1. Dunia hii inamilikiwa na yule aliyeiumba kulingana na imani yako.
2. Kuhusu kugawa dunia, hii ilikuwa ni kazi ya Watawala waliokuwepo enzi hizo ili waweze kutawala kwa urahisi bila kuingiliana na kusababisha vita; rejea falsafa ya "Gawa Utawale" au kwa lugha ya Kiingereza "Divide and Rule" Rejea kilichofanyaka katika mkutano wa Berlin mwaka 1884 na matokeo yake
3. Kabla ya Tanganyika, eneo hili lilikuwa German Osta Afrika ikiwa na rasilimali nyingi, misitu, wanyamapori ila watu walikuwa wachache sana ambao waliishi kwa misingi ya kikabila na walikuwa tayari kupinga uvamizi kutoka mataifa mengine rejea Mkwawa, Kimweri, Mirambo, Mangi Sina na wengine wengi
4. Binadamu hajawahi kuwa nyani, binadamu ni binadamu na nyani ni nyani. Kinachotokea ni mabadilko (evolution) yanayosababishwa na harakati za binadamu katika kupambana na mazingira yake. Mabadliko haya yanatokea katika mwonekano wake na uwezo wa kufikiri na kutenda; na bado yanaendelea (angalia mwonekano wa watoto wanaozaliwa sasa hivi au linganisha picha za miaka hata ya 60 na za watu wa miaka hii). Binadamu wa zamani walikuwa na miili mikubwa kwa sababu ya aina ya kazi walizofanya, kwa sasa milili ni midogo lakini akili nyingi. Katika Tanzania, tafiti zinaonyesha kuwa binadamu walikuwepo tangu miaka milioni 3.6 iliyopita, ushahidi huo unapatikana katika Bonde la Olduvai kule Ngorongoroa ambako mnmo mwaka 1959 kuligunduliwa fuvu la binadamu aliyetwa Zinjanthropus boisei. Kabla ya ugunduzi wa moto, binadamu waliishi porini kama wanyama wakila matunda, mayai ya ndege, mizizi na nyama mbichi; wakinyweshewa na mvua na kupigwa na baridi kwa maana hiyo hata miili yao ilikuwa na manyoya kwa ajili ya kuukinga mwili na baridi. Baada ya ugunduzi wa moto, binadamu walianza kuishi pamoja kwenye mapango (mwanzo wa vijiji?) na kutokana na kuota moto, manyoya yalianza kupungua miilini mwao. Aidha, walianza kutumia moto kuchoma chakula chao. Kwa hiyo jinsi ambavyo binadamu amekuwa akijitahidi kupambana na kuboresha maisha yake amekuwa akibadilika na kuwa na sura kama hiyo yako. Ila kama ungezwaliwa miaka milini 3.6 iliyopita, hakika ungekuwa na sura mbaya ukilinganishwa na binadamu wa sasa.
Angalia aina hii ya maisha: Kuishi porini na kula chakula kibichi - kutumia zana za mawe - ugunduzi wa mto - kuishi katika mapango na kuota moto - ugunduzi wa zana za chuma - kuishi kwenye nyumba za nyasi - kuishi kwenye - nyumba za bati/ghorofa - matumizi ya teknlojia kukabili maisha; badala ya kutembea mwendo mrefu binadamua anatumia magari, ndege, simu na vingine vingi ambavyo vimefanya dunia kuwa kijiji. SASA FIKIRIA MARA MBILI KABLA HUJAANZA KUKUFURU KUWA BINADAMU ALIKUWA NYANI, HEBU JIULIZE NI KWA NINI NYANI WA SASA HAWABADILIKI KUWA BINADAMU.