Nani mkubwa ndani!

Tetra

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
1,521
761
Fatuma alimtazama Eric,,kwa muda mrefu,,alikumbuka mengi waliyopitia.Alikumbuka mara ya kwanza walipokutana na Eric..jinsi Eric alivyokuwa mpole,msikivu na mtulivu sana.Fatuma alikumbuka zaidi siku ya arusi yao,kila kitu kilionekana safi,salama na chenye matumaini.Kweli walipendana sana!
::
Fatuma alikuwa ni mwanamke mwenye akili sana.Aliweza kujadili mambo kwa busara sana.Eric aliona fahari sana kumtambulisha kwa rafiki zake.Lakini sasa mambo yanaonekana yamebadilika.Eric hafurahii tena.Hata Fatuma anapotoa maoni au shauri,Eric anajibu tu.."Je,unataka kunifundisha! Jali kazi yako!.."
::
Fatuma hakupenda ndoa yao yenye mwaka mmoja tu ikose mawasiliano.Alifikiri kwa muda,aliona kuwa madam wote wanapata mshahara mzuri,,basi wajadili juu ya matumizi ya hela yao,kwani pesa ilikuwa inatoka upesi zaidi nyumbani kuliko ilivyoingia.
::
Usiku mmoja baada ya chakula cha jioni,Fatuma alimfuata Eric akamwambia "Mume wangu,unaonaje kama tutapanga namna ya kutumia fedha tunazopokea sote wawili,ili tuweke akiba ya kutusaidia baadaye?"...Bila kuinua macho kwenye laptop yake,Eric alijibu "..Kwa nini unajiingiza katika mambo ya fedha? Shughulika na jiko lako,hiyo inatosha.Ni nani mkubwa hapa ndani?.."
::
Fatuma hakupendezwa na jibu hilo,hakusema zaidi.Alijiona ameachwa nje ya uamuzi uliowahusu wote wawili.Mwezi ulipita na Eric alikuja amenunua Kamera.Fatuma hakufurahi,aliamua kusema "Mume wangu,kamera ni yako,lakini hukukumbuka hatuna kitanda kwenye chumba cha wageni,hatuna mapazia sebuleni naona aibu wageni wakija,inaonekana sijui kutunza nyumba?"..Eric alimkata kauli Fatuma,akamjibu kwa ghadhabu "Unaanza tena kunifundisha! Kutunza nyumba,mimi ndie kichwa cha familia sio we mwanamke! Ni nani mkubwa ndani?"
::
Fatuma aliumia.Aliona hana nafasi katika nyumba ambayo alidhani ni yao wote.Alijua namba ya siri ya akaunti zao.Alijisemea "ntaenda kwa rafiki zangu,ntanunua nguo,ntapitia club nikajirushe,nile vizuri hotelini,,Eric atajifunza kwamba KAMA yeye ni mkubwa basi SI mkubwa wake Fatuma"
Naam,,Eric aliwaza "KUNIFUNZA MIMI,MWANAMKE?" Fatuma aliwaza "NANI MKUBWA?"
=
Ndugu wana Jf nani mkubwa katika nyumba hii?
 
Dero

JF-Expert Member
Dec 2, 2010
328
188
Hadithi hii amekufundisha nani?

Kwamba mwanamke ana nafasi ya kutoa ushauri kwenye nyumba, na sio vizuri kumtreat kama mtoto, na mchango wa mwanamke unaleta mandeleo kwenye familia.
 
MR. ABLE

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
1,480
940
Hadithi yako ni nzuri sana, ila hujatupa umri wa kila mmoja ili tujue ni nani mkubwa
BUT in my opinion mkubwa ni Fatuma coz anamawazo mazuri kuliko huyo kalaghabao Eric.
 
