Uchaguzi 2020 Nani mwenye uwezo wa kuishtaki Tume ya uchaguzi kwa kutumia sheria ya takwimu endapo itabainika Imetangaza matokeo yasiyo sahihi

Mung Chris

JF-Expert Member
Sep 12, 2017
3,367
3,778
Haijawahi tokea, kwanini walio gombea ubunge au udiwani wakibaini msimamizi wa tume au tume ya uchaguzi imetangaza matokeo tofauti na waliyopewa kwenye chumba cha kuhesabia kura wasiwashtaki hawa wahusika kwa kutumia sheria ya takwimu badala ya kwenda kupinga uchaguzi mahakamani? na isitumike sheria ya uchaguzi. kipi rahisi.
 
Mkuu utapata taabu sana ni kwamba majukumu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi yameainishwa katika Ibara ya 74 (6) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ambayo ni Kusimamia na Kuratibu Uandikishaji wa Wapiga Kura katika Uchaguzi wa Rais na Wabunge katika Jamhuri ya Muungano;Kusimamia na kuratibu uendeshaji wa Uchaguzi wa Rais na Wabunge; Kuchunguza mipaka na kuigawa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya Uchaguzi wa Wabunge; Kusimamia na kuratibu uandikishaji wa Wapiga Kura na uendeshaji wa Uchaguzi wa Madiwani; na

Kutekeleza majukumu mengine yoyote kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge.

Majukumu mengine ya Tume kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa ni pamoja na yaliyotajwa katika kifungu cha 4C cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, na Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, ambayo ni:- Kutoa Elimu ya Mpiga Kura kwa nchi nzima, kuratibu na kusimamia watu wanaotoa Elimu hiyo; na Kuteua na kuwatangaza Wabunge na Madiwani Wanawake wa Viti Maalum.

Sasa endapo mgombea anaona hajatendewa haki katika uchaguzi na iwapo ana ushahidi wa kutosha anaruhusiwa kwenda Mahakamani kupeleka madai yake kwa msingi wa sheria hizo hapo juu nilizozitaja! Hapo hakuna mazingaombwe hapo kinachoangaliwa ni sheria za uchaguzi kama zimekiukwa na si vinginevyo nje ya hapo ni sawa na kukimbiza upepo!
 
Uwezo huo haupo,hii tume kwanza ipo taifani tu kwenye ngazi zingine za kiutawala haipo,waendesha uchaguzi wa kuanzia ngazi ya ubunge ni wakurugenzi (political appointee wa ruling party)bila ya kuifanyia mabadiliko katiba iliyopo sasa tutasubiri sana,elewa hata kuishitaki serikali hapa kwetu ni ndoto,hiki kivuko kilichozama na kuuwa watanzania wenzetu kwa nchi zinazojielewa serikali iliyopo madarakani ingekuwa na kesi ya kujibu,ila kwa sababu tupo ndani ya shithole country tuendelee kusubiri;President Madiba aliliona hili ndio maana huwezi kusikia jaji anafanya kazi kwenye tume ya uchaguzi ya SA ili kuepusha hii conflict ya maingiliano kati ya JUDICIARY NA NEC.
 
Tume ipo Taifani tu ndio kitu gani? Nani kakudanganya? Nani wameendesha uchaguzi wa Buyungu, Monduli n.k? Acha kupotosha
 
Nzungumzia takwimu ya idadi ya kura pekee zinazo tangazwa endapo ni tofauti simamia hapo je atapeleka karatasi ya takwimu na kufungua mashitaka chini ya sheria ya takwimu? acha habari ya majukumu
 
kama tume y uchaguzi haiwezi kushitakiwa kwa sheria ya takwimu maana yake wana uwezo wa kutangaza matokeo yoyote yale wanayoweza kutangaza
 
