Nani Mkweli Juu ya Mauaji ya Polisi Ngara?

Nani Mkweli Juu ya Mauaji ya Polisi Ngara?

kibogo

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2012
Posts
9,739
Reaction score
4,745
Tamko la kamanda wa Polisi

“Askari hawa walikuwa katika doria ya kawaida, walimkamata mwenye bodaboda na alikuwa anagoma kutii amri na wakati wanabishana alitoa kisu ndipo askari huyo akampiga risasi,” alisema kamanda huyo.

Hata hivyo, alisema kituo hakikuteketea chote, na kwamba hata nyaraka zilizoungua ni chache.

Tamko la Mashuhuda Wananchi

Awali, ilielezwa na mashuhuda kuwa, chanzo cha mauaji hayo ni kuwa polisi walifika katika Kijiji cha Mugoma kwa lengo la kukagua pikipiki mbovu na zisizokuwa na usajili na walifika katika gereji moja na kukuta mmiliki wa gereji hiyo akitengeneza pikipiki, kumtaka aipeleke kituoni kwa maelezo kuwa ilikuwa mbovu.

Baada ya hapo, fundi aligoma kutekeleza agizo hilo na polisi mmoja alimpiga risasi, kitendo ambacho kiliamsha hasira kwa wananchi waliokuwa jirani na eneo hilo.

Ilielezwa na mashuhuda kuwa baada ya tukio polisi aliyefyatua risasi alikimbilia kujificha katika nyumba iliyopo jirani na gereji hiyo, huku akimuacha mwenzake.

“Wananchi walimvamia yule askari aliyebaki pale gereji na kuanza kumcharanga kwa mapanga na kumpiga mawe hadi akafa,” alisema mmoja wa mashuhuda.

Alifafanua kwamba baada ya kuhakikisha kuwa wamemuua, wananchi hao walikwenda katika nyumba aliyojificha askari aliyekimbia, kutaka kuichoma moto iwapo angegoma kutoka.

“Mmiliki wa nyumba ile baada ya kuona wananchi hao wanataka kuichoma moto nyumba yake alimtaka askari huyo kutoka nje, alipotoka tu wananchi walimvamia na kuanza kumpiga mawe na kumuua,” alisema.

Kituo cha polisi kilichoteketezwa kwa moto, kipo karibu na mpaka wa Tanzania na Burundi.


My Take!
Hivi inapoteza heshima ipi iwapo hawa viongozi wetu wa Polisi watakuwa wakweli? Kauli yake hii inataka kuaminisha umma kwamba huyu raia aliyeuawa alitaka kuwadhuru Polisi ndo wakachukua hatua ya Kumuua

CHANZO GAZETI LA MWANANCHI
 
Serikali hii haiwezi kuwa upande wa Raia. Je gereji hupelekwa kitu kizima au kibovu?
 
Haya ni maigizo mengine........sio mapya, ni copy and paste tu kutoka kaigizo ya zamani.
Hakuna mwenye ruhusa ya kuondoa maisha ya mwingine.
Kila mtu atimize wajibu wake........Eti fundi huyo akatoa kisu....yani fundi amtolee polisi mwenye SMG kisu?
Hizi bange za wapi hizi??
 
Polisi ni waongo, hebu hizo kauli mbili ziweke kwenye mizani utagundua hiyo taarifa ya RPC inapwaya kiasi gani.
 
Mkuu Police ni kiboko kwa kucingizia.. Mie nina mfano hai kabisa.. Walikamatwa jirani zangu wawili ndani kwao katika operation ya kumtafuta mwizi.. Walitonywa kuwa huyo wanaemtafuta analala humo.. Walipoenda hawakumkuta mtu wao wakaamua kuwakamata hao jirani wawili.. Baadae katika kuwapiga na kuwalazimisha kusema wakamvunja mmoja mguu kwenye goti.. Ndugu zake huyo alievunjwa goti wakaja juu.. Kilichotokea ni kupewa keci ya uvunjaji wa kutumia nguvu na kwamba walikamatwa kwenye eneo la tukio la ujambazi..! Huwezi kuamini walikaa ndani miezi sita na keci ikaisha kwa gharama kubwa sana..! Hiyo ilitosha kunipa sababu ya kutowaamini Police maisha yangu yote..

Nikicikia jambazi au majambazi yameuawa katika "majibishano" ya risasi na Police ninacikitika kwa kuwa ninaamini hao waliouawa ciyo majambazi.. Ila wameuawa na majambazi walio na magwanda..
 
Msemaji wa polisi aliambiwa na nani kama wote wameuawa?

Wamezoea kutunga.

Wananch lazima tujilinde sisi na mali zetu na adui yetu wa kwanza ni polisi
 
Hatuwezi kuupata ukweli kama kila mtu atakuja na uchunguzi kama wa kwako:

Polisi maelezo yao mistari miwili na ya wananchi mengi kama ulivyofanya. Unatoa hoja na mwisho una conlude - polisi ni waongo..!

Nadhani tutaupata ukweli pakiwepo na kitu huru cha kuchunguza na kuelezea tukio hili bila ya kuegemea upande wowote.
 
Polisi ni waongo, hebu hizo kauli mbili ziweke kwenye mizani utagundua hiyo taarifa ya RPC inapwaya kiasi gani.

RPC, kasema uongo wa kutunga kichwani mwake! Kwani watu ambao wangemweleza kwamba fundi pikipiki aliwatolea kisu wote wawili wamekufa ina maana Ma- RPC wa tz huwa na uwezo wa kuwasiliana na maasikali wao walioko kuzimu?
 
Nawaunga mkono wananchi kwakweli ningewapa tuzo kwa kuonyesha kuchoshwa na hawa wanaojiita polisi kumbe ni majambazi wauaji wakubwa...Get this lesson from mwangosi..Mia
 
Ni vigumu sana kuupata ukweli kwa kuwa wahusika wakuu wameshatangulia mbele ya haki!!
 
rpc, kasema uongo wa kutunga kichwani mwake! Kwani ambao wangemweleza kwamba fundi pikipiki aliwatolea kisu wote wawili wamekufa ina maana ma- rpc wa tz huwa na uwezo wa kusiliana na maasikali wao walioko kuzimu?
hakuna ubishi askari wameuwawa kinyama na askari wameua raia,cha msingi ni kusubiri tume ije ichunguze na kutoa mapendekezo na maoni kuhusiana na jinsi ya kushughulikia matukio ya aina hiyo yasitokee tena.pia katika matukio ya namna hiyo wapo baadhi ya watu wameona tukio zima na wapo tayari kutoa ushahidi.swala la nani anauwezo wa kuwasiliana na marehemu siyo issue,mbona usia wa marehemu unakubalika akisha kufa kama ushahidi sembuse madai ya mtu kutolewa kisu?.kama tunaweza kukubali usiwa wa marehemu kwanini tusikubali mambo mengine?.kama unaushahidi peleka ktk tume iliyoundwa usaidie,kama huwezi kufikisha ujumbe/ushahidi wako basi ukubaliane na majibu ya tume.
 
Polisi huku ndiko wanakotupeleka.uonevu wao watu wameanza kupambana nao kwa njia ambazo hazifurahishi
 
Hatuwezi kuupata ukweli kama kila mtu atakuja na uchunguzi kama wa kwako: Polisi maelezo yao mistari miwili na ya wananchi mengi kama ulivyofanya. Unatoa hoja na mwisho una conlude - polisi ni waongo..! Nadhani tutaupata ukweli pakiwepo na kitu huru cha kuchunguza na kuelezea tukio hili bila ya kuegemea upande wowote.

Mi sijafanya Uchunguzi nimenukuu taarifa iliyotolewa na Gazeti la Mwananchi kama huna imani nami nunua na soma kwenye habari inayohusu kukamatwa kwa watu 40 kuhusiana na mauaji hayo.
 
"Askari hawa walikuwa katika doria ya kawaida, walimkamata mwenye bodaboda na alikuwa anagoma kutii amri na wakati wanabishana alitoa kisu ndipo askari huyo akampiga risasi," alisema kamanda huyo.

Siku zote polisi ni waongo na wamefuzu katika kutunga na kusema uongo. Na bosi wao ndiye baba wa huo uongo.
Mwananchi akichomoa kisu ndo anapigwa risasi ya kichwa?

Nadhani huko kwenye vyuo vyao vya polisi hawafundishwi mafunzo ya ukakamavu, bali ni siasa za kuilinda ccm kwakuwa wanajua hata wakiua raia hakuna mtu wa kuwachukulia hatua.
 
Hatuwezi kuupata ukweli kama kila mtu atakuja na uchunguzi kama wa kwako: Polisi maelezo yao mistari miwili na ya wananchi mengi kama ulivyofanya. Unatoa hoja na mwisho una conlude - polisi ni waongo..! Nadhani tutaupata ukweli pakiwepo na kitu huru cha kuchunguza na kuelezea tukio hili bila ya kuegemea upande wowote.

...watu wengine mmekuwa wangojwa wa tume....jana nimemwona mbwa wa jirani akimla kuku wa mama mwenye nyumba,ndugu Katalina unaweza kutusaidia kupata tume ya kuchunguza hili tukio ili tujue huyu mbwa alimtafuna kuku kwa meno ya juu au ya chini?...
 
"Askari hawa walikuwa katika doria ya kawaida, walimkamata mwenye bodaboda na alikuwa anagoma kutii amri na wakati wanabishana alitoa kisu ndipo askari huyo akampiga risasi," alisema kamanda huyo.
Huyu RPC ni kiboko, amejuaje hayo ya kutoleana visu na kupigana risasi wakati wahusika wote wawili wamefariki?
Au yeye ni kigagula na anaweza kuwasiliana na marehemu? mwaka huu tu unakwisha huku tukiendelea kushuhudia killa aina ya sinema kutoka policcm.
 
Wao wakiua hata kama ni kwa makusudi watapindisha mambo kwel, lakin kwan nn sisi tukiwaua wanatukamata, nani anaejua kuwa sheria ipo mikononi mwa police mnatua silaha kutuangamiza wakati mnalipwa mshahara kwa kujumu la kutulinda sisi na mali zetu
 
Ni vigumu sana kuupata ukweli kwa kuwa wahusika wakuu wameshatangulia mbele ya haki!!

...mbona unainyima uhuru akili yako!?...asili ya ukweli ni kuwa wazi ila watu ndo tunatabia mbaya ya kujaribu kuuficha ukweli...na kwa kuwa ukweli huwa haujifichi lazima iposiku tutake ama tusitake utajidhihirisha tu...hao waliotangulia mbele za haki sidhani kama watakuwa wameondoka pia na ufaham za walioshuhudia tukio hilo mwanzo mwisho...
 
Back
Top Bottom