Tetra

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
1,521
761
kusudio la hadithi hii ni nini, nini unachotafiti hapa?

nataka tujadiliane ni wakati gani au namna ipi njema ya kuishi na hawa tunaowaita hawawezi kutushauri kwa sababu tu tumepewa kuwa kichwa cha familia? Je ni kweli wanaume ndio wenye kauli ya mwisho?
 
Tetra

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
1,521
761
Hadithi yako ni nzuri sana, ila hujatupa umri wa kila mmoja ili tujue ni nani mkubwa
BUT in my opinion mkubwa ni Fatuma coz anamawazo mazuri kuliko huyo kalaghabao Eric.

Naam,ukubwa wa umri ni muhimu ila tujadili ktk familia ambayo tofauti ya misimamo kama hii ipi njia sahihi ya kufuata
 
Bra-joe

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
1,562
978
Yes, Eric ni mwanaume halisi wa kiafrika, hata kama mama atakuwa na mshahara na mchango mkubwa kiuchumi katika familia dume litabaki kuwa kichwa na maamuzi yake ni ya mwisho. Nafikiri wanawake wa .com wameielewa hadithi yako.
 
majany

JF-Expert Member
Sep 30, 2008
1,223
576
Fatuma alimtazama Eric,,kwa muda mrefu,,alikumbuka mengi waliyopitia.Alikumbuka mara ya kwanza walipokutana na Eric..jinsi Eric alivyokuwa mpole,msikivu na mtulivu sana.Fatuma alikumbuka zaidi siku ya arusi yao,kila kitu kilionekana safi,salama na chenye matumaini.Kweli walipendana sana!
::
Fatuma alikuwa ni mwanamke mwenye akili sana.Aliweza kujadili mambo kwa busara sana.Eric aliona fahari sana kumtambulisha kwa rafiki zake.Lakini sasa mambo yanaonekana yamebadilika.Eric hafurahii tena.Hata Fatuma anapotoa maoni au shauri,Eric anajibu tu.."Je,unataka kunifundisha! Jali kazi yako!.."
::
Fatuma hakupenda ndoa yao yenye mwaka mmoja tu ikose mawasiliano.Alifikiri kwa muda,aliona kuwa madam wote wanapata mshahara mzuri,,basi wajadili juu ya matumizi ya hela yao,kwani pesa ilikuwa inatoka upesi zaidi nyumbani kuliko ilivyoingia.
::
Usiku mmoja baada ya chakula cha jioni,Fatuma alimfuata Eric akamwambia "Mume wangu,unaonaje kama tutapanga namna ya kutumia fedha tunazopokea sote wawili,ili tuweke akiba ya kutusaidia baadaye?"...Bila kuinua macho kwenye laptop yake,Eric alijibu "..Kwa nini unajiingiza katika mambo ya fedha? Shughulika na jiko lako,hiyo inatosha.Ni nani mkubwa hapa ndani?.."
::
Fatuma hakupendezwa na jibu hilo,hakusema zaidi.Alijiona ameachwa nje ya uamuzi uliowahusu wote wawili.Mwezi ulipita na Eric alikuja amenunua Kamera.Fatuma hakufurahi,aliamua kusema "Mume wangu,kamera ni yako,lakini hukukumbuka hatuna kitanda kwenye chumba cha wageni,hatuna mapazia sebuleni naona aibu wageni wakija,inaonekana sijui kutunza nyumba?"..Eric alimkata kauli Fatuma,akamjibu kwa ghadhabu "Unaanza tena kunifundisha! Kutunza nyumba,mimi ndie kichwa cha familia sio we mwanamke! Ni nani mkubwa ndani?"
::
Fatuma aliumia.Aliona hana nafasi katika nyumba ambayo alidhani ni yao wote.Alijua namba ya siri ya akaunti zao.Alijisemea "ntaenda kwa rafiki zangu,ntanunua nguo,ntapitia club nikajirushe,nile vizuri hotelini,,Eric atajifunza kwamba KAMA yeye ni mkubwa basi SI mkubwa wake Fatuma"
Naam,,Eric aliwaza "KUNIFUNZA MIMI,MWANAMKE?" Fatuma aliwaza "NANI MKUBWA?"
=
Ndugu wana Jf nani mkubwa katika nyumba hii?

