Baada ya ugomvi wa muda mrefu, mke alianza kukusanya nguo na vitu vyake vingine tayari kwa kuondoka, mume akamuuliza mbona wakusanya vitu unaenda wapi? Mke, akajibu kwa ufupi, 'naenda kwa mama!' kuona hivyo mume nae akaanza ukusanya vitu vyake, ndipo mke akamuuliza kwa ukali! 'sasa na wewe unaenda wapi?' kwa upole mume akajibu, naenda kwa mama pia! Mke akauliza tena akiwa ameghadhibika! 'watoto hawa wataishi na nani sasa? Mume akajibu! Na wao waende kwa mama yao!