Nani Kamdanganya Rais wetu?

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
55,499
86,036
Hapa sizungumzii siasa za uchaguzi ila naomba kuuliza swali la msingi kabsaaa...kwamba nani aliemdanganya Raisi wangu kuwa UKIMWI ni ugonjwa wa kujitakia?? ( Hapa ilikuwa wakati Raisi anatoa speech ya kuzima mwenge jana)

Baada ya kusikia jana kwa masikio yangu mawili na kusikia tena leo asubuhi kwenye redio wakati wa taarifa, nimeshawishika kuamini kuwa maneno haya yanayotolewa na Rais huyu yana mkono wa mtu, haiwezekani arudie jambo lile lile kila siku.

Yawezekana kabsaa kuna watu/ washauri either wa kisiasa au kidini/jamii wamemfanya aamini kuwa UKIMWI ni gonjwa la kujitakia, akiusahau UKWELI kuwa wapo walioambukizwa wakiwa kazini katika kuwahudumia wengine, na wengine na kwenye ajali, wengine ni wale wezee wa watu maskini kule kijijini akimhudumia mwanawe pasi kujua njia ya kujizuia, je hawa nao wamejitakia?

Ni kweli kuwa tukishika maneno ya viongozi wetu wa dini tutapona kama ulivyodai mheshimiwa? Mbona sasa na wao wanakufa? Je, watotoyatima na ambao pia ni Positive nao wamejitakia?

Naombeni, nipeleekeeni ujumbe huu kwa RAIS wangu kuwa, kwa hili ameniuumiza sana, apate muda asikilize na kusoma Speech ya Nkosi kijana wa miaka kumi na moja na ambaye sasa ni marehemu, je na yeye alijitakia? na yeye ni kiherehere chake???

Mungu Tuokoe kwa NEEMA yako tu

Click hapa usome hii

http://www.beholders.org/spirit/inspirationalpeople/110-nkosijohson.html
 
Amechanganyikiwa!!!
 
wala sishangai kwani hajui hata kwa nini watanzania ni maskini wakati anawakumbatia mafisadi na wabadhirifu wa mali na huduma za uma
 
Aibuu . Raisi aisyejua maana ya HIV na jinsi inavyoambukizwa ..Hopeless
 
Kila neno baya alisemalo binadamu kwa kuwaonea watu wengine, majibu yake hupatikana mapema. Siku mpendwa wake atakapougua maradhi hayo hata kama kwa kujitakia kama anavyosema, atajifunza kwa nini hotuba zake za ukimwi kuita ugonjwa wa kujitakia zinawaumiza watanzania.
 
Poleni sana ndugu zangu "Wapendwa" nawapa pole nikijua kuwa mliowengi hamkuwahi kuwaza kujikuta katika hali hiyo. lakini pole zaidi kutokana na maneno ya kashfa mnayoyapata kuanzia kwa watu wasio na ulewa hadi kwa wale wenye madaraka makubwa nchini, eti kwamba kupata kwenu UKIMWI ni kiherere chenu; mimi nakataaa.

Naomba sana soma Speech hii, na kisha mpeleke na mwingine, kijana huyu aliwatoa machozi UN sijui huyu anaewakashifu kama aliiona hii.

http://www.beholders.org/spirit/inspirationalpeople/110-nkosijohson.html
 
unamshangaa hilo? when it comes to prevention of communicable diseases JK ni bogus mno. inawezekana ama hasikilizi ushauri wa wataalamu au hana wataalamu wenye nia njema naye. jiulize alitumia pesa kiasi gani kupigia mbu muziki pale leaders club!
 
"Care for us and accept us- we are all human beings.We are normal. We have hands. We have feet. We can walk, we can talk, we have needs just like everyone else- don't be afraid of us- we are all the same!"

Nkosi Johnson - 13th International AIDS Conference - Durban
 
unamshangaa hilo? when it comes to prevention of communicable diseases JK ni bogus mno. inawezekana ama hasikilizi ushauri wa wataalamu au hana wataalamu wenye nia njema naye. jiulize alitumia pesa kiasi gani kupigia mbu muziki pale leaders club!
Dah,, ule mziki ulisadia sana bwana, acha utani, si ndio mbu wakazaliana wakafika mpaka Muhimbili, au umeshasahau....mbu wakubwa kama nzi!!!
 
jk, anamatatizo makubwa,
nawaomba watu wanaoishi na virusi ya hiv, waandamane kupinga kauli yake huu jamaa
 
Back
Top Bottom