Wote watoto!!!
 
kimeloki

JF-Expert Member
Jul 9, 2012
2,713
2,692
mwanamke ana nafasi kubwa sana kuliko hata mwanaume tatizo hawezi kuwa mkuu wa boma.tafakari.
 
Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
66,436
127,460
Nini dhumuni la ndoa? Mbaya sana kuingia kwenye mkataba usioujua kwa nini unaingia.
Ndoa haiitaji ukubwa, ndoa ni kusikilizana na kuelewana.
Ndoa isipo ongozwa na Roho wa Mungu haina uhai ndani yake
 
Kaunga

JF-Expert Member
Nov 28, 2010
12,538
13,440
Nini dhumuni la ndoa? Mbaya sana kuingia kwenye mkataba usioujua kwa nini unaingia.
Ndoa haiitaji ukubwa, ndoa ni kusikilizana na kuelewana.
Ndoa isipo ongozwa na Roho wa Mungu haina uhai ndani yake

Ikikaribia jumapili huwa una akili!
 
Chimbuvu

JF-Expert Member
Jul 17, 2012
4,402
2,324
Hahahaha i wish wanawake mngejua kitu kimoja ili ndoa zenu zidumu,mfanoi umkute mwanaume anahangaika kuweka pazia huku anakosea,,usijaribu hata siku moja kwenda kumwambia umekosea fanya hivi kamwe usijaribu,muache akosee mwenyewe mpaka atakapokuuliza,huyo mwanamke alikuwa na wazo zuri lakini hapo ni sawa unamfundisha mwanaume na yeye mwanaume huwa hapendi hicho kitu,,chukua nafasi yako kama mwanamke,nyenyekea kwa mwanaume wako hiyo ndiyo silaha ya mwanamke,eg mme wako akiamua kuitupa peni chini makusudi halafu akakuambia iokote ni wanawake wangapi watatii?
 
karembo

Senior Member
Nov 2, 2012
129
44
Nini dhumuni la ndoa? Mbaya sana kuingia kwenye mkataba usioujua kwa nini unaingia.<br />
Ndoa haiitaji ukubwa, ndoa ni kusikilizana na kuelewana.<br />
Ndoa isipo ongozwa na Roho wa Mungu haina uhai ndani yake
Amina mtumishi....Mungu akutunze, shalom
 
karembo

Senior Member
Nov 2, 2012
129
44
Hahahaha i wish wanawake mngejua kitu kimoja ili ndoa zenu zidumu,mfanoi umkute mwanaume anahangaika kuweka pazia huku anakosea,,usijaribu hata siku moja kwenda kumwambia umekosea fanya hivi kamwe usijaribu,muache akosee mwenyewe mpaka atakapokuuliza,huyo mwanamke alikuwa na wazo zuri lakini hapo ni sawa unamfundisha mwanaume na yeye mwanaume huwa hapendi hicho kitu,,chukua nafasi yako kama mwanamke,nyenyekea kwa mwanaume wako hiyo ndiyo silaha ya mwanamke,eg mme wako akiamua kuitupa peni chini makusudi halafu akakuambia iokote ni wanawake wangapi watatii?

Mimi nitatii...nitainama na kuiokota kwa unyenyekevu.
 
mmang'ula

Member
Nov 27, 2012
22
3

<br />
<br />
Mimi nitatii...nitainama na kuiokota kwa unyenyekevu.
Huna lolote au ndo unajipigia promo?
 
Donnie Charlie

JF-Expert Member
Sep 16, 2009
12,670
11,776
wamekutana wawili ambao hawaendani kitabia, hapo nadhani kila mmoja anatakiwa afikiri + na wakubaliane au atafute wa kufanana nae
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Top Bottom