Nani kama Makonda?

Nani kama Makonda?

Tuusubiri uteuzi wa ma DC na Rc's ndio utajua JPM ni team Warioba. Makonda atarud lima vitunguu Ruaha Mbuyuni nakuambia
 
Ameonyesha uongozi kwa vitendo.. Ni mtendaji.

Ni mbunifu sana. Hasubiri maagizo ya wakubwa au kusukumwa muda wote anawaza ni namna gani anaibadilisha Kinondoni.

Sio mtu wa visingizio ni mtoa majawabu. Yale mambo ya bajeti haitoshi, mchakato unaendelea, tusubiri iki tusubirie kile. Kwake si vitu vya kuendekeza.

Kiukweli ana kutana na upinzani wa hali juu kutoka kwa wakawa na watu wa mlengo huo lakini hajawai kurudi nyuma.

Kinondoni kuna upungufu wa shule akaja na wazo la kujenga shule mpya 7 za kata kwa kudunduliza (kuna mpumbavu mmoja alikuja na hoja eti aonyeshwe mifuko ya cement ipo wapi eti anaiba cement)

Kinondoni kuna migogoro mingi ya ardhi, alikuja na system ya kusikiliza malalamiko yote ya ardhi na wengi sana wamenufaika na hii operation zimebaki kesi za kisheria ila amesuluisha mengi ( Sumaye ni shaidi kasaidiwa sana)

Amekuja na operation ya kucheki afya kwa wana kinondoni bure.

Amekuja na idea ya walimu kupanda mabasi bure ili kuwapunguzia mzigo wa maisha . Amekuja na hii idea sababu ndio kitu kilicho kwenye uwezo wake wa kimamlaka na kiushawishi.

Amekuja na idea ya kuondoa bar za vichochoroni kwenye majumba ya watu anashawishi kuwe na mtaa maalum wa kumbi za starehe. Hii itasaidia sana kuondoa kero zisizo za lazima kwa raia.

Na bado halali anawaza kila siku aifanyie nini Kinondoni.

Kiukweli kuna wanasiasa wazuri sana wa kupiga domo lakini vitendo ni sufuri. Wananchi sasa tunataka kuona watu wanaofanya kazi sio walalamikaji. Ata kama unafanya kidogo tunaappreciate kuliko kuhubiri unaleta pepo lakin ukipewa jimbo ni kulaumu serikali kuna mambo hayaitaji bajeti ya serikali ni uthubutu.

Mawaziri wa Magufuli mtazameni Makonda kwa makini wengi amewafunika japo mna rungu kubwa mnashindwa kulitumia . Tunataka vitendo vyenye tija.

Wabunge wa upinzani na madiwani msimchukulie Makonda kwa jicho hasi anazidi kuwapoteza. Fanyeni kazi tuone sio kulaumu tu.

Big up pia kwa Zitto naona nae ameanza siasa za utendaji. Kazi yake inaonekana Kigoma Ujijji.

Makonda tukimchukulia positive ana mengi ya kutufunza. Tunajua awezi kukosa mapungufu.
Umeongea Ukweli wote. Tunahitaji Vitendo na si maneno. Hongerah sana Mh. Makonda!
 
Hukuona jana Dr Shein kaenda kumjulia hali Maalim Sifu? Hivi unadhani mambo ni sawa? Siasa ndivyo zilivyo. Lakini ndugu yangu usijiaminishe kama upo katika moyo wa mtendwa. Aidha usisahau kuwa Mzee Warioba ni kiongozi yeye anasamehe je wafuasi wake unadhani tumesahau? Mshauri bwa mdogo aombe hadharani msamaha
Wewe ndio uombe msamaha hadhara kwa udanganyifu. Yaani wewe ndio uliyeumia kuliko Warioba mwenyewe?!?!? kwa uchungu gani. Mh. Warioba anajua Makonda ndio aliyemprotect na si kama mnavyotaka kutuamninisha. Hebu niambvie ninyi UKAWA huyu Makonda aliwafanyia nini? au kwa kuwa mnamuona jasiri mnamuogopa? Hebu nitajie UKAWA mmoja aliyefikia hata robo anayoyafanya Makonda hebu nieleze mmoja tu maana nikisema wawili ntakuonea just one!
 
Baada ya kujua kwamba kuna watu wanalipwa kuwasifia hawa wanasiasa, nikiona mtu anasifia inabidi nikae zangu kimya tu.
Ni lipi la uiongto alilosema? lipio? Ninyi ndio ingekuwa hamna vyombo vya habari mngetudanganya sana. Hebu site moja tu ambalo ni uongo!
 
Makonda yeye aendelee lakini subiri ukawa ipewe jiji halafu tuone mashindano kati ya ukawa na kada wa ccm makonda nani mshindi, lakini mashondano yao ni neema kwetu wananchi, tunamtaka maghufuli awaambie watendaji wake kuwa wanachelewesha maendeleo ya dar
Actually hao wanaodhani kupewa umeya ndiyo kuwaletea maendeleo watu ndio wanachemka. Kwa capacity zao wamefanya nini la maana zaidi ya kwenda mahakamani kupigana mabusu ya kijinga na mamigomo ya kijinga, Actually hao ndio wacheleweshaji wa maendeleo. Mh. Magu Futa kule mamanispaa upange safu yako ichape kazi. Tumechoka mabishoo wa kwenye maTV.
 
