Nani kama Mke

Nani kama Mke

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,038
Reaction score
34,743
Utenzi.

NANI KAMA MKE.

Hodii ndugu zanguni,
Naingia uwanjani,
Kuwaletea maoni,
Mke kumfagilia.


Nataka kuweka wazi,
Kati yake na mzazi,
Nani hasa ana kazi,
Ukubwani kifikia.


Ya mama tumeyaona,
Kazi yake kubwa sana,
Hapa si pakubishana,
Rai tunaangalia.


Mama yetu metulea,
Mazuri metutendea,
Huruma metuonea,
Abishae kapungua.

Nuru yake huizimi,

Hata akiwa hahemi,
Mwenginewe hasimami,
Fadhilaze kuchukua.

Bali mefika wakati,
Mazingira tofauti,

Huduma kwake hupati,
Kwa mke yamehamia.

Mke ndie kila kitu,

Huyu mtoto wa watu,
Heshima huruma utu,
Mebeba masuulia.

Mke hukusafishia,
Usafi hukufanyia,
Kufua na kufagia,
Chumba hukuandalia.


Hutizama nyumba yako,
Wewe na watoto wako,
Na hutunza mali yako,
Isije ikapotea.


Chakula hukupikia,
Muda akasubiria,
Pindi unaporejea,
Mezani hukuwekea.

Hukuingiza bafuni,
Na tauloyo begani,
Maji ya moto ndooni,
Kitambo mekwandalia.

Nguo safi sandukuni,

Zimepangwa kwa makini,
Zingine zikabatini,
Utakazo wachagua.

Hukuulizia hali,
Mnapokuwa wawili,
Vipi kazini amali,
Upole aulizia.

Akili akuliwaza,

Hasirazo hutuliza,
Mwilio aupumbaza,
Machovu ayaondoa.

Mke ndie kinga yako,

Kwa watu wake na wako,
Meshika mikono yako,
Daima akutetea.

Mke pekee mwenzako,
Ajuae siri zako,
Yeye mshirika wako,
Mkataba mmetia.


Siri zako za nguoni,
Mwinginewe hazioni,
Za chumbani na chooni,
Ni mke anayejua.

Siku ukiwa na homa,
Mkeo takutizama,
Sio tena yule mama,

Takae kuangalia.

Mke ninaemsema,
Ni mke alie mwema,
Dini alieisoma,
Haki ya mume ajua.

Si wale viruka njia,

Nyumbani waloingia,
Tamaa na yao nia,
Uchumi mejipangia.

Na sio mlogombana,

Talaka mkaachana,
Huyo sie mke tena,
Wajibu memwondokea.

Kumbuka mama ni mke,
Msichana enzi zake,

Babako mpenzi wake,
Maisha wamepitia.

Na mke nae ni mama,
Kwao ameshapahama,
Watotoe atizama,
Ana yake familia.


Kwa sasa ana daraja,
Ya mke hiyo ni moja,
Na ya mama nayo yaja,
Mbili tajinyakulia.

Mke ninamsifia,

Si wangu na wako pia,
Wema wanotufanyia,
Hakuna wa kufikia.

Hayo ni maoni yangu,

Metoa kichwani kwangu,
Sijui nyinyi wenzangu,
Vipi mnachukulia.

Sijapunguza ya mama,
Daraja yake ya wema,
Bali mke metizama,
Sifa anastahilia.


Hapa beti nasimama,
Yatosha niliyosema,
Sifa za mke na mama,
Zote nimewatajia.
 
Haaaa labda malaika waje waniambie nioe lakini huko uliko hongera xana
kwanza hongera kwa kazi nzuri ya kisanaa
Tunga wa mabachera msifie mama nitafurahi zaidi ya hapa
 
Kwa mabachela sasa.


naingia bila hodi
hata salam siwapi
kweli nimetahamaki
kuona huo utenzi

kuwa na mke si dili
dili kuwa peke yako
mzizi hajaelewa
kwa kuwa ameshaoa


ukapela raha sana
tena unakuwa huru
hakuna wakuzingua
gheto uko peke yako


wala kupika sipiki
nakula kwa mama lishe
na kufua nikichoka
nazipeleka kwa dobi.


nikichelewa kurudi
sina wa kuniuliza
wala wa kunilaumu
ninaishi pekeyangu.
 
Kwa mabachela sasa.


naingia bila hodi
hata salam siwapi
kweli nimetahamaki
kuona huo utenzi

kuwa na mke si dili
dili kuwa peke yako
mzizi hajaelewa
kwa kuwa ameshaoa


ukapela raha sana
tena unakuwa huru
hakuna wakuzingua
gheto uko peke yako


wala kupika sipiki
nakula kwa mama lishe
na kufua nikichoka
nazipeleka kwa dobi.


nikichelewa kurudi
sina wa kuniuliza
wala wa kunilaumu
ninaishi pekeyangu.

Asanteeeee
 
Nzuri.. Japo sio kila Mwanamke au Mke ana sifa hzo.. Huyo ni Mke Mwema so ingefaa pale juu uweke "Mke Mwema" nzuri
 
Kwa mabachela sasa.


naingia bila hodi
hata salam siwapi
kweli nimetahamaki
kuona huo utenzi

kuwa na mke si dili
dili kuwa peke yako
mzizi hajaelewa
kwa kuwa ameshaoa


ukapela raha sana
tena unakuwa huru
hakuna wakuzingua
gheto uko peke yako


wala kupika sipiki
nakula kwa mama lishe
na kufua nikichoka
nazipeleka kwa dobi.


nikichelewa kurudi
sina wa kuniuliza
wala wa kunilaumu
ninaishi pekeyangu.

Ahsante xana
 
Back
Top Bottom