Nani atafidia madeni haya NMB?

Lihakanga

JF-Expert Member
Dec 17, 2016
4,823
6,401
Nina uhakika kuwa wengi wa wafanyakazi ambao wataachishwa kazi baada ya uhakiki wa vyeti, walikuwa na mikopo katika taasisi mbalimbali za kifedha akiwemo mkopeshaji mkuu wa watumishi wa umma ambaye alipewa dhamani pia kupitisha mshahara ya watumishi wa umma katika wilaya zote nchini.
Kwa wale waliokopa na sasa ajira imesitishwa, nani atawalipia madeni ya mikopo hiyo NMB?
Mytake: serikali imeamua kwa haraka mno, ilitakiwa ifikirie athari kama hizo ambazo zimesababishwa na zoezi la uhakiki kama ya kutengua ajira za watumishi hao.
 
Ungetuambia kwanza kama ule mkataba unasemaje ukifukuzwa kazi na kama ukifa,,,tukishajua hapo ndio tutakua na la kusema
 
Matokeo kidato cha nne, div 1 moja, d
div 2 moja ,
Div 3 Na 4 hakuna,
sifuri 200.
Afisa elimu: mkuu wa shule mbona wanafunzi wengi wamefeli
Mkuu wa shule: tumewaandaa wawe wakuu wa Mikoa Na wilaya
 
Itategemea mikataba yao na benki walikubaliana vp, tofauti na bima km wenzangu walivyoelezea hapo, pia wana mafao yao nssf, pspf kwa kipindi hicho walichofanya kz huenda yakatumika kukatwa madeni yao
 
Bima haihusiki na mtu kuachishwa kazi au kuacha kazi, bima ina cover mtu akifariki au akipata ukemavu wa kudumu, reasons beyond there Lender inabid adili na mkopaji husika,akishindwa kumpata imekula kwake!
 
Back
Top Bottom