Elections 2010 Nani kuiwakilisha CHADEMA 2010?

Mwiba vipi rafiki? kama una ujumbe wa uhakika tupo habari. JF ni sehemu ya kupashana habari wewe unaficha! Sema tukupe mji gani ili utegue hicho kitendawili?
 
Mwiba, nafikiri kufanya hivyo (vyama kinzania kujiunga pamoja na kumtoa mgombea mmoja) kutakuwa mithili ya uvuvuzela, per excellence! Kimbunga! Lakini baada ya Uchaguzi Mkuu, makapi yaaanza kudondoka chini moja, moja na kusambaratika kwa umoja huo ki-vyama!
 
Wadau ninauliza kuhusu hiyo mada,kama ndiyo naombeni sababu.
Ndugu Kamaka, siyo tu ni muhimu kwa Chadema kusimamisha mgombea wa urais bali ni lazima, kwa kutosimamisha mgombea watu wengi watakuwa wamenyimwa haki yao kumchagua kiongozi makini kutoka chama makini. Ukizingatia kwamba vyama vingi vya upinzania ikiwemo chadema havijafanikiwa kuweka mzizi wa wanachama na viongozi mpaka matawini(siyo lazima sana) hivyo mgombea urais anakuwa kiunganishi muhimu sana kwa wagombea ubunge majimboni na udiwani katani.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom