Imekuwa ni mazoea ya sisi watanzania kulalamika sana kwenye media mbalimbali hasa linapotokea jambo linalogusa na kuathiri maisha yetu. Hivi karibuni gharama za umeme zimetangazwa kupanda, baada ya muda nauli zitapanda pamoja na gharama za chakula, kinachoshangaza ni sisi wenyewe waathirika kutochukua hatua ili kuondoa madhila haya tumebaki kulalamika na baadae tutazoea na kuona kawaida tu huku tunazidi kuumia na kuwa masikini, nani atatulilia ikiwa tuliofiwa tunacheka. nini suluhisho; chama kingine na serikali nyingine au wananchi wenyewe tukatae hali hii kwa maandamano na njia nyingine yeyote? kama ni kuamua ni sasa.