Nani mwanzilishi wa shule za kata?

Nani mwanzilishi wa shule za kata?

UGORO87

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2014
Posts
824
Reaction score
383
Wakuu, nataka nilete hii mada mbele yenu kati ya Edward Lowassa na Dr. Slaa kuhusu shule za kata.

Dr Slaa alianzisha Sekondari za kata kabla ya mwaka 2000, wakati Lowassa anatangaza sekondari za kata zijengwe nchi nzma tayari Dr Slaa jimboni kwake kila kata iwe na a-level na sekondari kila kijiji na dispensari kila kijiji.

Dr Slaa ameacha hizo program tayari kwa asilimia 90. Lowassa yeye alihamasisha nchi nzima kama Waziri Mkuu.

Nawapongeza wote kwa nafasi zao wamecheza na wameweza.
 
si mjinga EL au ni nani wa kuanzisha shule bila walimu mjinga zaidi ya huyu jamaaa
 
Waandishi wa habari wanaowaambia Watanzania kwamba shule za kata alianzisha Lowassa. Huo ni uwongo ambao unapaswa kulaaniwa na watu wanaosimamia ukweli katika maisha . Shule za kata zimeanza wakati wa utawala wa rais Mkapa miaka ya 2002.

Mpango huo wa MMEM na MMES ulioasisiwa na rais mkapa na kusimamiwa na waziri mkuu Sumaye na waziri wa elimu wa wakati huo bila shaka atakuwa Mungai kama sikosei ndio waliosimamia utakelezaji wa mipango ya MMEM na MMES .

Tukumbuke mipango hiyo ilianza na crush program iliyolenga kuongeza idadi ya walimu nchini ikazoa wanafunzi waliomaliza kidato cha nne na kuwapeleka vyuoni kwa mwaka mmoja na wale wa sekondari wapo waliopata mafunzo ya miezi mitatu ili kuziba pengo la walimu.

Lowasa anaingia madarakani tayari shule za kata zilishaanza kujengwa . Lazima tukubaliane Lowasa kaingia madarakani novemba 30, 2005 na kuondoka madarakani kama waziri mkuu february 7 , 2008. Kwa maana hiyo yeye Lowasa kaweza kusimamia bajeti mbili tu katika utawala wake,bajeti ya julai 2006- juni 2007 na bajeti ya Julai 2007 hadi Juni 2008.

Sasa kwa bajeti hizo mbili tu unaweza kujenga shule za kata nchi nzima. Huo ni uwongo wa dhahiri. tena bajeti yenyewe ya 2007-2008 hakuimalizia kutokana na kuondoka miezi minne kabla ya muda wa bajeti mpya.

Waandishi wa habari msimpe mtu sifa zisizo zake. Shule za kata alizikuta zilizoanzishwa na Sumaye na kuziacha zikaendelezwa kujengwa na waziri mkuu wa sasa Pinda. Tena Pinda ndiyo aliyofanya kazi kubwa ya kuhakikisha anaongeza idadi ya walimu nchini kwa kupango mipango mbalimbali kama vile kuajiri walimu wengi wa sekondari na kupeleka vyuoni walimu wengi wa sayansi, kuimarisha mafunzo na semina shirikishi kwa walimu.

Leo hii walimu nchi nzima wapo UDOM Dodoma wakipata semina. Sumaye alikazia kujenga madarasa na nyumba za walimu, Lowassa akaendeleza tu jitihada alizozianzisha Sumaye kwa miaka miwili na yeye akakazia kujenga nyumba za walimu na si madarasa kwani miaka ya 2006 ilipigwa marafuku kwa madiwani kwamba shule za sekondari zilizojengwa zinatosha kwa kazi aliyoifanya ni kuboresha madarasa na kujenga nyumba za walimu na kuongeza madawati .

Sifa anazopewa Lowassa kana kwamba yeye ndiye aliyeanzisha huo mpango na wengine waliomtangulia na kumpokea majukumu ya uwaziri mkuu hawajafanya kitu. Tunawakatisha tamaa viongozi wetu. Leo hii kila shule ina maabara waziri mkuu atakaye kuja atakuwa na kazi ya kupeleka vifaa tu hii haina maana kwamba sasa tumbeze aliyefanya kazi ya kuzijenga maabara hizo.

Kila mtu apewe sifa zake stahiki na si kumpa mtu sifa kwa sababu ya njaa yako inayokusumbua.
 
Mwandosya nae kasema yeye ndo muasisi wa shule za kata.
 
