Nani bora, JK au Mkapa aliyekoroma tukakaa kimya?

akilimtindi

JF-Expert Member
Jun 30, 2008
421
83
Nani bora kati ya JK au Mkapa aliyekoroma tukanyamaza ingawa "underground" alifanya ubaradhuli?

Nauliza hivi kwasababu JK kama ni rubani basi keshatoka nje ya ndege na sisi hatuna habari. Kama yupo bado kwenye ndege yetu basi tusijiaminishe na safari yetu maana rubani wetu anashinda chooni tena hayuko peke yake, ana limwanamke lake la kiarabu au vinginevyo wameamua kusahau kwamba kuna haja ya kucheki ndege inakwenda wapi au imefikia wapi.

Kama ni referee basi hapa naona amekimbilia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo na sasa amekwama huko kwa kisingizio cha kusimamia wageni wavae vizuri. Nadhani huko nako hakosi jimama yuko nalo maana naamini huyu referee ni mtu wa vimwana. Huku uwanjani mpira unajicheza wenyewe na matokeo ni kwamba kwanza wenye nguvu ndio wanaopiga mpira na wanapiga kuelekea wanakotaka wao, kisha wakiona kuna wasiyemtaka anataka kupiga mpira wanauchukua wanashika kwa mikono. Baya zaidi hata ambao hawakuwepo kwenye mechi sasa wameingia uwanjani nao wanataka kupiga mpira na wanapewa wanapiga wanakotaka, tena ikibidi wanapiga hadi kwa watazamaji ambao wanaushika kwa muda kisha wanawapa tena wale wababe ambao wanaamua wapige au la tena wapige kuelekea upande gani...???

Je, mechi hii itakwisha? Ni nani atashinda? Je, tuwaache wenye mabavu wapige mpira kwenda wanakotaka? tuwanyang'anye kwa nguvu au tubadilishe referee maana hata hivyo hayupo tena uwanjani?

Mifano halisi ya mpira kupigwa kwa watazamaji na kuushika kwa muda ni kama ripoti ya madini kupewa Sinclair mtu asimamaye kama mtazamaji

Mifano halisi ya mijibwa kushika mpira kwa mikono ni kama Mafisadi ku-hold kesi zao zisiende mahakamani

Mifano halisi ya rubani kushinda chooni au referee kushinda kwenye vyumba vya kubadilishia nguo ni kama JK kushinda nje ya nchi halafu akirudi anatueleza habari za huko maana hajui hapa ndani mambo yalikuwaje.

Mwisho nilimsikia Pinda akichemsha tena bungeni na kushusha hadhi yake kwamba JK hakuweza kuhutubia wananchi kwa kipindi ambacho hana hakika nacho, ("miezi miwili hivi..., sidhani kama ni mitatu"- Pinda) kwa kuwa alikuwa busy nje ya nchi. (JK alipohutubia alidhihirisha hajatuhubiria pumba zake kwa miezi mitatu na hakufanya hivyo kwasababu wananchi walipenda live performance yake, siyo recorded aliyokuwa akiacha zamani ikarushwa hata kama hayupo - contradiction with Pinda, his very PM). Je, haiwezekani mambo mengine mengi na ya msingi kuhusu nchi yetu kukwama kwa kuwa prezidaa yuko bize nje ya nchi most of the time?

Je, tutafika kwa style hii ya rubani kushinda chooni? Ningeshukuru Mungu walaa kama ndege yetu ingefika bila kukwaa mlima maana huo ndio wasiwasi wangu mkubwa kwa sasa...!!!
 
Sio Mimi, Wanafunzi wanasema WAZI ndani ya JIJI lilojaa mafisadi hao hao, na naamini waliyaona haya mabango na kuyasoma kinagaubaga...!

Baadhi ya mabango ya wanafunzi walioandamana yalisomeka: "Wafilisiwe Chenge, Mkapa, Karamagi na Yona tuletewe mabasi ya shule, J.K utawala umekushinda, Tulipe Sh100 kwa lipi uliloboresha?".

Mabango mengine yalisomeka: "Tumegundua Kandoro na askari wake pia mafisadi, Heri Makamba kuliko Kandoro, Bora Mkapa kuliko Jakaya na imekuaje hatuna kazi na tulipe Sh100 huku polisi wanapanda bure"

Asanteni sana wanafunzi kwa kuamka walau majibwa yashtuke...!
 
