Nani atazishauri mamlaka za Tanganyika?

Nani atazishauri mamlaka za Tanganyika?

Taifa liko kwenye mkwamo wa vifo vya maelfu, maombolezo ni kila kina, vilio ni kila mahali matanga ni kote
Wengine wamezika nguo... Wengine bado wanawatafuta wapendwa wao, sintofahamu ni kubwa sana kwa ambao hawajulikani walipo ... Majeruhi ni wengi, acha walio mahabusu na wale waliopewa kesi za uhaini... Tusiwasahau na waliofichwa kwenye nyumba za siri za mateso

Kwa mshangao mkubwa na taharuki ya kuishangaza dunia ccm kwa kushirikiana na mamlaka wako busy kuapishana bungeni na kupeana vyeo

Hakuna kauli ya chama

Hakuna kauli ya serikali

Hakuna kauli za viongozi

Wote wako kimya as if nothing bad has happened!

Ninini hiki lakiniTanganyika inapitia!?😭😭😭
View attachment 3501388
Wataanzaje kutoa pole wakati walituambia waliouwawa walitoka nje ya nchi?? Na tayari wameshazika miili ya ndugu zetu kwenye makaburi ya pamoja . Wakitoa pole itabidi watuambie nani aliuwa ndugu zetu.

Watanganyika wamepigwa risasi mchana kweupe, hakuna hatua zitakazochukuliwa.
The way forward, ni tarehe 9 Dec.
 
Sishangazwi na reaction ya serikali kujifanya hamna kilichotokea na kuendelea na shughuli zao, kwa sababu serikali ndio muhalifu aliyeua watu 10k+, unatarajia nini? waje mbele wakiri kilichotokea, I mean walichokifanya? Nope.

Nashangazwa na taasisi zinazoiambia serikali ifanye uchunguzi kuhusu mauaji ya trh 29, ni kama kumwambia muhalifu ajichuguze then akijikuta na hatia ajishtaki.

Nashangazwa na watu wanaojua kilichotokea lakini bado wanaendelea kujadili nani awe waziri, mara makonda this, nchemba that, as if serikali ipo kwenye power kihalali.
Mtu mwenye utimamu hawezi kuitambua hii serikali, kwa sababu haipo kihalali.
 
Like seriously?
20251114_015506.jpg
 
Nani wa kumfunga paka kengele. Ngoja mwenyewe atoke aseme atakayksema utaona viitikio vyao. Sasa hivi hawajui anawaza nini. Wamejawa na hofu.
HONGERA na POLE Kwa MWIGULU MCHEMBA.

1. Nimeupokea uteuzi wa Waziri Mkuu Mwigulu Mchemba kama ndoto ya mchana. Nampongeza kwa sababu waliokuwa wanataka hiyo nafasi ni weeeeeengi. Waliishashona suti lakini simu zao zikawa hazipokelewi na “sponsor”na mwishowe zikawa “blocked”. Kwa hiyo, hongera kwa kuonekana kati ya weeengi walioitaka hiyo nafasi.

2. Nakupa POLE SANA kwa sababu mbili. Kwanza, katiba yetu inatupatia RAIS MTENDAJI. Ukiaminishwa au kujiaminisha kuwa wewe ni mtendaji, ndipo utagundua kuwa nyoka ana miguu. Nakushauri “unyatenyate”, usitembee kwa mikogo, na kwenye kiti kalia kwa tako moja tu, jingine libaki hewani. Usicheke, Uzingatie. Pili, kigezo kilichotumika kukuteua (SIRI YA BOSS) huwezi kukijua. Siku ukikijua, muda wa kukaa ofisi utakuwa umeisha.

3. Taifa liko gizani hata kama taa zinawaka. Punguza ahadi, fungulia matumaini. Watanzania waliishaahidiwa mengi na kuletewa ambayo hawakuahidiwa: Risasi za moto kwa watoto na vijana. Usifanye sherehe, tuko msibani.

4. Aliyekuteua, halazimiki kufuata unachomshauri. USINUNE. Boss hanuniwi. Wewe ni mshauri wake kikatiba; yeye ni mshauri wako kiuhalisia. Katiba ni kijitabu, fuata uhalisia.

5. Bila shaka umewahi kusikia gonjwa linaitwa UTEKAJI. Popote uendapo; Usipoaminika utamkapo kitu, usiposhangiliwa, ukinuniwa, ukifanyiwa unafiki, ukiona machozi machoni pa watu, na ukiona tabasamu la kulazimisha, ujue gonjwa hilo tayari liko hapo. Usiliogope maana linakujua na wewe unalijua. Usilionee aibu maana lenyewe halina aibu. Msipoteze fedha zenu kwa waganga na manabii. Gonjwa hili ndilo mchawi wetu.

6. Kwa kuwa hakuna aliyejitokeza mpaka sasa kutufariji, nakushauri usikimbilie kufariji. Ruhusu watu walie na kuomboleza. Wengine wanalia vibaya - waache walie. Taifa linahitaji uponyaji. Anayezuia watu kulia, anayewawinda mtandaoni, anayeendelea kuwasaka wanaolia, ndiye aliyeleta kilio na anakerwa na vilio. Kifo hakina aibu, kwa wazikaji muone aibu?

Bila shaka utaapa ili uanze kazi yako. Fungua Biblia/Koran hiyo uone ndani kama kuna maandiko matakatifu au tunachoona ni box tu la kushika ili kuapa.

Nayasema haya kwa sababu sisi viongozi wa dini tumewafanya muamini kuwa mbingu haipo. Tumetengeneza mbingu hapa hapa, na jehanamu hapa hapa.

Hongera na Pole tena.
Umepata kazi au Kazi Imekupata?
 
Taifa halina Wazee, wote wamenunuliwa au hofu imewakamata. Sehemu wasipokuwepo lazima vurugu zitamalaki.
 
Wengine wameanza kukata tamaa na kufikia kuona kama Mungu ametusahau?,au Mungu hayaoni haya?,au Mungu hasikii maombi yao?
Mungu yupo ,Mungu anajibu kwa wakati wake hakawii wala hawai anajibu kwa wakati.
MUNGU WA HAKI ANAJIBU KWA HAKI YAKE...kila mmoja Mungu atamlipa kwa haki yake sawasawa na stahiki yake kadiri ya matendo yake.
KISASI na HUKUMU ni kazi ya Mungu,ni juu ya Mungu...Mungu atajilipizia kisasi kwa hukumu yake ya ghadhabu yake hasira yake Mungu kwa haki yake...

Zab 53:1
Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wametenda uovu wa ufisadi na kuchukiza, Hakuna atendaye mema.

Rum 1:28-32

Kwa maana ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wanadamu waipingao kweli kwa uovu. Kwa kuwa mambo ya Mungu yanayojulikana yamekuwa dhahiri ndani yao, kwa maana Mungu aliwadhihirishia. Kwa sababu mambo yake yasiyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana, na kufahamika kwa kazi zake; yaani, uweza wake wa milele na Uungu wake; hata wasiwe na udhuru; kwa sababu, walipomjua Mungu hawakumtukuza kama ndiye Mungu wala kumshukuru; bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza. Wakijinena kuwa wenye hekima walipumbazika; wakaubadili utukufu wa Mungu asiye na uharibifu kwa mfano wa sura ya binadamu aliye na uharibifu, na ya ndege, na ya wanyama, na ya vitambaavyo. Kwa ajili ya hayo Mungu aliwaacha katika tamaa za mioyo yao, waufuate uchafu, hata wakavunjiana heshima miili yao. Kwa maana waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo, wakakisujudia kiumbe na kukiabudu badala ya Muumba anayehimidiwa milele. Amina. Hivyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili; wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke, ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa, wakapata nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao. Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa. Wamejawa na udhalimu wa kila namna, uovu na tamaa na ubaya; wamejawa na husuda, na uuaji, na fitina, na hadaa; watu wa nia mbaya, wenye kusengenya, wenye kusingizia, wenye kumchukia Mungu, wenye jeuri, wenye kutakabari, wenye majivuno, wenye kutunga mabaya, wasiowatii wazazi wao, wasio na ufahamu, wenye kuvunja maagano, wasiopenda jamaa zao, wasio na rehema; ambao wakijua sana hukumu ya haki ya Mungu, ya kwamba wayatendao hayo wamestahili mauti, wanatenda hayo, wala si hivyo tu, bali wanakubaliana nao wayatendao.