Ni lipi la uiongto alilosema? lipio? Ninyi ndio ingekuwa hamna vyombo vya habari mngetudanganya sana. Hebu site moja tu ambalo ni uongo!

Mkuu hakuna mahali niliposema kwamba kuna swala la uongo amelisema, nilichokisema ni kwamba imebidi niongeze umakini kwenye kuchuja habari na nikishindwa kuichuja nakaa kimya, na sababu ya yote ni juu ya memba mmoja humu JF kukiri kuwa amewahi kufanya kazi ya kuwatetea wanasiasa kwa malipo, na ilikuwa ni kikundi kikubwa tu.

Tena anaongezea kwamba alikuwa wakati mwingine anatetea hata vitu asivyovijua.
 
Mi nilivyosoma uzi huu niliona yoote ninayoyafahamu na ambayao yamefanika. Sasa kwa hao wanaolipwa sijui na wanafanya hivyo kwa faida ya nani? Watu husahau ukitetea upuuzi in one way inaweza kuaj kukuathiri mwyenyewe au uzao wake. Tuwaunge mkono kwa walio kwa ajili ya wengi na si wachache!
 
Mleta mada nataka kwanza unihakikishie 'usalama wa akili yako' ndio nilete hoja. Je hujawahi kufikishwa Muhimbili au Mirembe kwa matatizo ya 'kichwa' kuuma.
 
Nafikiri bado ujaijua vizuri picha ya Makonda now kwa wananchi. Nimeandika hii baada ya mjadala mzito hapa Kinondoni watu wanasema kawafunika mpaka mawaziri wa Magu. Wewe unalazimisha image unayotaka wewe. Kaa hivyo hivyo.
kama kijiwe kilichokuwa kinasema hayo ni cha mateja, wavuta bange au vijiwe vya wambea wenzio unatarajia nini. Jiongeze kdg acha kuja na umbea wa vijiweni.
 
Mi nilivyosoma uzi huu niliona yoote ninayoyafahamu na ambayao yamefanika. Sasa kwa hao wanaolipwa sijui na wanafanya hivyo kwa faida ya nani? Watu husahau ukitetea upuuzi in one way inaweza kuaj kukuathiri mwyenyewe au uzao wake. Tuwaunge mkono kwa walio kwa ajili ya wengi na si wachache!

Okay mkuu.
 
Actually hao wanaodhani kupewa umeya ndiyo kuwaletea maendeleo watu ndio wanachemka. Kwa capacity zao wamefanya nini la maana zaidi ya kwenda mahakamani kupigana mabusu ya kijinga na mamigomo ya kijinga, Actually hao ndio wacheleweshaji wa maendeleo. Mh. Magu Futa kule mamanispaa upange safu yako ichape kazi. Tumechoka mabishoo wa kwenye maTV.
Tayari wana umeya wa kinondoni na ilala hakuna walichofanya hadi sasa wapowapo tu.
 
Tayari wana umeya wa kinondoni na ilala hakuna walichofanya hadi sasa wapowapo tu.
Unaona eeeh. Watu wanapenda vyeo ila kutumia vyeo hivyo kuletea wananchi maendeleo ni sheeder!
 
Kwako mleta uzi mr. Gentleman et al. Kwanza tupunguzie sifa za kijinga humu na mtoto wa kiume hutakiwi kujipendekeza kwa mtu yeyote na kwa namna yoyote. Huo ubunifu ni ule wa kuwaweka jamaa wa upimaji lockup, wa kuwatukana wabunge, wa kumpiga Warioba, wa kuwaombea walimu lift, wa kuwadanganya watoto wa wenzake waunde vikundi wapewe kazi, wa kujenga mtaa wa walevi na madadapoa au wa kukaa studio za clouds tv? Kama umetumwa na kutumika ili kumjenga kupitia media ila hana sifa za kiuongozi labda abebwe kama alivyozoea. Mwambie aache kudandia hafla zisizomhusu kama ile ya firstlady wakati anawaaga staff wenzake shuleni. Ukuu si kuuza sura na kuwabomoa viongozi waliochaguliwa na wananchi bali kushirikiana kuwaletea wanaoongozwa nanyi maendeleo. Aache fitina kwa Kubenea, Mdee, Mnyika, madiwani na mameya. Tumeanza kumchoka siye wakazi wenye vision na mision.
 
Actually hao wanaodhani kupewa umeya ndiyo kuwaletea maendeleo watu ndio wanachemka. Kwa capacity zao wamefanya nini la maana zaidi ya kwenda mahakamani kupigana mabusu ya kijinga na mamigomo ya kijinga, Actually hao ndio wacheleweshaji wa maendeleo. Mh. Magu Futa kule mamanispaa upange safu yako ichape kazi. Tumechoka mabishoo wa kwenye maTV.

Labda nikuulize makonda kabla hajawa mkuu wa wilaya alifanya nini kwa ajili ya wilaya ya kinondoni
 
Labda unikumbushe alikuwa na cheo gani vile?!?!

Ndiyo maana nikasema ipeni ukawa cheo cha umeya uone hayo maendeleo, tatizo mnahukumu na kuhisia bila kuhakikisha kiuhalisia
 
Back
Top Bottom