Hakuna aliye bora, wote ni mafisadi tu. Mkapa alitumia awamu zake mbili kutuibia ili ajitajirishe na yeye na familia yake. Kikwete hii awamu yake anawakingia kifua mafisadi kwa kuwaogopa maana mara atakapoamua kuwashughulikia nao wataibuka na stories jinsi alivyofanya ufisadi wa hali ya juu na hatimaye kuibuka kama mgombea wa CCM. Wote wanaiangamiza Tanzania.
 
Ingawa wote hawafai lakini JK hafai kabisa ,MKAPA alianza vizuri na akajenga uchumi then baadae akaiba na kuondoka lakini huyu jamaa ambae aliitwa chaguo la MUNGU hamna alilofanya tangu kaingia ikulu ye kazi yake kwenda ulaya kila siku kununua nguo sijui 2010 atawadanganya vipi watanzania
 
Hawa Watoto vipi? kila kata ina sekondari, wanapanda basi kwenda wapi?

Kutoka azikiwe (dar 0km) hadi gongo la mboto ni 20km yaani 45min kwa mguu. Nihalali kweli mwanafunzi kupanda gari kutoka mnazi mmoja hadi forodhani sec. mpirani wanakimbia 90min kutembea 15min hawataki!

Toyota Coaster ni us$35,000 japani hapo haujaweka freight ushuru registration road licence, zingatia itakuwa imetembea 400,000km halafu zinapigwa rivasi zinabaki 89,000km. Brand new ni 200m halafu uanze kutoza nauli 100/=

Bei ya diesel ni 2000/=, tairi @350,000/= (firestone), nadhani nauli iwe moja tu hakuna cha mtoto wanaoshindwa watembee kwa mguu. niliwahi toroka jkt chita kwa mguu hadi moro then nikapanda basi kuja dar, nilikuwa naenda kujaza form za udsm. Kama wanania ya kusoma kweli watatembea watasoma na kufaulu.
 
duh!, si mchezo
basi kama ni hivyo, basi hata raia wasio wanafunzi wasilalamike, maana hata wao wanaweza kutembea kwa mguu na kadhia ya nauli kuwa juu ikesha
 
Ingawa wote hawafai lakini JK hafai kabisa ,MKAPA alianza vizuri na akajenga uchumi then baadae akaiba na kuondoka lakini huyu jamaa ambae aliitwa chaguo la MUNGU hamna alilofanya tangu kaingia ikulu ye kazi yake kwenda ulaya kila siku kununua nguo sijui 2010 atawadanganya vipi watanzania

Fisadi Mkapa aliweza kuongeza makusanyo ya kodi ya mapato kwa kiasi kikubwa tu, lakini ongezeko hilo halikuwasaidia lolote Watanzania. Pia uchumi unasemekana ulikua kutokana na number za WB na IMF lakini Watanzania walio wengi waliona ongezeko la hali ngumu ya maisha.
 
Hawa Watoto vipi? kila kata ina sekondari, wanapanda basi kwenda wapi?

Kutoka azikiwe (dar 0km) hadi gongo la mboto ni 20km yaani 45min kwa mguu. Nihalali kweli mwanafunzi kupanda gari kutoka mnazi mmoja hadi forodhani sec. mpirani wanakimbia 90min kutembea 15min hawataki!

Eddy,

Naomba majina ya waliotembea kilometa 20 kwa dakika 45 ili tuwapeleke Beijing tupate medali za zote za ile marathoni ya kutembea!
 
Hawa Watoto vipi? kila kata ina sekondari, wanapanda basi kwenda wapi?

Kutoka azikiwe (dar 0km) hadi gongo la mboto ni 20km yaani 45min kwa mguu. Nihalali kweli mwanafunzi kupanda gari kutoka mnazi mmoja hadi forodhani sec. mpirani wanakimbia 90min kutembea 15min hawataki!

