Nani kafumaniwa

Wakati ananipigia simu kunitakia usiku mwena alionyesha wasiasi fulani hivi. Nina mazoea ya kwenda kwake ila huwa namtaarifu kuwa nakuja. sasa aliponipigia simu kujua kama naenda nikamwambia siendi. Nilibana pale club kusubili muda upite ili nim-suprise kwenda, kumbe ndo Mungu ananiongoza kuona niliyoyaona.
Kufanya kosa si kosa.. kosa ni kurudia kosa. msamehe!
 
Tatizo la vijana (wachangiaji wengi kwenye hii post), mnajaribu ku-over-act badala ya kufikiria kwa ukaribu zaidi...

Huyu in MCHUMBA (probably - mke mtarajiwa): Huyu binti siyo MKE wa Chimps: Huyu anayo maisha na matarajio yake kama alivyo Chimps: Huyu binti anao uhuru wa kwenda kokote atakako na kujumuika na marafiki zake bile Chimps kuwapo (hawana mkataba hawa wawili so far):::

Kama ilivyo kwa Chimps: akishampatia "lift" na kumfikisha kwake, na yeye Chimps anapitia Rose Garden, Corner Bar, au kwingineko nakujumuika na marafiki zake (bila kumhusisha huyu binti - ni uhakika na hilo):::

Kwahiyo "at this stage" hakuna ambaye "anammiliki" mwenzake - Kumlipia Kodi, Kumsomesha, e.t.c ni mambo unayotenda kwa sababu unamjali (siyo kumpenda - although inawezekana) kama rafiki yako wa karibu na siyo kama "MKE" wako... Wengi tuliochumbia muda mrefu - tulilipa sana KODI, Tulisomesha mpaka ndugu za wachumba, e.t.c - Na wengine hatukuweza kuwa nao kwa sababu mbalimbali - BUT - hatukujilaumu, kwa maana hatukuwa tunatenda hayo kama "UWEKEZAJI"...

Ushauri: Ukimkuta "MCHUMBA" wako mahali (kwenye starehe) bila ya kuwa mmetaarifiana kabla, the best thing you can do ni kusalimiana (possibly na kutamblishana kama anayo kampani yake) basi... Baada ya hapo kila mtu anachukua "time"... Kama "nafasi ipo" mnaweza kujumuika pamoja katika kustarehehe, otherwise, peaneni nafsi ili mpate kufahamiana vizuri!

umeoa?nakupenda ghafla
 
mim nakushauri utemane nae huyo dem kaka ,kwavile ameleta mapicha picha atakuletea magonjwa ,weanawakwe hawakuubwa kama adam ndo mana roho zao hazitabirik ,na uwezo wa wakupambanua mambo nn mdogo sana,
 
Tatizo la vijana (wachangiaji wengi kwenye hii post), mnajaribu ku-over-act badala ya kufikiria kwa ukaribu zaidi...

Huyu in MCHUMBA (probably - mke mtarajiwa): Huyu binti siyo MKE wa Chimps: Huyu anayo maisha na matarajio yake kama alivyo Chimps: Huyu binti anao uhuru wa kwenda kokote atakako na kujumuika na marafiki zake bile Chimps kuwapo (hawana mkataba hawa wawili so far):::

Kama ilivyo kwa Chimps: akishampatia "lift" na kumfikisha kwake, na yeye Chimps anapitia Rose Garden, Corner Bar, au kwingineko nakujumuika na marafiki zake (bila kumhusisha huyu binti - ni uhakika na hilo):::

Kwahiyo "at this stage" hakuna ambaye "anammiliki" mwenzake - Kumlipia Kodi, Kumsomesha, e.t.c ni mambo unayotenda kwa sababu unamjali (siyo kumpenda - although inawezekana) kama rafiki yako wa karibu na siyo kama "MKE" wako... Wengi tuliochumbia muda mrefu - tulilipa sana KODI, Tulisomesha mpaka ndugu za wachumba, e.t.c - Na wengine hatukuweza kuwa nao kwa sababu mbalimbali - BUT - hatukujilaumu, kwa maana hatukuwa tunatenda hayo kama "UWEKEZAJI"...

Ushauri: Ukimkuta "MCHUMBA" wako mahali (kwenye starehe) bila ya kuwa mmetaarifiana kabla, the best thing you can do ni kusalimiana (possibly na kutamblishana kama anayo kampani yake) basi... Baada ya hapo kila mtu anachukua "time"... Kama "nafasi ipo" mnaweza kujumuika pamoja katika kustarehehe, otherwise, peaneni nafsi ili mpate kufahamiana vizuri!

Wewe baba, usiwe kichwa nazi, hapa ishu sio kwenda club, ishu ni kwanini alidanganya???kama kwa wema na heri kwanini asimjulishe huyu mchumba wake???mahusiano kama yamefikia huko kwenye uchumba lazima umtoe mwenzako doubt, lazima umfanye mwenzako aamini kwamba hakufanya adverse selection.....kwakweli pakishakuwa na uongo na hila hapo hakuna penzi bali kuchezeana akili....
 
Kunguru wa Zanzibar hafugiki. Huyo ni kinguchiro achana naye ASAP na misaada yote kata mara moja.
 
kWANZA kabisa USHAKULA? Maana inabidi utafute kioo (any way hapa nachokoza tu!!)

Lakini nakua pole sana hata uliweza kuvumillia muda wote huo wa hiyo move (ndoto).......ndugu yangu dunia imebadilika sana haya mambo yalikuwa zamani kwamba unaweza kumtrust mtu as such lakini siku hizi watu wote wameoza, wamepotoka na hakuna aliye mwaminifu hata mmoja, ndio maana umeulizwa je ww wenyewe ni mwaminifu kwa kiasi gani? yamkini tunachangia kwa sababu ww una nguvu kubwa na umeshika mpini katika penzi hili (Patriarchy).tumia busara sana katika hili kwa sababu najua kiukweli bado unampenda sana. Kwenye sheria kuna natural justice..itumie hiyo japo wengine watasema hili ni suala a kijamii lakini kumbuka lina impact kotekote--(socio-economic aspect) ndiyo maana umekileta humu kushare kijamii lakini umeingiza masuala ya economic effect.

Katiaka sociolojia na baadhi ya mila wanasema kuna three faces of LOVE...the If love, the because LOVE and despite of LOVE, kWA KIFUPI WATALAMU (Wazaramu) wanasema mafiga matatu yaani anayekupenda kwa fedha, kwa mahaba (kukolezwa) na jinsi ulivyo, naona unachofanya hapa niupendo wa mshumaa.........(unamhudumia mwenzako wakati wewe mwenyewe unateketea) ni kweli kabisa kwamba kunguru hafugiki.....hasa katika tasnia ya malavidavi maana huwezi jua ameanzana nao lini na kwa vipi na much as hampo pamoja na ameshalamba asali (maana kama ni penzi la kuiba huwa linanoga sana) itakuwa ngumu kwako kufanya M and E, ITAWEZEANA kwa siku za mwanzo za makanyo lakini ngoma itarudi tu kwa uzoefu wangu

Any way
  1. Mweleze ukweli wote japo picha ameshaiona (kwa kuthibitisha ulivyoumia hata huu uzi unaweza kumkopia wote akajisomee...huwa ina some outcomes...
  2. Nimeona kama kitendo cha kuishiwa nguvu na kukufuata ni some element ya respect, maana hapo alikuwa anawajulisha kwamba NINA WANGU , kifupi alichagua BEGA LAKE....na huenda alishawajulisha (early warning)
  3. Huwezi jua ni kwa kiwango gani alishazama kwenye hilo penzi....pengine ilikua nwezi nchanga maana huna precedent ya huko nyuma japo machale yalikucheza kwa siku hiyo.........ingawa kizuoni ni dalili fulani tayari ilishaanza kukuingia ukifika hatua hiyo
  4. any way MILUZI MINGI HUMPOTEZA MBWA .....TAFAKARI, CHUKUA HATUA
 
