Nani kaenda Geneva, Uswisi na Ndege ya Rais?

Nani kaenda Geneva, Uswisi na Ndege ya Rais?

Joined
Mar 9, 2015
Posts
65
Reaction score
85
Asalaaam Aleykum Warrahmatullahi Wabarakattuhu.

Ndugu Wa Tanzania.

Ndege ya Rais Ndugu John Pombe Magufuli imetinga Geneva Uswisi masaa 24 yaliyopita.

Commander in Chief (NDUGU MAGUFULI) kama mnavyojua kapiga marufuku safari za nje . Na kwa kuonyesha kuwa yuko serious, yeye mwenyewe kaamua kwenda Dodoma kwa barabara ili kuokoa mapesaza walipa kodi ili walau vipatikane vitanda vya wagonjwa na dawa hospitalini
Gulfstream_G550_Tanzania_-_Government_5H-ONE,_ZRH_Zurich_(Zurich-Kloten),_Switzerland_PP1360524007.jpg

Sasa swali, hii ndege ya Rais inafanya nini Geneva ? Hapa sizungumziii ndege ile ya serikali ambayo nayo hawa inakodishwa la shashi, hapa nazungumzia Presidential Jet aina ya GULF STREAM G550 ambayo ilinunuliwa kwa zaidi ya DOLA MILIONI 100 ( kwani ilibidi jamaa wa Gulf stream waifanyie upgrade ili ifike kiwango cha Rais) imempeleka nani huko maana Rais wa Zanzibar ndugu Shein yuko hapa Tanzania. Na kama kulikuwa na ulazima wa kwenda huko Geneva imeshindikana vipi kwenda na ndege ya shirika la ndege la Uswisi? Ina maana kuna Commander in Chief mwingine zaidi ya Ndugu JOHN POMBE MAGUFULI au tuelewe vipi?

Mkitaka ushahidi msipate yaabu

Ingia kwenye mtandao huu:

www.https://www.flightradar24.com

kisha kwenye kitufe cha ku search wewe andika 5H-ONE
attachment.php


na kwa mtakaopiga kelele jueni kuwa mtandao huo unaweza kuona mpaka ndege ya Obama ilipo na inafanya nini. Hivyo hakuna siri na hakuna cha kuficha


Kama agizo la Ndugu Magufuli limekaidiwa kiasi hiki, tunaomba tujuzwe ni nani huyo ambaye anakaidi agizo la Rais wetu ambaye hata wiki 3 hajamaliza Wala Nchi washaanza kumdharau na kumkaidi.



Wabillahi Taufiq
 

Attachments

  • MKU KAKAIDI AGIZO LA MAGUFULI.PNG
    MKU KAKAIDI AGIZO LA MAGUFULI.PNG
    6.1 KB · Views: 31,905
Hata wewe unaweza kuikodi Ndege ya Rais kupitia Wakala wa ndege za serikali Tanzania.

Kama ukitaka kufahamu nani ameikodi, kawaulize wakala wa ndege za serikali.

Nadhani pia Wakala wa ndege za serikali Tanzania wanatakiwa wazuie ndege ya Rais kuwa tracked kwenye mitandao.

Ndege kama ya Rais Obama na zingine nyingi za watu binafsi huwezi kuziona zikiwa tracked kwenye mitandao kama frightradar and frightstats.
 
Kwa ndege ya rais inakodishwa na kufanya kazi kama za teksi?????
Yes, ndege ya Rais unaweza kuikodi.

Kwani tatizo ni nini?

Soma hii habari ambayo iko hapa Jamiiforums.
Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA), umesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilimlipia Sh. milioni 8.4 mgombea wake wa urais, Dk. John Magufuli, kwa ajili ya kutumia ndege ya Serikali kwenda mkoani Mwanza kwenye ziara maalum ya kujitambulisha.​

Akizungumza na NIPASHE ofisi kwake, Ofisa Mtendaji Mkuu wa TGFA, Kapteni Keenan Mhaiki, alisema chama hicho kilifuata taratibu zote zinazohusiana na kukodi ndege hiyo na kusisitiza kwamba mtu au chama chochote kitakachohitaji huduma ya usafiri kinapata ndege hizo, lakini inategemea ratiba za viongozi wa serikali ambao huzitumia kwa safari mbalimbali.

"Hakuna mtu aliyenyimwa ndege ukiona hajapatiwa kunatokana na ratiba kuwa ngumu mara nyingine hutoa huduma ya usafiri timu za mpira zinaposafiri," alisema Kapteni Mhaiki.

