Nani Mkweli Juu ya Mauaji ya Polisi Ngara?

Nani Mkweli Juu ya Mauaji ya Polisi Ngara?

Hatuwezi kuupata ukweli kama kila mtu atakuja na uchunguzi kama wa kwako: Polisi maelezo yao mistari miwili na ya wananchi mengi kama ulivyofanya. Unatoa hoja na mwisho una conlude - polisi ni waongo..! Nadhani tutaupata ukweli pakiwepo na kitu huru cha kuchunguza na kuelezea tukio hili bila ya kuegemea upande wowote.

Sasa wewe unayeshabikia polisi kuwa ndio wakweli tuambie huyo rpc alipata hayo maelezo toka kwa malehemu polisi? Mbona kila kitu mnaleta siasa? Akiuawa raia sawa wakiuawa polisi tume ya watu zaid ya 10,umefika wakti polisi watimize wajibu wao wa kulinda raia na sio kuua raia. Eti kisu kimfanye askali amuue raia,ni mafunzo ya polisi gani hiyo km sio upuuzi. Ni mpaka auawe ndugu yako ndio utambue makosa ya polisi?
 
Ni ajabu kusikia mwema anatetea wananchi,anajua polisi wake wote ni mbumbumbu wamefeli form 4,wanavuta bange,wanakula mirungi hapa Arusha,wanawaazima majambasi silaha kufanya uhalifu hapa moshi,acha wafe wote tulindwe na jwtz
 
Inasikitisha sana,matendo maovu ya askari yasiyo kemewa na viongozi wenye dhamana na hata askari wanaofanya vitendo hivyo vya kinyama kutochukuliwa hatua ndy kumetufikisha hapa.
Vitendo vyote ni vyakukemewa wananchi hawakuwa na haki ya kufanya haya km ambavyo askari hawakupaswa kufanya hivyo.
Ni lazima kitu kifanyike kulibadilisha jeshi hili,ninadhani ni wakati wa dhaifu kuazima akili na kufanyia kazi yale mapendekezo ya CHADEMA.
 
poleni sana watanzania, kodi yenu inalipa majambazi ili yawnyanyase na kuwaua, chukueni hatua kama hao raia wa ngara walivyo fanya ili wajue mmechoka.
 
Mkuu Police ni kiboko kwa ku{c}ingizia.. Mie nina mfano hai kabisa.. Walikamatwa jirani zangu wawili ndani kwao katika operation ya kumtafuta mwizi.. Walitonywa kuwa huyo wanaemtafuta analala humo.. Walipoenda hawakumkuta mtu wao wakaamua kuwakamata hao jirani wawili.. Baadae katika kuwapiga na kuwalazimisha kusema wakamvunja mmoja mguu kwenye goti.. Ndugu zake huyo alievunjwa goti wakaja juu.. Kilichotokea ni kupewa ke{c}i ya uvunjaji wa kutumia nguvu na kwamba walikamatwa kwenye eneo la tukio la ujambazi..! Huwezi kuamini walikaa ndani miezi sita na ke{c}i ikaisha kwa gharama kubwa sana..! Hiyo ilitosha kunipa sababu ya kutowaamini Police maisha yangu yote..

Niki{c}ikia jambazi au majambazi yameuawa katika "majibishano" ya risasi na Police nina{c}ikitika kwa kuwa ninaamini hao waliouawa {c}iyo majambazi.. Ila wameuawa na majambazi walio na magwanda..
Hiki ni nini?
Je c ni sawa na s, naogopa kukwambia urudi darasa la kwanza.
 
Samahani afande, nadhani hayo mawili si sawa kimaelezo wala kisheria. Wosia anaandika mtu kabla hajawa marehemu, kwamba kilitolewa kisu, mtu hawezi kusema kabla wala baada ya kufa, isipokuwa kama amesalimika au alikuwa shahidi wa pembeni.
hakuna ubishi askari wameuwawa kinyama na askari wameua raia,cha msingi ni kusubiri tume ije ichunguze na kutoa mapendekezo na maoni kuhusiana na jinsi ya kushughulikia matukio ya aina hiyo yasitokee tena.pia katika matukio ya namna hiyo wapo baadhi ya watu wameona tukio zima na wapo tayari kutoa ushahidi.swala la nani anauwezo wa kuwasiliana na marehemu siyo issue,mbona usia wa marehemu unakubalika akisha kufa kama ushahidi sembuse madai ya mtu kutolewa kisu?.kama tunaweza kukubali usiwa wa marehemu kwanini tusikubali mambo mengine?.kama unaushahidi peleka ktk tume iliyoundwa usaidie,kama huwezi kufikisha ujumbe/ushahidi wako basi ukubaliane na majibu ya tume.
 
