bendaki
JF-Expert Member
- Feb 5, 2013
- 952
- 346
Wanaume wawili walikuwa jirani na mahasimu sana. Kila jioni mmoja wao alipokuwa akipita pale nyumbani kwa mwenzie husema kwa sauti kuwa alimwona mke wa huyo jirani yake akiwa na wanaume wengine guest wakifanya ufuska.
Alirudia maneno hayo mara kadhaa huku yakimfikia huyo jirani hasimu yake. Siku moja huyo jirani yake alihamaki na kumfukuza yule mke wake.
Mara tu huyo mama alipofukuzwa huyu jirani aliyekuwa akimzungumzia ufuska wake aliona ndio muda wa kumtafuta na kumchumbia maana huyu mama alikuwa mama mrembo sana katika huo mtaa wao.
Alipomtaka kumuoa yule mama kwa alivyokuwa amefukuzwa na mume wake wa awali alimkubalia huyu jirani yao sawia. Sasa kati ya wanaume hawa wawili mahasimu lofa ni yupi.
Lofa ni yule bwana aliyekuwa mume wake wa kwanza au lofa ni huyu mume wa pili aliyewahi kumkandia lakini alipofukuzwa yeye akamuoa?