Nani mwenye makosa, CHADEMA au serikali? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nani mwenye makosa, CHADEMA au serikali?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kisendi, Nov 9, 2011.

 1. K

  Kisendi JF-Expert Member

  #1
  Nov 9, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 700
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Tutafakari kwa kina, nani alaumiwe katika suala zima la vita kati ya chadema na ccm huko arusha. Binafsi napenda tupate mtaalamu wa sheria humu atupe ufafanuzi bila hiana na asiwe kwenye magamba. Siku lema ameenda mahakamani alienda kwa mguu kutoka ofisi za cdm arusha, kesi ikaarishwa maana lema alikuja na group la watu wengi waliomfuata kama wapenzi wa cdm, wakati anarudi kutoka mahakamani watu wengi walimfuata kwa kuwa alikuwa anatembea kwa mguu kama kawaida yake. Alifika sehemu akuwaasa waananchi kuwa watawanyike maana kesi imearishwa mpaka tar nyingine. Lakini wananchi walitaka aseme zaidi, polisi walifika na kuwakamata lema na baadhi ya wafuasi. Je hilo ni kosa kisheria au hii ikoje, swali kwenda na watu mahakamani ni kosa au sio kosa. Mwisho kabisa dr slaa na wenzake kulikuwa na umhm wa kukesha pale maana waliambiwa mwisho saa 12 jioni.

  Binafsi inabidi pia tujaribu kupunguza mvutano ili angalau wana arusha tupate maendeleo, lini lema na wenzake watapanga mikakati ya 2015 kuchukua nchi, kuleta mabadiliko katika majimbo waliyochukua 2010.

  Nawakilisha
   
 2. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #2
  Nov 9, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,570
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  Nimekusaidia editing sina hakika kama uko sawa

  ila kama uko sawa, swali lako zuri mno japo hutapata jibu kwenye sayari ya Tanzania ya chadema
   
 3. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #3
  Nov 9, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  hapa hutapata jibu sahihi wapo watakajibu kichadema na wengine kiCCM. hapa JF hakuna professional kila mtu anavutia kwake
   
 4. J

  J.K.Rayhope JF-Expert Member

  #4
  Nov 9, 2011
  Joined: Oct 26, 2011
  Messages: 316
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu,jibu lipo wazi.Wala sioni mwenye akili kati ya wote hao.Aliyepewa madaraka,atuongoze nae anaongozwa ktk kufanya vurugu.
   
 5. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #5
  Nov 9, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  nenda kwenye ofisi za wanasheria wenye rekodi nzuri ya kutoa majibu bila kuvutwa na hisia. Wanasheria wa hapa Jf ni wanasiasa tunawaita siasheria
   
 6. s

  seniorita JF-Expert Member

  #6
  Nov 9, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 674
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  relative question....
   
 7. Joel

  Joel JF-Expert Member

  #7
  Nov 9, 2011
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 908
  Likes Received: 259
  Trophy Points: 80
  unaposema hivyo unamaanisha nini wewe?Proffessional wa nini katika kujibu swali kama hilo?
   
 8. E

  EMMANUEL NSAMBI JF-Expert Member

  #8
  Nov 9, 2011
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 402
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Labda tungepata ufafanuzi wa maana halisi ya neno maandamano.Nijuavyo mimi maandamano ni matembezi ya kundi
  la watu wenye lengo la ama kupinga au kuunga mkono jambo fulani.Lakini kwa hawa waliotokea mahakamani wakisindikiza
  mbunge wao lnanipa ugumu kidogo.Hivi watu wanapotoka kuzika makaburini,huwa wanaomba kibali cha polisi?
  Mbunge anapotaka kuongea na wananchi wake kuhusu kuchangia maendeleo ya jimbo lake lazima kibali?
  Nakumbuka wakati fulani Tembo walivamia mashamba ya watu kule rombo na Mramba akiwa mbunge aliandamana na
  wananchi wake tena usiku,mbona sikuona akikamatwa?
   
 9. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #9
  Nov 9, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Wote wanamakosa! cdm wamepotosha fikra ya lema na serikali wamekurupuka na mibavu yao ya kidikteta.
   
 10. Lenana

  Lenana JF-Expert Member

  #10
  Nov 9, 2011
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 422
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  fikra ya lema ni ipi!!!???
   
 11. Mundali

  Mundali JF-Expert Member

  #11
  Nov 9, 2011
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 749
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Majibu ni mepesi sana, sisi waafrika tunaamini katika kukandamizwa, tunaishi kinyonge na kuamini sisi ni wanyonge tusio na haki zozote. Ndio maana watawala wetu wanaamini hivyo na kutufanya hivyo. Suala la Lema ni moja tu kati ya milioni kadhaa ya uonevu wa dhati kabisa tunaofanyiwa na watawala na tunakaa kimya. Mfano, huu msemo wa "kuingia bure kutoka na hela" umetokana na utamaduni uliohalalishwa na Jeshi la polisi pindi wanapokamata watuhumiwa. Pia ni kitu cha kawaida sana kusikia askari akimtishia raia kumweka ndani bila kujali ni kwa kosa gani. Ni wangapi waliobambikwa kesi za ujambazi, wakati ni raia wema kabisa? Wengine kuuawa na polisi kwa visingizio kama hivyo. Rejea kesi ya Zombe na wenzake. Je, ni mara ngapi watawala wameua ama kupiga watu kwa makusudi, kisha waathirika kuonekana ndio wakosaji, mfano kesi ya marehemu Ditopile. Kwa sababu tunaishi kwa mazoea na kuonewa ndio majaliwa yetu, sishangai watu kuanza kuhoji suala la Lema kwa mtazamo wa kinyonge na kitumwa zaidi kuliko kwa fikra za binadamu aliye huru.
  Dhana nzima ya ndugu Lema (Mb) kukataa dhamana sio kwamba anajitafutia umaarufu kama baadhi ya wanasiasa wanavyodai, bali ni kupinga ukandamizaji wa watawala kupitia vyombo walivyojiundia. Hii haina tofauti na utawala wa kidikteta wa Nduli Iddi Amini.
  Tofauti ni kwamba Amin alitoa amri moja kwa moja za kukamatwa na kuuawa wapinzani wake.
  Tulipofikia hatuko huru kama tunavyojidanganya. Mbunge wa CCM, mwana mtandao anatuhumiwa kuandaa mauaji hakamatwi mpaka kibali kitoke ofisi ya bunge, wa CDM anarudi kwa miguu toka mahakamani kusikiliza kesi inayomhusu, anakamatwa ati katembea bila kibali.
  Hii maana yake ni kwamba, Mh. Lema haruhusiwi kushiriki misa yoyote, misiba, kuangalia michezo, itafika wakati hata bungeni hataruhusiwa kuongozana na wabunge wengine. Sababu kote huko kuna mikusanyiko ya watu, na mkitoka ni lazima mtaandamana kwa umbali fulani.
  Kuhusu, suala la Slaa na wafuasi wao hapo ni kielelezo tosha cha polisi wafanyao kazi kwa hulka pasi kutumia busara. Mkutano ni mahali ambapo watu wanajadili hoja, na kunakuwa na msemaji na wasikilizaji. Mkusanyiko ni mahali ambapo watu wamekusanyika kwa sababu fulani. Je, walimkuta Dr. Slaa anahutubia ama amekaa katika mkusanyiko wa maombolezo? Hivi ni lazima ulale kwenye nyumba? Mbona wamasai wanalala porini hawakamatwi? Hivi kwenye misiba kuna vibali vya kulala matanga?
  Ni hayo tu, wapendwa wa nchi ya vibali.
   