Methali 6:16-19
Kuna vitu sita anavyochukia Mwenyezi-Mungu; naam, vitu saba ambavyo ni chukizo kwake: Macho ya kiburi, ulimi mdanganyifu, mikono inayoua wasio na hatia, moyo unaopanga mipango miovu, miguu iliyo mbioni kutenda maovu, shahidi wa uongo abubujikaye uongo, na mtu achocheaye fitina kati ya ndugu.


Danieli 5:20 BHN
Lakini alipoanza kuwa na kiburi, akawa na roho ngumu na mwenye majivuno, aliondolewa katika kiti chake cha enzi, akanyanganywa utukufu wake.

MENE MENE TEKELI NA PERESI

Maandishi yenyewe ni: ‘MENE, MENE, TEKELI, PARSINI.’ Na hii ndiyo maana yake: MENE maana yake, Mungu amehesabu siku za ufalme wako na kuukomesha. TEKELI maana yake, wewe umepimwa katika mizani, nawe ukaonekana huna uzito wowote. PERESI maana yake, ufalme wako umegawanywa kati ya Wamedi na Wapersi

Kut 3:7-9
BWANA akasema, Hakika nimeyaona mateso ya watu wangu walioko Misri, nami nimekisikia kilio chao kwa sababu ya wasimamizi wao; maana nayajua maumivu yao; nami nimeshuka ili niwaokoe na mikono ya Wamisri, niwapandishe kutoka nchi ile, hata nchi njema, kisha pana; nchi ijaayo maziwa na asali; hata mahali pa Mkanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi. Basi, tazama, kilio cha wana wa Israeli kimenifikilia; tena nimeyaona hayo mateso ambayo Wamisri wanawatesa.
 
Taifa liko kwenye mkwamo wa vifo vya maelfu, maombolezo ni kila kina, vilio ni kila mahali matanga ni kote
Wengine wamezika nguo... Wengine bado wanawatafuta wapendwa wao, sintofahamu ni kubwa sana kwa ambao hawajulikani walipo ... Majeruhi ni wengi, acha walio mahabusu na wale waliopewa kesi za uhaini... Tusiwasahau na waliofichwa kwenye nyumba za siri za mateso

Kwa mshangao mkubwa na taharuki ya kuishangaza dunia ccm kwa kushirikiana na mamlaka wako busy kuapishana bungeni na kupeana vyeo

Hakuna kauli ya chama

Hakuna kauli ya serikali

Hakuna kauli za viongozi

Wote wako kimya as if nothing bad has happened!

Ninini hiki lakiniTanganyika inapitia!?😭😭😭
View attachment 3501388
Our country!
Lord have mercy.
 
Taifa liko kwenye mkwamo wa vifo vya maelfu, maombolezo ni kila kina, vilio ni kila mahali matanga ni kote
Wengine wamezika nguo... Wengine bado wanawatafuta wapendwa wao, sintofahamu ni kubwa sana kwa ambao hawajulikani walipo ... Majeruhi ni wengi, acha walio mahabusu na wale waliopewa kesi za uhaini... Tusiwasahau na waliofichwa kwenye nyumba za siri za mateso

Kwa mshangao mkubwa na taharuki ya kuishangaza dunia ccm kwa kushirikiana na mamlaka wako busy kuapishana bungeni na kupeana vyeo

Hakuna kauli ya chama

Hakuna kauli ya serikali

Hakuna kauli za viongozi

Wote wako kimya as if nothing bad has happened!

Ninini hiki lakiniTanganyika inapitia!?😭😭😭
View attachment 3501388
the end justifies the so called....
 
Back
Top Bottom