Nani kasema Dongo Fleva imekufa? Sikiliza hizi..

Nani kasema Dongo Fleva imekufa? Sikiliza hizi..

Covid-19

Senior Member
Joined
Mar 2, 2020
Posts
162
Reaction score
365
Imepita muda kidogo tangu niache kufuatilia mziki wa hapa nyumbani kutokana na wafalme wenu Ally na Naseeb kuimba vitu visivyoeleweka vyenye maigizo mengi.

Sasa leo wakati napita barabarani nikasikia kijana mmoja kwenye kibanda cha kukodisha CD analalamika kwa hisia kali za mapenzi, nikasogea kujiridhisha kama ni mtu anaimba live au ni radio inapiga. Basi nikakuta ni flash inapiga wimbo wa msanii ambaye mwenye kibanda aliniambia anaitwa B2K unaitwa '' HIVI KWA NINI''.

Ikanibidi nimwambie aniwekee kwenye flash yangu ili nikausikilize vizuri nyumbani lakini wakati naondoka dogo wa kibandani akanipa nyimbo nyingine mbili za msanii anaitwa KAYUMBA na nyimbo zake 'MAZOEA'..

Hakika baada ya kuzisikiliza nimeona kuna uwezekano mkubwa wa bongo fleva ya miaka ya 2000 kurudi tena kama DJ'S wetu wataamua kutoa support kwa vijana na kuachana na hawa waganga njaa wanaojiita wafalme.

Kama kuna wimbo mwingine wowote mzuri wa Upcoming niwekee hapa nikasikilize nipate fleva za bongo nilizozikosa kitambo.
 
Uyo b2K anajua sana ana ngoma nzuri kama tunaendana, mama, uhakika, vipi, na mwambie hzo ni ngoma nnazozkubali kutoka kwa uyo jamaa sema ana nyota ya best naso ngoma zake znapigwa kwenye mabasi ya mkoani tuu na vijijini ila redioni sjawahi kumskia kabsaaa
Ngja niitafute hyo nymbo
 
  • Thanks
Reactions: BRN

Similar Discussions

Back
Top Bottom