 12. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #12
  Nov 9, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Chadema wapo sahihi
   
 13. FREDRICK KIMARO

  FREDRICK KIMARO Member

  #13
  Nov 9, 2011
  Joined: Aug 15, 2011
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kuna siku haya yatafika mwisho
   
 14. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #14
  Nov 9, 2011
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Fafanua zaidi, kumbe ni vita dhidi ya CDM na CCM? Ina maana watumishi wote wa vyombo vya umma kama polisi na jeshi ni CCM? Kama suala ndo hivyo - basi mambo si shwa kote kote.
   
 15. Gwalihenzi

  Gwalihenzi JF-Expert Member

  #15
  Nov 9, 2011
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 5,117
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  we hayawani, unawezaje ku-edit post ya mtu bila idhini yake? Mbona unafanya ubabe usio na maana hapa?
   
 16. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #16
  Nov 9, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Hayo unayoyasema ndugu yangu uliyashuhudia kwa macho yako au umesoma tu kwenye magazeti yetu ambayo yako tayari kuona nchi inatumbukia katika hatari kwa sababu tu yamenunuliwa au kwa chuki binafsi dhidi ya baadhi ya watu. Nadhani ifike wakati jamani tutambue kuwa Jeshi letu Polisi lipo kisheria na hayo linaloyatekeleza arusha ni mujibu ya sheria na taratibu za nchi. kUHUSU dokta SLAA na wenzake, mimi nadhani wananchi sasa tumeshafanywa mazezeta na wanasiasa. SLAA na wenzake wanawakusanya watoto, vijana na wazee kulala huko wakati wao wakiwa na SILAHA za moto na mbaya kabisa wanakimbia na kuwaacha. hii siyo sahihi kabisa. Mimi nilitegemea kabisa wawe na ujasiri wa kukabiliana na POLISI kwa vile tayari walikuwa na SILAHA. Ndiyio maana siku zote naamini kuwa huwa wanataka kuwafurahisha watu tena ili wapate umaarufu tu. KITENDO HIKI CHA KUTOROKA NA KUJIFICHA kwa viongozi hawa ni uthibitisho kwamba wanatambua kuwa wanavunja sheria tena kwa makusudi.
   
 17. doctorz

  doctorz JF-Expert Member

  #17
  Nov 9, 2011
  Joined: Aug 10, 2010
  Messages: 907
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  The most important human endeavor is the striving for morality in our actions. Our inner balance and even our very existence depend on it. Only morality in our actions can give beauty and dignity to life.

  Serkali iwa achie wananchi kuandamana. Jeshi la Polisi wasiwe watabiri wa ktoa hoja hati wanasitisha maandamano hata kama ni ya amani. Mara nyingi imetokea kuwa waanzilishi wa fujo ni polisi pale wanapo chukuwa uamuzi wa kupiga wananchi bila ya hatia. Sio kila mtanzania ni mpenda fujo. Lakini kila polisi hii leo ni hakimu wa kuamuwa kuwa kila mkusanyiko wa watu ni wa fujo. Hii inawatibua wananci na wanajihisi kuonelewa na chombo ambacho wanakitegeme kiwalinde.
   
 18. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #18
  Nov 9, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,570
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  sikuwezi nasikia umeanza kutukana wakati unatoka tu kwenye ile njia kuu, ebu sema kisa cha kuniita hayawani ni nini? utakufa kwa presha

  ukiendelea kutukana nakupiga ban la milele, usifikiri JF ya watu fulani hii

  kama hauamini ebu tukana tena uone, nitabadili jina lako na tarehe ya kujiunga JF sasa hivi!! oh oooh!
   
 19. Gwalihenzi

  Gwalihenzi JF-Expert Member

  #19
  Nov 9, 2011
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 5,117
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Acha vitisho wewe, jibu hoja, mandate ya ku-edit post ya mtu mwingine umepata wapi?Death is reality hence am not afraid of it, swine.
   
 20. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #20
  Nov 9, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,570
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  nimeisha kupiga ban sichezi na watoto kama ww
   
Loading...