlima mrefu.

samahani kama nimekuudhi ndugu kwa kuuliza kwangu,lakini ilikuwa sio lazima kwa wewe kujibu hayo uliyoyajibu
 
samahani kama nimekuudhi ndugu kwa kuuliza kwangu,lakini ilikuwa sio lazima kwa wewe kujibu hayo uliyoyajibu
Huwezi kuniudhi mimi kwakuwa mimi si mmiliki wa channel 10, vilevile huwezi kunipangia namna ya kujibu kwasababu niko huru ku-question credibility ya swali lako...limekaa kama magazeti ya mengi are so important to US than magazeti mengine? ndio maana nakuhoji una interest gani na mengi??? who is he???
 
Kuhusu swali lako "Nani mmiliki wa Channel 10" ni kwamba channel hii ina historia ya kumilikiwa na mafisadi na matapeli wa kimataifa. Aliyeanzisha ni Muitaliano mmoia --wa kundi la Mafia -- Franco Tramontano aliypewa uraia wa Tanzania na utawala wa Mkapa baada ya serikali kuikatalia serikali ya Belgium kum-extradite kwenda kusimama kizimbani kwa wizi wa USD 2 milioni zilizokuwa za msaada kwa Tanzania na ambazo alizitumia kuanzisha Channel 10. Hiyo ilikuwa mwishoni mwa 1990s.

Akaiuza kwa Tanil Somaya -- Mtuhumiwa wa ufisadi wa radar na sasa tunasikia mtuhumiwa wa ufisadi wa Kagoda -- RA kanunua hisa nyingi. Hawa wanahisa kazi yao kubwa ni kuibomoa TV ya mzalendo Mengi baada ya kufanikiwa kuwaweka mfukoni maafisa wa TCRA na Waziri wa Habari. Hapa Tanzania tunakwenda vizuri sana.

Hiyo ndiyo historia fupi ya Channel 10 ambao nao hawasomi kabisa magazeti ya IPP Media.

Kwa kuongezea tu serkali ya Mkapa ilimpa uraia Muititaliano Tramontano mwezi uleule aliyomnyang'anya Jenerali Ulimwengu uraia. Hii ni pamoja na mmafia huyo kuiba hela za msaada zilizokuwa zikija Tanzania.
 
Huwezi kuniudhi mimi kwakuwa mimi si mmiliki wa channel 10, ....
Sasa kama wewe si mmiliki, jazba za nini? Mbona swali linaeleweka tuu?
gabu-albums-mapicha-picture537-bombface.jpg
 
Last edited:
Huyu mshikaji Tumaini ana matatizo gani? Kwa nini usikae kimya kama huna jibu? Tafadhali jiheshimu na heshimu wana JF na omba radhi.Mmiliki ni Rostam na inasemekana alinunua vyombo vya habari baada ya saga la richmond ili kutumia vyombo hivyo kujisafisha yeye na Lowasa.
 
To be fair, labda tuseme Mengi ndio kaanza haka ka-mchezo ka kutokusoma magazeti ya wenzake. Sina uhakika nani alianza, lakini ukweli ni kwamba ITV au Redio One hawachambui magazeti mengine zaidi yao. Zamani walikuwa wanachambua, lakini sasa hamna kitu.Wanachambua magazeti ya IPP Media tu.

Kwa uchambuzi wa magazeti, sikiliza Clouds FM 88.4 in Dar, 87.8 in Mbeya.

I LIKE THIS
Unajua mtu ukiwa BIASED ni sawa na KIPOFU wa FIKRA

Huwezi kuniudhi mimi kwakuwa mimi si mmiliki wa channel 10, vilevile huwezi kunipangia namna ya kujibu kwasababu niko huru ku-question credibility ya swali lako...limekaa kama magazeti ya mengi are so important to US than magazeti mengine? ndio maana nakuhoji una interest gani na mengi??? who is he???

kwa mara ya KWANZA nakuunga mkono mzee wa JIHAD.....
 
Katika taarifa za habari ambazo nikizikosa huwa nasikitika ni za C10. Vipindi vyao vya mahojiano ni vizuri mno, wamiliki hawajinadi sana kwenye channel hii. Mnakumbuka walivyotangaza matokeo ya KWELI ya URAIS wa Zanzibar 1995?
 
si magazeti ya kampuni zake tu yanayokosa nafasi katika channel 10, hata habari kuhusu Mengi ni marufuku kuonyeshwa tangu akina tanil wamiliki kituo hicho...
 
ungejua kama mwandishi wa stori ile ni CUF asilia usingesema hayo..na kama matokeo yalikuwa ya kweli basi Rais asingekuwa huyu wa sasa.
 
ungejua kama mwandishi wa stori ile ni CUF asilia usingesema hayo..na kama matokeo yalikuwa ya kweli basi Rais asingekuwa huyu wa sasa.
Tangu mwaka 1995 matokeo ya uchaguzi wa URAIS Zanzibar hayajawahi kuwa ya kweli. Tusiipotoshe mada hii. Zipo mada nyingi zilizolizungumzia suala hili. Mzee Mengi anaoneshwa sana C10 hasa kwenye shughuli za CTI, wagonjwa mioyo kwenda India,.....ambako anashirikiana na wahindi wengi tu wakiwemo hao wa C10.
 
si magazeti ya kampuni zake tu yanayokosa nafasi katika channel 10, hata habari kuhusu Mengi ni marufuku kuonyeshwa tangu akina tanil wamiliki kituo hicho...

Sakina Dotoo alisema, Waziri wa habri akanukuu
"wamiliki wa vyombo vya habari ndio kikwazo cha uhuru wa vyombo vya habari"

Awe MENGI, RA whatever wote WACHAFUZI wa uhuru wa vyombo vya habari.
 
Huyu mshikaji Tumaini ana matatizo gani? Kwa nini usikae kimya kama huna jibu? Tafadhali jiheshimu na heshimu wana JF na omba radhi.Mmiliki ni Rostam na inasemekana alinunua vyombo vya habari baada ya saga la richmond ili kutumia vyombo hivyo kujisafisha yeye na Lowasa.

Mimi nilikuwa banned kwa muda hapa JF kwa kile kilichoitwa lugha isiyofaa kwa mmoja wa members, naye si mwingine bali TUMAIN. Nilikerwa na posts zake za ajabu ajabu. Sasa sirudii tena naogopa kuwa banned tena. Ila nimefurahi na wenzangu pia mmeona dosari kwa mtu huyu
 
Katika taarifa za habari ambazo nikizikosa huwa nasikitika ni za C10. Vipindi vyao vya mahojiano ni vizuri mno, wamiliki hawajinadi sana kwenye channel hii. Mnakumbuka walivyotangaza matokeo ya KWELI ya URAIS wa Zanzibar 1995?

Mwaka 1995 haikuwepo Channel 10. Nadhani unamaananisha DTV. Soma post No 17 ya thread hii, mwana JF kalieleza suala hili vizuri.
 
Back
Top Bottom