Jambo usilolifahamu ni vema ukakaa kimya au hata ukauliza. Ni mwendawazimu anayeweza kubisha ukweli kuwa si Lowassa aliyesimamia ujenzi wa hizi shule. Mwaka 2006,, kama utakumbuka kuna wanafunzi walianza kujiunga shule MWEZI March baada ya kutoa agizo kwa wakurugenzi kuhakikisha wanakamilisha shule hizo ikiwa ni pamoja na kuchangisha wazazi wa kila kata na c bajeti kubwa ilipelekwa huko nna serikali.

Baada ya hapo ilianza operesheni ya walimu waliokuwa wanaitwa vodafasta, nakumbuka Julai 2006 tulikutana pale kigurunyembe morogoro watahiniwa kama 20,000 kwa mchujo ili kutafuta nafasi hizo za ualimu.

Japo wazo lilianza kipindi cha Mkapa lakini full and speed implementation ilifanyika miaka yake hiyo miwili na c kwa bajeti zaidi kama unavyotaka wenzio waamini. Baba yako akianzisha Plan asipoifanyia kazi wewe mtoto ukaimplement huwezin kusema baba ndo kaimplement.

Mfano ukimsikiliza Mohamed Dewji leo hii anadai mtaji alipewa na baba yake lakini alienda mbali zaidi na kuidealize kazi za baba yake zilizokuwa za kununua na kuuza bidhaa hadi yeye kuamua kutengeneza bidhaa za viwandani na kulima mashamba. leo hii hata baba yake hatambuliki kabisa Africa nzima inamjua Mo basi. So kuweni na fikra pevu kabla ya kubishana na kuandika vitu msivyo na uhakika navyo.
 
ligera
Watakuja kukuthibitishia tu kuwa wao ndio walioasisi mkakati hyo
Uzuri wenyewe wana data
Kimewauma mpaka mnakata mawasiliano kabisa?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Ligera,
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Wazo la kila kata kuwa na shule ya sekondari lilitolewa na Lowassa.

Mwaka 2006 mwanzoni, Lowassa alitoa directives mbili muhimu kuhusu elimu ya shule za sekondari.

1. Kila kata lazima iwe na shule ya sekondari
2. Minimum asilimia 75 ya wanafunzi waliofaulu mitihani kuingia sekondari wawe wamejiunga na sekondari kufikia tarehe 01/04/2006.

Kabla ya hapo hizo shule zilikuwa haziitwi shule za kata. Ni kweli shule ziliongezeka kipindi cha Mkapa lakini bado zilikuwa chache sana. Kuingia kwa Lowassa ndio kuliziongeza hizo shule kwa idadi kubwa sana. Baada ya hapo shule zote zilizojengwa kabla pamoja na hizi mpya za Lowassa ndio zikaitwa shule za kata.

Unaweza kusoma hii paper ya Hakielimu ili kukusaidia.
http://internationalbudget.org/wp-content/uploads/HakiElimu-Case-Study.pdf

In terms of recent trends in policy implementation, PEDP and SEDP have dramatically expanded access to primary and secondary education. At primary level, the Gross Enrollment Rate increased from 78 percent to 112 percent between 2000 and 2006.31 Actual enrollment grew by over 60 percent, up from 4.4 million in 2000 to well over 7 million in 2006.32 Expansions in access to secondary education have been even more dramatic.

For example, 401,011 students were enrolled in the first year of secondary school in 2007, up from 148,412 just two years earlier. These numbers far exceeded SEDP projections and likely resulted from the impact of two related directives issued by former Prime Minister Edward Lowassa, namely to build a secondary school in each ward and to enroll 75 percent of those who pass the primary education examinations.
 
kwani mbona JK anabebeshwa sifa zote za ujenzi wa lami wakt mpango ulianza mwaka 2002 na mkapa baada ya kupokea mawazo toka world bank na kuanzisha ROAD FUND????
 
Hata hilo la walimu, ni kipindi hicho hicho cha mwaka 2006.

Soma zaidi hapa chini.

The Tanzanian government's initial response to the teacher shortage was largely in keeping with the politicized nature of the policy process. In 2006 it reduced normal teaching diploma training from a two-year taught course to a one-year taught course and one year's teaching experience.

Furthermore, in an attempt to fill acute gaps even more quickly, the government instituted a "crash program" nicknamed VodaFasta (a reference to a rapid electronic airtime distribution and recharge service promoted by one of Tanzania's major mobile phone companies) through which high school leavers were "trained" in as few as three months before being dispatched to schools.35 Around the same time came a directive from former Prime Minister Lowassa to build secondary school in every ward.

