Nani anastahili kulipa kodi ya jengo?

Donyongijape

JF-Expert Member
May 28, 2010
1,497
812
Habari wanabodi.

Hivi karibuni nimepata Hati ya Madai ya Kodi ya Jengo kwa Mwaka 2015/2016 ya kibanda changu ambacho kina umri wa mwaka mmoja. Eneo langu halina HATI (TITLE DEED) ni mikataba tu ya kuuziana eneo.

Sasa ningependa kujua kutoka kwa Manguli wa Sheria au Wenye uzoefu humu JF, je hata Mimi natakiwa kulipa hio kodi ya Jengo ilihali sijapata Title Deed na hakuna report yoyote inayoonyesha value ya Nyumba yenyewe zaidi ya kiwango kilichoandikwa kwenye hio hati ya Madai (Demand Notice)?.

Naomba msaada tafadhali. Ningetamani mnifafanulie zaidi, ikiwezekana na vifungu vya sheria.

Asanteni sana.
 
Umepokea hiyo taarifa kwa njia gani? Kama ni barua, itoe photocopy kisha uipeleke ofisi za manispaa yako. Waulize haya maswali yote uliyouliza, kama hawaeleweki nenda ofisi ya mkuu wa mkoa au wizara ya ardhi.
 
kama unamiliki jengo lolote lazima ulipe kodi na kodi unayotakiwa kulipa ni 0.15% ya thamani ya jengo ila wakadiriaji kodi wanatabia ya kuweka kodi kiwango cha juu hapo itabidi mpambane ikiwezekana mtathimini aitwe ili kupata thamani halisi ya jengo
 
Ukienda ofisi ya afisa mtendaji kata utapata orodha na kiwango cha kodi, kuna aina mbili ya njia ya kudai hiyo property tax, njia ya kwanza huwa wanakadilia tu nyumba yako na mara nyingi viwango vya kodi huwa ni vidogo na aina ya pili huwa wanaokotoa kutoka kwenye valuation report, kuna baadhi ya miji wamefanya majaribio kwa baadhi ya blocks/mitaa ambapo katika baadhi ya miji kodi kwa nyumba ya makazi huwa ni 2% ya thamani ya nyumba na kama ni makazi na biashara huwa ni 4% na kama ni biashara tu basi huwa ni 6% ya thamani ya nyumba kwa market price na sio gharama za kujengea
 
Kodi hii ni mpaka wathaminishe jengo lako lina thamani gani ndipo watakupa kodi itakayo tozwa,
 
Kodi ya MAJENGO ni kodi inayotozwa kwa mmiliki wa jengo la makazi au biashara... jengo hilo ufanyiwa tathimini na kutoa kodi yko...
 
NI KODI YA JENGO. NIMEISIKIA LEO ILA BADO SIJAIELEWA

Yanini utusumbue humu Mkuu? Piga tu haraka hii namba 0800750075 utajibiwa kila aina ya Swali lako huko. Usisahau kuja kushukuru huku ukimaliza kupewa ufafanuzi wote uliokuwa ukiuhitaji kutoka Kwao. Kila la kheri!
 
Habari wanabodi.

Hivi karibuni nimepata Hati ya Madai ya Kodi ya Jengo kwa Mwaka 2015/2016 ya kibanda changu ambacho kina umri wa mwaka mmoja. Eneo langu halina HATI (TITLE DEED) ni mikataba tu ya kuuziana eneo.

Sasa ningependa kujua kutoka kwa Manguli wa Sheria au Wenye uzoefu humu JF, je hata Mimi natakiwa kulipa hio kodi ya Jengo ilihali sijapata Title Deed na hakuna report yoyote inayoonyesha value ya Nyumba yenyewe zaidi ya kiwango kilichoandikwa kwenye hio hati ya Madai (Demand Notice)?.

Naomba msaada tafadhali. Ningetamani mnifafanulie zaidi, ikiwezekana na vifungu vya sheria.

Asanteni sana.
KAMA UNAWAPANGAJ WALA USIWAZE

GAWANYA HIO HELA KWA IDADI YAO WALIPE
WAKIGOMA MWISHO WA KODIZAO WAOANDISHIE ONGEZEKO LILELILE ASIETAKA AKAKAE KWABABAKE
 
kama unamiliki jengo lolote lazima ulipe kodi na kodi unayotakiwa kulipa ni 0.15% ya thamani ya jengo ila wakadiriaji kodi wanatabia ya kuweka kodi kiwango cha juu hapo itabidi mpambane ikiwezekana mtathimini aitwe ili kupata thamani halisi ya jengo
0.15% *thamani ya nyumba, je kwa bajeti hii mpya si kuna mabadiliko? kwa mwaka tutatumia calculation zipi kupata kodi ya jengo......,na nyumba yangu mpaka nianze kuchajiwa kodi ya jengo ni masharti gani ni lazima niyatimize kuanza kulipa kodi ya jengo
 
0.15% *thamani ya nyumba, je kwa bajeti hii impya si vitu vimebadilika, kwa mwaka tunatumia calculation zipi kupata kodi ya jengo......,na nyumba yangu mpaka nianze kuchajiwa kodi ya jengo ni masharti gani ni lazima niyatimize
Kwa bajeti hii hakuna kilichobadilika ila kwa nyumba ambayo haijafanyiwa tathimini ya chini watachaji 10,000/= na ghorofa watachaji 50,000/= lakini kwa zile zilizofanyiwa tathimini gharama itabaki ileile 0.15% ya thamani ya nyumba
 
Back
Top Bottom