Nani kafufua ukabila Nchini?

Nani kafufua ukabila Nchini?

Askofu Gwajima na Usukuma
Askofu Shoo na Uchagga

Tarehe 3.3.2020 Viongozi wa dini wawili hapa nchini wamekata mawimbi ya anga kwa jambo linalofanana.

Askofu Gwajima wa Kanisa la ufufuo na uzima lililopo Dar es salaam, alihojiwa na polisi kwa kusambaza vipeperushi vyenye lugha ya kisukuma akiwahamasisha wajitambue na kusaidiana, alitumia picha ya Mhe.Rais ili kuwahamasisha waungane na kuunda chombo madhubuti.

Huko Moshi Mkoani Kilimanjaro tarehe 3.3.2020 Askofu Shoo wa KKKT alikutana na wachungaji wake wapatao 200 na kuwaambia serikali ya awamu ya tano na baadhi ya maaskofu wanawaonea wivu wachagga .

Akasema wachagga wamefanikiwa sana kusababisha waonewe wivu au kuonewa na akawataka waungane na kusaidiana na kulinda Dayosisi yao, bahati mbaya Askofu Shoo hajahojiwa na polisi kama Gwajima.

Kuwabagua wachagga au wasukuma ni kosa kubwa, lakini na wao kujibagua na kujiona bora kuliko makabila mengine ni kosa kubwa zaidi.

Watanzania tujiulize nani kafufua ukabila tena nchini mwetu?
Mwananchi namba moja ndio tatizo
 
Si ungeenda moja kwa moja tu mkuu kwenye point kuliko kuzunguka we ungesema tu ukweli maana unajua kanda ya ziwa sasa ndio iko on peak we ungesema tu
 
Ukabila na ukanda utarudi kwa sababu hakuna mtu wa kukemea ukabila na ukanda!
 
kwenye sekta ya sheria Ukabila upo tokea enzi na enzi. Fuatilia law firms, wamiliki na wafanyakazi ni kabila moja, hata asilimia kubwa ya wateja ni toka kabila la mmiliki wa hiyo law firm.
Hapo dominant tribes Ni Chagga and Haya.

You're most likely meaning Chagga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom