Nani kama Makonda?

Na aende akafute vumbi viatu vya riz tena ili amoombee apate ukuu wa Mkoa
 
kiukweli makonda yupo vizuri sana kiuongozi hata mkuu wa mkoa hagusi kabisa.
 
Kama ni kweli alimpiga ngwala Mzee Warioba basi DHAMBI huwa haifutiki mpaka uombe poo (msamaha) ndipo kila utendalo litakuwa na hekima pande zote.
Kwa anayofanya Kinondoni yanafuta ata makosa ya nyuma kama yapo. Wananchi wanatazama wanahesabu kila kitu, anayefanya kazi na anayepiga domo.
Vinginevo hata shetani hutoa mibaraka na mafanikio pia!!
 
Watu waovu, wabaya dhulmati, wanataka kumpora kiwanja walichomuuzia, kisa tuu hakubadili jina baada ya kukinunua, waliomuuzia, wamedanganya hati imepotea, wakaomba hati mpya, ikatolewa sasa wanajifanya hawakuwahi kuumuuzia hicho kiwanja na sasa wamempora!. Ukweli ni huu
Asante Sana kwa taarifa hii, naomba Mimi Mwanajeiefu mwenzenu, niwe mtu wa kwanza kuwajulisha kuwa hii vita ya kutaka kumdhalilisha mpakwa mafuta wa Beans, Paul Makonda, sasa ndio mwanzo WA mwisho wa hasidi huyu!. Karma ndio itamaliza kila kitu. Simaanishi Makonda ni malaika, bali, ni binaadamu kama binadamu wengine, hakuna mkamilifu, hivyo na yeye kuna makosa ametenda na tayari karma imeisha mshughulikia, hivyo kwa maonevu anayotendewa na hasidi huyu, ni Mungu, Baba ndiye atamlipia.
Kwanza mafanikio yake ni kutoka kwa Mungu.

Kisha, Wale mnaosubiri kwa hamu Makonda atumbuliwe, mtasubiri sana!. Ukiwa ni mpakwa mafuta, ni mpakwa mafuta!

Hivyo, hata kampeni batili ya kutaka kumpora kiwanja, ni upepo tuu na utapita.

Watu kumfanyia fitna na majungu, Makonda, hawakuanza leo

Yote haya yatapita, na Makonda atasimama.
P
 
Uliandika kwa kutumwa, kushikiwa akili au hiari yako mwenyewe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…