Mkuu, mbona kuna mabinti hapa JF wanatafuta waume wa kuwaoa, si uangalie mmojawapo aliye siriasi mkipendana umwoe? Huyo amenyea kambi, achana nae. Anakuchuna tu huyo hayuko siriasi.
 
pole sana kaka. mi naamin kwanza dem huyo hakufai kabisa hapaswi kuitwa mke wa mtu, kitu kimoja kibaya alichokifanya na mimi kimeniudhi ni kukwambia kuwa amellala na kukutakia usiku mwema then mnakutana Club. Kilichopo we kashakuona mambo poa unampenda, unadrive na unamjali hapo hao wengine ni wa kumpa matakwa ya mwili wake kama sex, make kama hata mnafanya hivo yeye hatosheki kabisa make unakuwa unamhurumia kwa kuwa unawaza siku moja atakuwa mke wako. lakin washikaj wakimgeuza hapo ndo anaona kuwa kafika haswaaaaaaaaa. pole sana kaka kwa hili naomba uachane naye kabisa hafai labda ukiendelea naye awe wa kuzugia na kutumia si wa kuoa.
 
sasa najiuliza maswali yasiyo na majibu
1. Kuna haja ya kuendelea naye
2. ananiambia wale ni kaka zake, je kaka kwa staili ile, na alitegemea kulala wapi maana nyumba anayoishi geti linafungwa saa nne kamili.
3. nilikuwa namlipia masomo ya kuendeleza shule yake, je niendelee au ndo mwisho??
4. nyumba anayoishi nailipia mimi maana mimi kwangu nakaa na wadogo zangu na hatujaanza kuishi pamoja, je nitaendelea kulipa


Naomba ushauri,

Chimps

Kijana wangu, hayo maswali yana majibu. Jibu lake ni moja tu. MUACHE. Kamata ufunguo wako, habari ya shule atalipiwa na 'kaka zake'...nadhani umenisoma hapo.
 
Wewe baba, usiwe kichwa nazi, hapa ishu sio kwenda club, ishu ni kwanini alidanganya???kama kwa wema na heri kwanini asimjulishe huyu mchumba wake???mahusiano kama yamefikia huko kwenye uchumba lazima umtoe mwenzako doubt, lazima umfanye mwenzako aamini kwamba hakufanya adverse selection.....kwakweli pakishakuwa na uongo na hila hapo hakuna penzi bali kuchezeana akili....

:shock::A S-coffee:
 
ngastuka machale kundesa n bora ujue unalea kunguru ww mwenyew unamatatizo huwez kufikia hatua ya kumsomesha n kumlipia m2 mjengu pasipo hata kuwa n abc ya familia yako!matokeo yk ndio hayo ss mara bro mara nn tna usikute ww unat...... wenzio wanakula mtandao kwa gharama nafuu!fukuzia mbali gahaba hlo
 
ni saa kumi na mbili jioni natoka kazini, nampita demu wangu ili nimpeleke kwake na mimi nirudi zangu kwangu.
Mara ananiambia nimpitishe mahala kuna club fulani karibu na kwake akachukue mzigo wake fulani kwa rafiki yake. Nafanya hivyo na tulipofika nje ya hiyo club nikapokea simu inayonilazimu nirudi ofisini. Hivyo tukakubaliane achukue mzigo na aende nyumbani maana mimi narudi ofisini. Nimekaa ofisini mpaka saa mbili usiku, akanipigia simu kuwa ameshalala na akanitakia usiku mwema. Nami nikamweleza kwamba ndo naelekea kwangu. Ila machale yakanicheza ikabidi nipite kwenye ile club, nika-paki gari mbali kidogo, nikaingia ndani ya hiyo club nikaagiza maji na kijichimbia kenye kona fulani ina kagiza.
Mtumeeeeee!!!, baada ya dakika kumi hivi sikuamini macho yangu kumuona demu huyohuyo anaingia akiwa ametinga pedo laini, mapaja yote nje. Akaenda kukaa meza moja walikaa mabrother men na baadhi ya mademu. Kilicho niuma ni brother men mmoja kumpokea kwa busu, wakakaa then demu akawaamemkumbatia huyo brother. Kweli roho iliuma kinoma. Nikawaacha waendelee na mishemishe zao, mara wanyanyuke wasindikizane nje, waende kwenye gari kutafuta koti na mengine.
Ulipopigwa mziki wa hakunaga, meza yao wote alinyanyuka na kuanza kusakata rumba. At around saa nne na robo wakawa wameshakolea kilevi. Sasa wakati anasakata rumba gafla demu kaniona nikiwa kona nimekaa nami namuangalia. Nguvu ya kucheza iliisha, akaangalia chini kwa aibu, akaja kunifuata. Kuja tu nikamzuia asinifuate aendelee na starehe maana mimi sijamuita. Then mimi nikaondoka zangu.
Sasa najiuliza maswali yasiyo na majibu
1. Kuna haja ya kuendelea naye
2. Ananiambia wale ni kaka zake, je kaka kwa staili ile, na alitegemea kulala wapi maana nyumba anayoishi geti linafungwa saa nne kamili.
3. Nilikuwa namlipia masomo ya kuendeleza shule yake, je niendelee au ndo mwisho??
4. Nyumba anayoishi nailipia mimi maana mimi kwangu nakaa na wadogo zangu na hatujaanza kuishi pamoja, je nitaendelea kulipa


naomba ushauri,

chimps


piga chini. Hajatulia huyo.
 
utasamehe mara ngapi? temana nae wanawake wapo kibao siku hizi na walio na sifa zote.

1. wakuoa
2. wakutumia
3. wakuzugia
Mkuu hawatofautiani sana ujue, na sisi ambao tunawadanganya hatutofautiani sana,wengi tuko hivyo na wao wengi wako hivyo hata ukienda kijijini ukamleta mjini, mjini shule, la maana ni maisha yaendelee mbele, huyu akisamsamehe itakuwa safi maana kesha jifunza hatomdanganya tena.
 
Good advice umetoa sista.... Follow ur heart kwanza then mengine yatafuata.

Mimi ushauri wa kumwambia mtu asikilize moyo wake unamwambiaje,kisa tu ndiyo mhusika sioni kama unamsaidia muomba ushauri. Kwanza nakupa pole.Kusameheka kunafaa sana atakapokiri kosa lake,na akalijutia... Akijiteteatetea na ukaendelea naye,hapo kuna mawili..kutulia na kuogopa kitumbua kuingia mchanga,ama ataendelea na tabia yake hiyo ila kwa tahadhari,na ikitokea ukamfuma tena atajua namna ya kukubembeleza usimwache..
 
msamehe then achana nae na gharama unazomlipia sitiza kuanzia sasa mana inaonekana hakujali tena hana mapenzi ya kweli kwako kwanini akufanyie yote hayo baada ya kumvumania bila shaka kama umeachana nae tafuta mwingine mwenye mapenzi ya kweli
 
kama wale ni kaka zake kwanin alikudanganya kuwa amelala, kwanini asingesema ukweli kwamba anaenda club na kaka zake? ina maana wew kaka zake uwajui hata kwa kuonyeshwa picha tu kama hawa ni kaka zangu? kuna mengi ya siri anayafanya bila wew kujua ila mungu amekusaidia umeweza kujua hilo moja.
ushauri wangu, ningekuwa mim ningeachana naye nianze upya kwa maombi kwa mungu anipatie aliye wangu mana kulazimisha eti atabadilika ukimweka ndani ndo utajuta zaidi. anza upya kaka mungu yupo pamoja nawe. Amen
 
Back
Top Bottom