While intended to address what was indeed a pressing need given large numbers of children now leaving primary school, Lowassa's action did not reflect policy. It was seen as a "blatant political decision" - described by a former ministry official as "ignoring policy, [because] that's politics."36, 37 Since that decision was taken, Tanzania has seen its secondary education sector expand faster than any other country in the world. However, the newly established "ward schools" typically exhibit much worse conditions in terms of staffing and teachers' qualifications.3
 
ligera Mtanzania

Mi nakubali kuwa unasema lile unalofahamu na kwa uwezo wako wa ufahamu. Kumbuka na nataka kukufahamisha kuwa shule za secondary ni mpango wa TASAF 2 mpango ulio kuwa adopted Malawi (MASAF 2) na Mkapa mh. Alienda mwenyewe na timu yake kupata darasa.

Kwa hiyo, Fanya intergration ya data Kabla kuruka hewani vinginevyo utashushia hadhi na heshima yako mkuu
 
Last edited by a moderator:
Ni mwendelezo wa kukumbatia ile dhana ya QUANTITY kuliko QUALITY. Shule zimejengwa nyingi hapa nchini hiyo ni kweli,swali linakuja,je hizo shule za kata zinatoa asilimia ngapi ya wanafunzi wanaofaulu nchini?Shule zimejengwa hazina laboratories wala libraries kwaajili ya wanafunzi Kujivunia,isitoshe walimu waliopo nao hawafundishi vizuri.

Tatizo la walimu kufundisha chini ya viwango linaweza kuchangiwa na aidha malipo duni,mitaala mibovu/vitabu vilivyo chini ya viwango na walimu wenyewe kutokuwa na sifa stahiki za kufundisha.Jiulize,huyo Lowassa aliwahi kuzungumzia changamoto hizi na nini ilikuwa msimamo wake katika kumaliza hizi changamoto?
 
NATTA WITO

Msimamizi hawezi akawa bora kumshinda muasisi, msimamizi anachokifanya ni kusimamia kwa kufuata maelekezo yaliyoachwa na mwazilishi.

Kosa linalofanywa ni kusema kuwa Lowassa ndiye aliyeleta secondary za kata wakati aliyeleta secondary za kata ni Mkapa.

Anaetakiwa kusifiwa kwa kuleta secondary za kata ni Mkapa na Lowassa ana takiwa asifiwe kwa kusimamia vizuri kile kilichoanzishwa na kuachwa na watangulizi wake.
 
Last edited by a moderator:
Hata kama wanaendekeza njaa na wameamua kujitoa ufahamu kwa kuto kuyaona matendo mabaya yaliyofanywa na Lowassa wanatakiwa wafanye kazi kwa kufuata maadili ya kazi yao,wawaeleze ukweli wananchi kuwa Lowassa ndiye muasisi wa ufisadi.

Ili watanzania wajue mtu anae kwenda kuwaomba kura ni mtu wa aina gani,na kama wanakwenda kumchagua wajue kuwa wanakwenda kumchagua mtu wa aina gani,ili baadae wasije wakajuta kuwa tulidanganywa ndio maana tukamchagua,vinginevyo tusingemchagua.
 
Mkuu Kalambo one,
Suala la kuongeza uwingi wa shule lilikuwepo wakati wa Mkapa.

Lakini aliyeamua kila kata ijenge shule ya sekondari ni Lowassa. Kutokana na agizo hilo la Lowassa ndio maana hata sasa zinaitwa sekondariza kata.

Soma hapo juu kwamba uamuzi wa Lowassa ulikuwa wa kisiasa. Kabla ya hapo hakukuwa na policy ya namna hiyo. Hata ilani ya uchaguzi ya ccm haikusema hivyi.

Hili la shuleza kata ni sawa tu na ujenzi wa UDOM. Yalikuwa maamuzi ya kisiasa.

Mnigeria mi nakubali kuwa unasema lile unalofahamu na kwa uwezo wako wa ufahamu.
Kumbuka na nataka kukufahamisha kuwa shule za secondary ni mpango wa TASAF 2 mpango ulio kuwa adopted Malawi (MASAF 2) na Mkapa mh. Alienda mwenyewe na timu yake kupata darsa.
Kwahiyo Fanya intergration ya data Kabla huruka hewani vinginevyo utashushia hadhi na heshima yako mkuu
 
Back
Top Bottom