Toyota Coaster ni us$35,000 japani hapo haujaweka freight ushuru registration road licence, zingatia itakuwa imetembea 400,000km halafu zinapigwa rivasi zinabaki 89,000km. Brand new ni 200m halafu uanze kutoza nauli 100/=

Bei ya diesel ni 2000/=, tairi @350,000/= (firestone), nadhani nauli iwe moja tu hakuna cha mtoto wanaoshindwa watembee kwa mguu. niliwahi toroka jkt chita kwa mguu hadi moro then nikapanda basi kuja dar, nilikuwa naenda kujaza form za udsm. Kama wanania ya kusoma kweli watatembea watasoma na kufaulu.
Hapa ndipo serikali inayojali wananchi wake tunapoipimia. Si hizi bra bra za maisha bora kwa kila mdanganyika.
Serikali bora kwa wananchi wake haijivui hata siku moja katika huduma za jamii.
Inaweza kujivua biashara, sawa. Lakini kuhudumia wananchi wake, haiwezi kujivua na kuwapa wafanyabiashara au wawekezaji.
Yapo majukumu ya wawekezaji katika kukuza uchumi wa nchi na lipo jukumu la serikali kuhudumia wananchi wake.
na hili la watoto kwenda shule na kurudi, kusoma shuleni kwa kupata elimu bora si bora elimu ni la serikali. Amini usiamini wewe na wengine wenye mawazo kama yako mjue ni la serikali. Ndio sababu tunaiweka madarakani. Haiwezi iondoke tuwape wanaoweza. Hatutaki bra bra.
 
Hawa Watoto vipi? kila kata ina sekondari, wanapanda basi kwenda wapi?

Kutoka azikiwe (dar 0km) hadi gongo la mboto ni 20km yaani 45min kwa mguu. Nihalali kweli mwanafunzi kupanda gari kutoka mnazi mmoja hadi forodhani sec. mpirani wanakimbia 90min kutembea 15min hawataki!

Toyota Coaster ni us$35,000 japani hapo haujaweka freight ushuru registration road licence, zingatia itakuwa imetembea 400,000km halafu zinapigwa rivasi zinabaki 89,000km. Brand new ni 200m halafu uanze kutoza nauli 100/=

Bei ya diesel ni 2000/=, tairi @350,000/= (firestone), nadhani nauli iwe moja tu hakuna cha mtoto wanaoshindwa watembee kwa mguu. niliwahi toroka jkt chita kwa mguu hadi moro then nikapanda basi kuja dar, nilikuwa naenda kujaza form za udsm. Kama wanania ya kusoma kweli watatembea watasoma na kufaulu.
Hapa ndipo serikali inayojali wananchi wake tunapoipimia. Si hizi bra bra za maisha bora kwa kila mdanganyika.
Serikali bora kwa wananchi wake haijivui hata siku moja katika huduma za jamii.
Inaweza kujivua biashara, sawa. Lakini kuhudumia wananchi wake, haiwezi kujivua na kuwapa wafanyabiashara au wawekezaji.
Yapo majukumu ya wawekezaji katika kukuza uchumi wa nchi na lipo jukumu la serikali kuhudumia wananchi wake.
Na hili la watoto kwenda shule na kurudi, kusoma shuleni kwa kupata elimu bora si bora elimu ni la serikali. Amini usiamini wewe na wengine wenye mawazo kama yako mjue ni la serikali. Ndio sababu tunaiweka madarakani. Haiwezi iondoke tuwape wanaoweza. Hatutaki bra bra.
Mbona hujaweka bei ya shangingi zinazozunguka tu ovyo kubeba vimwana wa hawa mafisadi? Ikifika suala la watoto wetu ndiyo bei zinajulikana zilivyo juu na kwenye mishangingi yao hapo mnakuwa mabubu?
 
Ukiondoa mambo ya ufisadi, MKAPA ni bora mara 200 kulinganisha na KIKWETE. Ulichukkua nchi ikwa na uchumi liokuwa umedidia toka kwa mazee wa unga MWINYI. Mkapa aliweka misingi imara kiuchumi kama barabara, inflation ilikuwa under control etc.

Watoto washule lazima walipe nauli mpya, wazazi wao wanajukumu ya ukulipa siyo wao, kama wazazi hawezi basi wawapeleke shule za jirani watembee kwa miguu. Kwanini wasiandame kwa bei ya mkate, mchele, mafuta ya diesel kuwa juu
 
Hawa Watoto vipi? kila kata ina sekondari, wanapanda basi kwenda wapi?

Kutoka azikiwe (dar 0km) hadi gongo la mboto ni 20km yaani 45min kwa mguu. Nihalali kweli mwanafunzi kupanda gari kutoka mnazi mmoja hadi forodhani sec. mpirani wanakimbia 90min kutembea 15min hawataki!

Toyota Coaster ni us$35,000 japani hapo haujaweka freight ushuru registration road licence, zingatia itakuwa imetembea 400,000km halafu zinapigwa rivasi zinabaki 89,000km. Brand new ni 200m halafu uanze kutoza nauli 100/=

Bei ya diesel ni 2000/=, tairi @350,000/= (firestone), nadhani nauli iwe moja tu hakuna cha mtoto wanaoshindwa watembee kwa mguu. niliwahi toroka jkt chita kwa mguu hadi moro then nikapanda basi kuja dar, nilikuwa naenda kujaza form za udsm. Kama wanania ya kusoma kweli watatembea watasoma na kufaulu.
Mkuu hapa tatizo umeshindwa kuangalia mambo kwa upana wake, hatukatai kwamba vitu vimepanda bei. Na wanafunzi wamekuwa na akili hawajakugomea wewe maana najua wewe kama huna daladala basi rafiki yako analo.

Wanafunzi wanajua kabisa aliyezembea mambo yakaharibika hapa ni serikali, maswala ya vitu kupanda na kushuka bei ni maswala ambayo serikali inatakiwa iyajue kabla ya madhara na ndio maana kuna wataalamu wa uchumi kwa ajili ya economic forecasts. Kazi yao ni kujua mwaka kesho hakuna chakula kwahiyo serikali itenge fungu la chakula, kuna uwezekano wa vita middle east kwahiyo mafuta yatapanda na serikali inatakiwa kufanya jambo kukabiliana na madhara, mabenki ya kigeni yanahujumu uchumi kwahiyo yabanwe kwa njia gani ili uchumi wetu usitetereke na mengine mengi kama hayo.

Sasa hapa inaonekana hao wahusika wako bize kupanga namna ya kula faranga ambazo hata ziliwekwa hazina kama insurance incase of emergency, sasa unadhani watapata wapi muda wa kufikiria kwamba jiji linakua, huduma zinahitajika zaidi tena za kisasa zaidi? watapata wapi muda wa kufikiria kwamba shule na wanafunzi wanaongezeka kila kukicha? hawana muda. Pinda alisema JK yuko bize hasa baada ya kupewa jukumu la AU, maana yake mkiona mambo mengine yanakwama mjue JK yuko bize na AU, Darfur, Zimbabwe etc...
 
Huwezi kumfananisha Brother Ben na huyu Mkwere,Brother Ben alifanya alichofanya best ingawa vipo alivyokosea.Ben Hakukuta hadhina kitu kama huyu Mkwere alivyoachiwa na kukiri mwenyewe,Madeni ya walimu na wafanyakazi wengine serikalini Ben alisawazisha,alilipa madeni ya Nje na mengine tukasamewewa kwa kuonyesha kweli jamaa anakusanya kodi na hata waliokuwa na moyo wa kusaidia tena wakatoa misaada.Tofauti na sasa hawataki hata kusaidia bajeti kutokana ya kuwa wanajua in and out kuhusu serikali ya sasa.Usimamizi wa barabara nyingi umefanyika kipindi chake.Kwa kifupi kimataifa jamaa aliheshimika pia.

Ila huyu mkwere JK ni mweupe kabisa,hayuko competent enough ,aliowaweka nao ndio vile na kaingia madarakani kwa fitna na waliomsaidia kifedha ndio wao wameiweka inchi mikononi.
Alichojaribu kufanya ni Kumuumbua Ben kijipembeni ili yeye aonekane safi lakini licha ya yote mwisho wa siku tunataka kuona wewe unafanya kitu hali inakuwa nzuri.
 
Hawa Watoto vipi? kila kata ina sekondari, wanapanda basi kwenda wapi?

Kutoka azikiwe (dar 0km) hadi gongo la mboto ni 20km yaani 45min kwa mguu. Nihalali kweli mwanafunzi kupanda gari kutoka mnazi mmoja hadi forodhani sec. mpirani wanakimbia 90min kutembea 15min hawataki!

Toyota Coaster ni us$35,000 japani hapo haujaweka freight ushuru registration road licence, zingatia itakuwa imetembea 400,000km halafu zinapigwa rivasi zinabaki 89,000km. Brand new ni 200m halafu uanze kutoza nauli 100/=

Bei ya diesel ni 2000/=, tairi @350,000/= (firestone), nadhani nauli iwe moja tu hakuna cha mtoto wanaoshindwa watembee kwa mguu. niliwahi toroka jkt chita kwa mguu hadi moro then nikapanda basi kuja dar, nilikuwa naenda kujaza form za udsm. Kama wanania ya kusoma kweli watatembea watasoma na kufaulu.

Dah,nadhani unayoyaandika mpaka PC yako inakushangaa!! haiwezekani na wala sitaki kuamini kuwa unaandika haya ukiwa na akili timamu kabisa.Hivi unaishi TZ wewe au? mbona sioni pointi yoyote mkuu huoni aibu kabisa.Ebu fikiria mara mbili kama unaweza kuongea pumba hizi mbele ya watu au kwa sababu hatukuoni !!! Ebu fikiria watu acha ubinafsi na kutokuwa mkweli.

''Nothing in the world is more dangerous than sincere ignorance and conscientious stupidity'' Martin Luther King, Jr.:

Waberoya
 
... niliwahi toroka jkt chita kwa mguu hadi moro then nikapanda basi kuja dar, nilikuwa naenda kujaza form za udsm.

Hii imenisikitisha sana. Hakukuwa na sababu ya kufanya watu waende Dar kujaza form za chuo.

Wakati wa JKT ( na inarudi tena) nadhani ilikuwa huwezi kwenda chuo mpaka upitie JKT. Kwa hiyo, wakati wowote ule eligible candidates wote wa chuo wanapatikana JKT. Sasa serikali inashindwa nini kuweka ma application form ya vyuo kwenye li bahasha na kuyatuma JKT zote za nchi ? You will reach all Tanzanians eligible for college. What's so hard about that jamani ? Au kama hiyo ni ngumu, watu wa JKT, kwa ruhusa ya vyuo, wanashindwa nini kutoa ma photo copy ya application forms za vyuo kugawia wanafunzi huko huko JKT ?

Inefficiencies ndogo ndogo kama hizi ndio hizo hizo ziko kila mahala, na ndio maana hatuendelei. Yani vitu vidogo kupita kiasi vinatushinda.

By the way, umbali kutoka Chita JKT, kule Kilombero interior, mpaka Moro mjini nadhani ni zaidi ya mara mbili ya kutoka Moro mjini mpaka Dar. Sasa kwa nini ulishindwa kumalizia kula mkia huo wakati ng'ombe ushamkata kuzidi nusu ? Unless, hakukuwa na mabasi kutoka Chita mpaka Moro. Pole.
 
...I wish Big Ben angerudi tena madarakani pamoja na ufisadi aliofanya angalau ali-take trouble kumwagilia nakuweka mbolea kwenye mmea kisha akajichumia tumatunda twake akalala mbele sasa huyu mkwere kala matunda aliyolima mwenzake na hana dalili ya kumwagilia mmea angalau matunda mengine yapatikane.....Halafu mnamsingizia mungu kuwa ametuachagulia mnaletea utani nyie...
 
Kipanga ulichosema ni kweli tupu!

Nabaki kusikitika kwamba wadanganyika sasa tumefikia hali mbaya ya kuanza hata kumtamani FISADI MKAPA!
 
Tangu aingie JK kwa muda mfupi tumeona
1.Migomo ya wanafunzi vyuoni imeongezeka kwani sasa hata wanafunzi wa sekondari na shule za msingi wanangoma
2.Uvunjwaji wa haki za binadamu-kubomolewa nyumba tabata na migogoro mingi ya viwanja
3.Kuvamiwa kwa waandishi wa habari
4.UFISADI
Hadi sasa hata miaka 3 bado afadhali hata MKAPA alianza kuharibu mwishoni lakini huyu jamaa mpaka miaka 10 ikipita sijui itakuwaje
 
Manung'uniko yamekuwa mengi sana katika Serikali hii ya awamu ya nne compared na serikali ya BM... na mbaya zaidi ni pale tunapoona kwamba Kiongozi mkuu wa Serikali anaendeleza kutabasamu na kuwachekea hao watuhumiwa ambao wanafanya kila jitihada kuumiza umma wa Watanzania.

BM ni bora kuliko huyu Kikwete tulienaye sasa, ila tungeshindanisha nani ni bingwa wa kusafiri badala ya Administration nadhani BM asingemkaribia JK hata kwa theluthi...

By the vway JK yupo busy na majukumu ya AU [I sincerely hope that members wote wa AU watakuja kupiga kura katika Uchaguzi wa TZ wa 2010]
 
Yaani naona hii ni hadithi ya zimwi likujualo... Kufa ni kufa tu, hakuna zimwi zuri, yote yanatula na tunakufa taratibu
 
Back
Top Bottom