Aidha, alisema ndege hiyo hukodishwa bila upendeleo huku akisisitiza kwamba hakuna mtu au chama kilichowahi kukodi kikanyimwa.

Alisema TGFA itaendelea kufanya jitihada za kutoa elimu ya matumizi ya ndege za serikali kwa jamii ili kuondoa dhana potofu iliyojengeka kuhusu suala hilo.

Julai 19, mwaka huu Dk. Magufuli alitumia Ndege ya serikali aina ya Fokker F28 kwenda Mwanza kujitambulisha kwa wanachama.

CHANZO: NIPASHE(
21 July 2015)
NDEGE-620x309.jpg
 
Ni Kikwete kaenda kwenye mkutano huko. Nasikia yeye ni mwenyeketi wa huo mkutano. Sijuwi kwanini hakutumia usafiri wa ndege za kawaida ambao ni bei rahisi zaidi. Mkwere noma, kaacha hazina haina kitu na wala hajali anazidi kutumbua tu, Mbayaaa.
 
Ni Kikwete kaenda kwenye mkutano huko. Nasikia yeye ni mwenyeketi wa huo mkutano. Sijuwi kwanini hakutumia usafiri wa ndege za kawaida ambao ni bei rahisi zaidi. Mkwere noma, kaacha hazina haina kitu na wala hajali anazidi kutumbua tu, Mbayaaa.
kama hili ni kweli basi kweli tutaisoma namba. wasituambie amekodi. hivi magari ya serikali nayo kuna wakala wa kukodisha?
 
Acha kupotosha watu..unajaribu kuaminisha watu kuwa hakuna anayeruhusiwa kusafiri nje ya nchi?? ukweli ni kwamba, mtumishu wa serikali unaweza kusafiri baada ya kupata approval ya ofisi ya rais au Vice President...
 
Hii mada kidogo imenichanganya.
Kwani hapa tunajadili ndege ya Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania kuonekana Uswis?
Au.......
Ndege ya Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania imempelekea nani Uswis wakati Rais wa Tz hajasafiri nje ya nchi?
Au.....
Ndege ya Rais wa Tz kwanini imekwenda nje ya nchi ilhali Rais wa Tz amepiga marufuku safari za nje?
 
Hata wewe unaweza kuikodi Ndege ya Rais kupitia Wakala wa ndege za serikali Tanzania.

Kama ukitaka kufahamu nani ameikodi, kawaulize wakala wa ndege za serikali.

Nadhani pia Wakala wa ndege za serikali Tanzania wanatakiwa wazuie ndege ya Rais kuwa tracked kwenye mitandao.

Ndege kama ya Rais Obama na zingine nyingi za watu binafsi huwezi kuziona zikiwa tracked kwenye mitandao kama frightradar and frightstats.

Kuikodisha ndege ya raisi TZ kama ni kweli hilo ni jambo jema kwani itapunguza gharama za kuitunza kama itakodishwa kwa taratibu nejma. Lakini pia ni vema tracking yake isifichwe wakati inapotumiwa na watu wengine isipokuwa tu ikitumiwa na Raisi. Hiyo ndio hali ya uwazi tunayoihitaji Tanzania.

Pia ingekuwa vema kwa magari ya Serikali yakatumika tu kwa safari za kiserikali na yasiruhusiwe kubeba watu wasio watumishi wa umma bila kibali maalumu.

Viongozi wote waende kazini na magari yao na wakifika ofisini ndio wakiwa na kazi za kiofisi ndio watumie magari ya serikali.

Asiwepo kiongozi yeyote, isipokkuwa Raisi, makamu na waziri mkuu ambaye anatumia gari la serikali kwa shughuli za kifamilia. Tukiweza haya, tutaweza kupunguza gharama serikalini na pia kurefusha uhai wa vyombo/ magari ya serikali.
 
Wewe the mole hunter unajaza server yetu bila sababu. Haya basi labda imepelekwa service.
 
Labda Tz tu huwezi kukodi ndege ya rais. Hope kuna ndege za serikali nyingine lakini ndege ya Rais ni ikulu, ni ofisi ya Rais lkn kama bongo kila mtu anaweza kukodi basi hayo ni maajabu mengine.
Na kama fast jet kapiga nayo misele, hakuna cha kushangaza tabia ya mtu haibadiliki ati 🙂
 
Back
Top Bottom