akilimtindi
JF-Expert Member
- Jun 30, 2008
- 421
- 83
Nani bora kati ya JK au Mkapa aliyekoroma tukanyamaza ingawa "underground" alifanya ubaradhuli?
Nauliza hivi kwasababu JK kama ni rubani basi keshatoka nje ya ndege na sisi hatuna habari. Kama yupo bado kwenye ndege yetu basi tusijiaminishe na safari yetu maana rubani wetu anashinda chooni tena hayuko peke yake, ana limwanamke lake la kiarabu au vinginevyo wameamua kusahau kwamba kuna haja ya kucheki ndege inakwenda wapi au imefikia wapi.
Kama ni referee basi hapa naona amekimbilia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo na sasa amekwama huko kwa kisingizio cha kusimamia wageni wavae vizuri. Nadhani huko nako hakosi jimama yuko nalo maana naamini huyu referee ni mtu wa vimwana. Huku uwanjani mpira unajicheza wenyewe na matokeo ni kwamba kwanza wenye nguvu ndio wanaopiga mpira na wanapiga kuelekea wanakotaka wao, kisha wakiona kuna wasiyemtaka anataka kupiga mpira wanauchukua wanashika kwa mikono. Baya zaidi hata ambao hawakuwepo kwenye mechi sasa wameingia uwanjani nao wanataka kupiga mpira na wanapewa wanapiga wanakotaka, tena ikibidi wanapiga hadi kwa watazamaji ambao wanaushika kwa muda kisha wanawapa tena wale wababe ambao wanaamua wapige au la tena wapige kuelekea upande gani...???
Je, mechi hii itakwisha? Ni nani atashinda? Je, tuwaache wenye mabavu wapige mpira kwenda wanakotaka? tuwanyang'anye kwa nguvu au tubadilishe referee maana hata hivyo hayupo tena uwanjani?
Mifano halisi ya mpira kupigwa kwa watazamaji na kuushika kwa muda ni kama ripoti ya madini kupewa Sinclair mtu asimamaye kama mtazamaji
Mifano halisi ya mijibwa kushika mpira kwa mikono ni kama Mafisadi ku-hold kesi zao zisiende mahakamani
Mifano halisi ya rubani kushinda chooni au referee kushinda kwenye vyumba vya kubadilishia nguo ni kama JK kushinda nje ya nchi halafu akirudi anatueleza habari za huko maana hajui hapa ndani mambo yalikuwaje.
Mwisho nilimsikia Pinda akichemsha tena bungeni na kushusha hadhi yake kwamba JK hakuweza kuhutubia wananchi kwa kipindi ambacho hana hakika nacho, ("miezi miwili hivi..., sidhani kama ni mitatu"- Pinda) kwa kuwa alikuwa busy nje ya nchi. (JK alipohutubia alidhihirisha hajatuhubiria pumba zake kwa miezi mitatu na hakufanya hivyo kwasababu wananchi walipenda live performance yake, siyo recorded aliyokuwa akiacha zamani ikarushwa hata kama hayupo - contradiction with Pinda, his very PM). Je, haiwezekani mambo mengine mengi na ya msingi kuhusu nchi yetu kukwama kwa kuwa prezidaa yuko bize nje ya nchi most of the time?
Je, tutafika kwa style hii ya rubani kushinda chooni? Ningeshukuru Mungu walaa kama ndege yetu ingefika bila kukwaa mlima maana huo ndio wasiwasi wangu mkubwa kwa sasa...!!!