Nani kinara wa kukandamiza demokrasia kati ya nchi za Afrika mashariki?

mpk

JF-Expert Member
Sep 26, 2012
3,115
3,863
Ukiondoa Kenya ambayo upinzani umewahi kuchukua dola lakini pia uwiano wa upinzani na chama tawala umekaribiana sana katiki uwakilishi bungeni na ngazi nyingine. Nchi zilizobaki hakuna demokrasia na chaguzi ktk nchi hizo ni kuharalisha 'madikiteta' kuendelea kuzikalia nchi hizo.

Tanzania, Uganda, Burundi na Rwanda nchi zote hizi zinafanana ktk njia moja au. nyingine. Burundi na Zanzibar mfano zinafanana baada ya viongozi wao kukatalia madarakini kinyume cha matakwa ya wananchi. Uganda baada ya Mseveni kushindwa na kujitangaza kwa nguvu amemuweka kizuizi cha Nyumbani mpinzani wake Dr Besigye mpaka leo

Hivi huyu ana tofauti gani na hapa kwetu ambako baada ya watawala kuhisi kuanguka walienda kukamata kompyuta za waliokuwa wanajumlisha matokeo makao makuu ya Chadema na kituo cha haki za binadamu?

Huko Rwanda Kagame anaongeza mihula kwa kura za bandia zinazoratibiwa kuupumbaza ulimwengu. Alimfunga mpinzani wake Mama Ingabile kwa makosa ya kutunga mpaka leo mama wa watu anaoza korokoroni.
 
Ukiondoa Kenya ambayo upinzani umewahi kuchukua dola lakini pia uwiano wa upinzani na chama tawala umekaribiana sana katiki uwakilishi bungeni na ngazi nyingine. Nchi zilizobaki hakuna demokrasia na chaguzi ktk nchi hizo ni kuharalisha 'madikiteta' kuendelea kuzikalia nchi hizo.
.

Kenya hakuna demokrasia kuna ukabila.Makabila ya wakikuyu na kalenjini wako na kenyatta,Makabila ya wajaluo na jamii zao wako ODM na Raila ODINGA.
Vikabila vidogo vilivyobaki viko CHAMA CHA KANU
Mjaluo akienda kugombea kwa wakikuyu hashindi na mkimkuyu akienda gombea ujaluoni hashindi.

Uwiano uliopo ni nguvu ya makabila na kura hupigwa kwa misingi hiyo.

Mfumo huo wa kikabila ndio unaotumiwa na CHADEMA na CUF.Zanzibar CUF kinaeleweka ni chama cha kabila gani.Na bara CHADEMA kinaeleweka ni cha kabila gani.
 
Kenya hakuna demokrasia kuna ukabila.Makabila ya wakikuyu na kalenjini wako na kenyatta,Makabila ya wajaluo na jamii zao wako ODM na Raila ODINGA.
Vikabila vidogo vilivyobaki viko CHAMA CHA KANU
Mjaluo akienda kugombea kwa wakikuyu hashindi na mkimkuyu akienda gombea ujaluoni hashindi.

Uwioano uliopo ni nguvu ya makabila na kura hupigwa kwa misingi hiyo.

Mfumo huo wa kikabila ndio unaotumiwa na CHADEMA na CUF.Zanzibar CUF kinaeleweka ni chama cha kabila gani.Na bara CHADEMA kinaeleweka ni cha kabila gani.
Umetoka nje ya mada..
 
Kwa demokrasia, usalama na utulivu wa nchi Tanzania huwez kuilinganisha na hizo nchi zingine. Tuko Juu sana. Hizi kasoro ndogo ndogo hazina maisha zitafutika tu katika uso wa nchi hii.

I
 
Tanzania ndio kinara ukisema tu wanakubanda?!
Sahz wanahabar kimyaaaaaa!! Wamekazana majipu majipu kansa hawazioni!!
 
Kwa demokrasia, usalama na utulivu wa nchi Tanzania huwez kuilinganisha na hizo nchi zingine. Tuko Juu sana. Hizi kasoro ndogo ndogo hazina maisha zitafutika tu katika uso wa nchi hii.

I
Demokrasia, usalama, na huo utulivu unaouzugumzia upo Juu kivipi? Watu wanaojaribu kusimama ktk haki wnakufa kimya kimya Na kuteswa sana, acha kutibua vilivyo lala
 
Mie nadhani Tanzania tunaongoza kwa kivuli cha amani. Unyenyekevu, upole na uvumilivu umewadhihirishia viongozi wetu kubaka demokrasia...
 
Back
Top Bottom