Sasa polisi akiwa mkweli hiyo rushwa ataipataje?! mimi niliswekwa lupango juzijuzi hapo chang'ombe kituo cha kanda ya temeke, wallahi niliyoyakuta humo balaha! sero zimejazwa watuhumiwa wa kesi ziso kichwa wala miguu eti kuingia bure kutoka pesa. Tena mkuu wa kituo ndio anaongoza mashambulizi ya kudai hela na ukikataa kutoa pesa kesi yako inabadilishwa unabambikwa kesi babkubwa kama ya armed robbery au murder!

Nikawakumbuka takakakuru nikisema ebu wajifanye watuhumiwa wawekwe lupango ili wakidaiwa pesa wawape za moto, lakini mtu mmoja akanijuza eti takakakuru wakijaribu kuwakamatia kituoni kwao wanawapiga risasi na kusingizia wameua jambazi aliyetaka kumnyang'anya siraha polisi
 
Huyu RPC ni kiboko, amejuaje hayo ya kutoleana visu na kupigana risasi wakati wahusika wote wawili wamefariki? Au yeye ni kigagula na anaweza kuwasiliana na marehemu? mwaka huu tu unakwisha huku tukiendelea kushuhudia killa aina ya sinema kutoka policcm.
POlis wanaingia ktk mtihani mwingine, mwema asipotumia akili na kujiandaa fidia wafiwa ,huku akitakiwa wapa memo polisi upesi wajifunze kuwa na adabu na wasitegemee tena ulinzi wa kijinga wa jeshi la polisi kwa uongo, atapelekea polisi wengi zaidi kuuwawa, na hao watu wa huo ukanda bado wana kumbukumbu za vita.Ujinga wa polisi unaweza kuw ani mwanzo wa vita full ambayo polisi hawata iweza. Mbaya hii habari imeshafungua vichwa vya raia, polisi watapigia simu ili wakauwawe, watauwawa uraiani.Watauwawa ktk guest house, watauwawa ktk pombe na madisco.Mwema aache usanii kwa issue very serious kama hii, ni matukio amabyo jeshi la polisi walipaswa omba yasitokee.Kwani majibu yoyote yatakayotoka bado raia wameshajifunza kitu, hakuta tofauti na kumwonyesha mtoto picture ya ngono, hatoacha itafuta kuitazama hata kama utamwambia ni mbaya.
 
Maelezo ya kamanda wa polisi hayaingii akilini kwa kweli:confused2:
 
Polisi hawaaminiki tena. hii kwa wenye akili inatumbia wananchi wamechoka na ccm wataangamiza Taifa kwa kutumia polisi kisiasa
Tamko la kamanda wa
Polisi


“Askari hawa walikuwa katika doria ya kawaida, walimkamata mwenye
bodaboda na alikuwa anagoma kutii amri na wakati wanabishana
alitoa kisu ndipo askari huyo akampiga
risasi,
” alisema kamanda huyo.

Hata hivyo, alisema kituo hakikuteketea chote, na kwamba hata nyaraka
zilizoungua ni chache.

Tamko la Mashuhuda Wananchi

Awali, ilielezwa na mashuhuda kuwa, chanzo cha mauaji hayo ni kuwa
polisi walifika katika Kijiji cha Mugoma kwa lengo la kukagua pikipiki
mbovu na zisizokuwa na usajili na walifika katika gereji moja na kukuta
mmiliki wa gereji hiyo akitengeneza pikipiki, kumtaka aipeleke kituoni
kwa maelezo kuwa ilikuwa mbovu.

Baada ya hapo, fundi aligoma kutekeleza agizo hilo na polisi mmoja
alimpiga risasi, kitendo ambacho kiliamsha hasira kwa wananchi waliokuwa
jirani na eneo hilo.

Ilielezwa na mashuhuda kuwa baada ya tukio polisi aliyefyatua risasi
alikimbilia kujificha katika nyumba iliyopo jirani na gereji hiyo, huku
akimuacha mwenzake.

“Wananchi walimvamia yule askari aliyebaki pale gereji na kuanza
kumcharanga kwa mapanga na kumpiga mawe hadi akafa,” alisema mmoja wa
mashuhuda.

Alifafanua kwamba baada ya kuhakikisha kuwa wamemuua, wananchi hao
walikwenda katika nyumba aliyojificha askari aliyekimbia, kutaka
kuichoma moto iwapo angegoma kutoka.

“Mmiliki wa nyumba ile baada ya kuona wananchi hao wanataka kuichoma
moto nyumba yake alimtaka askari huyo kutoka nje, alipotoka tu wananchi
walimvamia na kuanza kumpiga mawe na kumuua,” alisema.

Kituo cha polisi kilichoteketezwa kwa moto, kipo karibu na mpaka wa
Tanzania na Burundi.


My Take!
Hivi inapoteza heshima ipi iwapo hawa viongozi wetu wa Polisi watakuwa
wakweli? Kauli yake hii inataka kuaminisha umma kwamba huyu raia
aliyeuawa alitaka kuwadhuru Polisi ndo wakachukua hatua ya Kumuua

CHANZO GAZETI LA MWANANCHI
 
Taarifa zipi ambazo utazipata katika nchi hii zilizotafitiwa kitaalam ndugu? Ya Ulimboka, Ally Zona(Moro) Mwangosi, Taarifa zake unazo? na umeziamini? je kama uziamini unategemea taarifa za kitaalam zitoke wapi.
kwa hiyo unataka kuniambia kwamba tanzania hamna uwezekano wa kupata taarifa sahihi juu ya mambo?
 
Hiki ni nini?
Je c ni sawa na s, naogopa kukwambia urudi darasa la kwanza.

Mkuu wewe ni Mwalimu wa Kiswahili..? Mbona sasa umenisahihisha huku ukiwa umekosea..?

Unapoandika kwa kuuliza "hiki nini" unamaanisha kitu gani..? Sentensi katu haiwezi kuwa addressed kama "hiki"..!

Ukaendelea kuandika "je c ni sawa na s,".. Mkuu uko sawa hapo kweli.. Umeandika katika form ya swali lakini mwisho umeweka alama ya koma..?

Anyway Mkuu ninapenda kuwa tofauti kidogo kwenye maandiko yangu (ambayo sio rasmi).. Kwa hiyo c imekuwa kama signature yangu.. Nashangaa hujaisemea hizo nukta mbili zinafuata baada ya kumaliza sentesi..

Mwisho Mkuu ni vizuri kuangalia ujumbe na sio maandishi.. Official letters huwezi kukuta haya but hapa JF yamejaa tele..
 
Tamko la kamanda wa Polisi

“Askari hawa walikuwa katika doria ya kawaida, walimkamata mwenye bodaboda na alikuwa anagoma kutii amri na wakati wanabishana alitoa kisu ndipo askari huyo akampiga risasi,” alisema kamanda huyo.

Hata hivyo, alisema kituo hakikuteketea chote, na kwamba hata nyaraka zilizoungua ni chache.

Tamko la Mashuhuda Wananchi

Awali, ilielezwa na mashuhuda kuwa, chanzo cha mauaji hayo ni kuwa polisi walifika katika Kijiji cha Mugoma kwa lengo la kukagua pikipiki mbovu na zisizokuwa na usajili na walifika katika gereji moja na kukuta mmiliki wa gereji hiyo akitengeneza pikipiki, kumtaka aipeleke kituoni kwa maelezo kuwa ilikuwa mbovu.

Baada ya hapo, fundi aligoma kutekeleza agizo hilo na polisi mmoja alimpiga risasi, kitendo ambacho kiliamsha hasira kwa wananchi waliokuwa jirani na eneo hilo.

Ilielezwa na mashuhuda kuwa baada ya tukio polisi aliyefyatua risasi alikimbilia kujificha katika nyumba iliyopo jirani na gereji hiyo, huku akimuacha mwenzake.

“Wananchi walimvamia yule askari aliyebaki pale gereji na kuanza kumcharanga kwa mapanga na kumpiga mawe hadi akafa,” alisema mmoja wa mashuhuda.

Alifafanua kwamba baada ya kuhakikisha kuwa wamemuua, wananchi hao walikwenda katika nyumba aliyojificha askari aliyekimbia, kutaka kuichoma moto iwapo angegoma kutoka.

“Mmiliki wa nyumba ile baada ya kuona wananchi hao wanataka kuichoma moto nyumba yake alimtaka askari huyo kutoka nje, alipotoka tu wananchi walimvamia na kuanza kumpiga mawe na kumuua,” alisema.

Kituo cha polisi kilichoteketezwa kwa moto, kipo karibu na mpaka wa Tanzania na Burundi.


My Take!
Hivi inapoteza heshima ipi iwapo hawa viongozi wetu wa Polisi watakuwa wakweli? Kauli yake hii inataka kuaminisha umma kwamba huyu raia aliyeuawa alitaka kuwadhuru Polisi ndo wakachukua hatua ya Kumuua

CHANZO GAZETI LA MWANANCHI

Polisi imekuwa genge la wahuni
 
Back
Top Bottom