Uwezo huo haupo,hii tume kwanza ipo taifani tu kwenye ngazi zingine za kiutawala haipo,waendesha uchaguzi wa kuanzia ngazi ya ubunge ni wakurugenzi (political appointee wa ruling party)bila ya kuifanyia mabadiliko katiba iliyopo sasa tutasubiri sana,elewa hata kuishitaki serikali hapa kwetu ni ndoto,hiki kivuko kilichozama na kuuwa watanzania wenzetu kwa nchi zinazojielewa serikali iliyopo madarakani ingekuwa na kesi ya kujibu,ila kwa sababu tupo ndani ya shithole country tuendelee kusubiri;President Madiba aliliona hili ndio maana huwezi kusikia jaji anafanya kazi kwenye tume ya uchaguzi ya SA ili kuepusha hii conflict ya maingiliano kati ya JUDICIARY NA NEC.
Je kuna taasisi ndani ya serikali ambayo haijui sheria kwa hiyo kwakuwa ni taasisi ya wateule wa rais ndio maana haiwezi kushtakiwa inapo fanya kosa na haiwezi kutii sheria zilizo ainishwa, nafikiri hujasema kitu hapo unaiona tu kama taasisi lakini hujui kama taasisi zipo kwa mujibu wa sheria na wote wana viapo kutii sheria, kanuni na kuilinda katiba ya nchi.
 
Nzungumzia takwimu ya idadi ya kura pekee zinazo tangazwa endapo ni tofauti simamia hapo je atapeleka karatasi ya takwimu na kufungua mashitaka chini ya sheria ya takwimu? acha habari ya majukumu

huwezi kufungua mashitaka yanayohusu uchaguzi chini ya sheria za takwimu kwa sababu kama tatizo ni matokeo ya uchaguzi yanatofautiana utafungua mashitaka ya uchaguzi.

kinachofanyika wakati wa kutangaza matokeo ni kwamba kura zikishahesabiwa na kujumlishwa hujazwa kwenye fomu ya matokeo ambayo kila wakala wa chama au mgombea anapewa nakala yake na ikitokea nakala hazifanani (ya msimamizi inaonesha chama a kimeshinda lakini ya wakala inaonesha chama b kimeshinda) hiyo ni kesi ya uchaguzi unafungua kupinga matokeo na sheria za uchaguzi ndizo zinazotumika.

kuna makosa ya kiuchaguzi mashitaka yake yanaendeshwa kwa kutumia sheria za uchaguzi lakini ukimchoma mtu kisu kwenye kituo cha kupigia kura utashitakiwa kwa mujibu wa sheria za kipolisi na wala hakuna sheria ya uchaguzi inayozungumzia kosa hilo.
 
Nzungumzia takwimu ya idadi ya kura pekee zinazo tangazwa endapo ni tofauti simamia hapo je atapeleka karatasi ya takwimu na kufungua mashitaka chini ya sheria ya takwimu? acha habari ya majukumu

Mkuu kwenye Uchaguzi hakuna karatasi ya takwimu nenda kawaulize hata hao wagombea wako, kilichopo ni Fomu za Matokeo kama ifuatavyo.

1. Fomu na 21A ambayo ni ya Matokeo ya Uchaguzi wa Rais katika kituo cha Kupigia Kura na hii iko chini ya Kanuni ya 60(1) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Bunge za 2015.
2. Fomu na 21B ambayo ni ya matokeo ya Kura za Ubunge katika Kituo cha kupigia Kura
3. Pia Fomu na 21C kwa ajili ya Matokeo ya Kura za Diwani katika kituo.

Fomu zote hizi zipo kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi, Narudia tena Fomu hizi zote zipo kwa mujibu wa Sheria.
Na zinasimamiwa na Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura ya 343 na Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292 na SIO Sheria ya Takwimu kama unafikiri sheria ya takwimu ndiyo inasimamia Uchaguzi imekula kwako na ukibisha zaidi nenda Mahakamani ukafanye uhakiki.
 
kama tume y uchaguzi haiwezi kushitakiwa kwa sheria ya takwimu maana yake wana uwezo wa kutangaza matokeo yoyote yale wanayoweza kutangaza

Matokeo yoyote ndio yapi? Kwenye uchaguzi hakuna matokeo yoyote kuna Matokeo ya Uchaguzi. Kwa Tanzania mgombea anatangazwa kuwa mshindi kwa kupata Kura nyingi halali kuliko wagombea wengine na hii ndiyo demokrasia.
 
Haijawahi tokea, kwanini walio gombea ubunge au udiwani wakibaini msimamizi wa tume au tume ya uchaguzi imetangaza matokeo tofauti na waliyopewa kwenye chumba cha kuhesabia kura wasiwashtaki hawa wahusika kwa kutumia sheria ya takwimu badala ya kwenda kupinga uchaguzi mahakamani? na isitumike sheria ya uchaguzi. kipi rahisi.

Kwani wewe unaona kipi rahisi?
 
Back
Top Bottom