Nani anastahili msaada wa kwanza hapa?

Nani anastahili msaada wa kwanza hapa?

ESCORT 1

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2015
Posts
1,501
Reaction score
3,342
Wanabodi Habari Zenu.

Nimepata Mtihani Kama Sio Majaribu Kwani Mama Yangu Mlezi (Aliyenilea Mpaka Nimekua) Anaumwa Sana Huko Kijijini Kwetu Na Wakati Huohuo Mpenzi Wangu Aliyenizalia Mtoto Wangu Mpendwa naye Anaumwa MNO na Wote Wananitegemea Mimi Ili Waweze Kupata Matibabu.

Sasa Mtihani Unakuja Kidume Nimeuwawa Kama Sio Kufulia Kulikobobea Na Ukizingatia Haya Majipu Yanayoendelea KUTUMBULIWA Yamenigusa Kwa Namna Fulani Hivyo Kwa Lugha Nyingine Niko Juu Ya Mawe.

Nimepata Kahela Kidogo Ila Sasa Hakatoshi Kuwahudumia Wote Wawili Kwa Pamoja. Yupi Nianze Kumhudumia Katika Matibabu Kati ya Mama Aliyenilea Kule Kijijini Na Huyu Mpenzi Wangu Ninayeishi Nae Japo Sijamuoa Lakini Tuna Mtoto Mmoja Nae??

Mawazo Yenu Wakuu Yanahitajika Maana Nipo Kwenye MAJARIBU Mno, Maana Kila Mtu Ana Thamani Kubwa Kwangu.
 
Mama ndo kila kitu katika hii dunia....Akili kichwani
 
Fanya kama roho wa bwana atakavyokuongoza
 
Sioni kama kuna mtu anatakiwa awe wa kwanza na mwingine awe wa mwisho. Fanya mipango huyo wa kijijini apelekwe hospital na huyu mpeleke hospital.

Hiyo hela uliyonayo fanya iwe ya vipimo kwa wote. Baada ya hapo wakishatibiwa Mungu atakufungulia milango.

Ukibagua kama likitokea la kutokea unalo brother. Make a wise decision, mambo mengine Mungu huleta ili aone unamtegemea kiasi gani. Pole sana
 
maneno kuntu
 
Mmoja anaumwa sana.. Mwingine anaumwa mno.. mimi naona uyo anae umwa sana apate attention kubwa zaidi ila hata uyu mwingine usimpotezee
 
Sioni kama kuna mtu anatakiwa awe wa kwanza na mwingine awe wa mwisho. Fanya mipango huyo wa kijijini apelekwe hospital na huyu mpeleke hospital.

Hiyo hela uliyonayo fanya iwe ya vipimo kwa wote. Baada ya hapo wakishatibiwa Mungu atakufungulia milango.

Ukibagua kama likitokea la kutokea unalo brother. Make a wise decision, mambo mengine Mungu huleta ili aone unamtegemea kiasi gani. Pole sana

Asante Sana Mkuu Na Ubarikiwe Kwa Ushauri Wako Uliobobea Ambao Umenipa Mimi Bila Ya Kunichaji.
 
Mkuu hujawaunga na Bima ya afya? Ni muhimu sana hasa unapokuwa huna cash
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom