Pamoja na kwamba sio kigezo kikuu kama unavyofikiri lakini lazima tukubali GPA ndio kigezo cha kwanza cha kupimia. Tangazo la kazi linapotoka huenda wakatokea watu wengi wakaomba kuliko idadi ya nafasi zilizopo. Assumption kubwa inayofanyika ni kwamba hakuna hata mmoja ambaye anafahamika zaidi ya ku-rely kwenye documents alizowasilisha. Hebu tusaidie ndugu, una applications za watu A wenye GPAs 3.8-4.5 na B wenye GPA ya 3.4-3.7; na tunataka tufanye usaili kwa wachache (shortlisting); ni kwa vipi tunaweza kumuacha wa 4.4 na kumuita wa 3.4?? Hebu tusaidie hapa.
Kuwa na GPA kubwa na kushindwa kuonyesha uwezo huo katika kazi, sio kosa la GPA asilani. Hatuwezi kulaumu GPA hapa (Rejea debate ya correlation and causation). Ni kosa aidha la mfumo uliopo unaozalisha hizo GPA au makosa mengine ambayo yanahitaji more research kuyabaini. Katika hali ya kawaida (ceteris paribas), tunatarajia mwenye GPA kubwa atachukuliwa amefuzu zaidi kuwa shortlisted kuliko mwenye GPA ndogo; kwani nyote mmepimwa na vigezo hivyohivyo isipokuwa yeye amefanya jitihada ndio maana akapata GPA kubwa kwa hiyo pia ni dalili njema kwamba mtu huyo ana chembe za kufanya jitihada katika kazi. Niliwahi kusoma utafiti mmoja unasema kuwa wenye GPA kubwa huwa wanashindwa kuonyesha uwezo huo ni kwasababu ya hali ya ku-relax baada ya kupata viwango hivyo (wanaamini wao wamefika; they are over-bright! business is over, hakuna gumu tena mbele yao; hali yakuwa wenye GPA ndogo wanakuwa na hali ya wasiwasi na hivyo kuwapa nafasi ya kutaka kusahihisha makosa yao (wanajua kwamba kwanini wamepata GPA ndogo). They want to hide their weaknesses; as they do so, is how they keep on performing!
Kuhusu kutofautiana njia za kukokotoa GPA, nadhani haina nguvu sana kwasababu GPA za kutoka sehemu tofauti zinafanyiwa "equivalent" kutokana na workload wanazopewa katika kusoma kwao lakini kiwango cha GPA kikilinganishwa duniani kote kinakuwa na rate sawa (given that mfumo wa elimu katika nchi husika ni wa kimataifa na usimamizi ni mzuri).
Kwa upande wa incompetence ya wahadhiri wetu, nadhani tatizo ni ushirikishwaji mdogo wa kuweza kujenga uwezo wa kuunganisha (linkages) kati ya policy issues and academic issues. Kwa msingi huu, utabaini Mhadhiri ambaye ametokea kwenye kazi nyingine nje ya kufundisha anakuwa yuko more exposed na policy issues hivyo anachokifundisha anaweza kukitafsiri katika misingi ya kisera kitu ambacho muhimu kwa wanafunzi wa elimu ya juu kufahamu. Katika kupunguza changamoto hizi, na ikizingatwa kuwa vyuo vina kawaida ya ku-retain vijana wao waliofulu vizuri; nchi zilizoendelea huwa zinawa-attach wahdhiri wao kufanya kazi za kiutafiti au uchambuzi katika taasisi tofauti (Say, World Bank, Google, UN, Government Ministries, nk) ili wapate real sense on how policy design, formulation and analysis is being undertaken na hatimaye waje watumie uwezo huo katika kuhudumu shughuli za uhadhiri. Bahati mbaya hili halifanyiki kwetu. Ukute chuo kimeomba wahadhiri wake wawe attached na Wizara za Kisera zinazihusiana na maeneo yao ya kufundisha, nop! Hivyo, as long hatuna njia mbadala sana zaidi ya GPA ambayo tutaingalia kwenye Transcript yake, nadhani bado hoja yako haina nguvu sana. Labda hoja ya utofauti wa vyuo kwa ngazi ya Kimataifa, lakini sio kitaifa. Naweza nikaamini mwenye GPA ya 4.0 kutoka Harvard "huenda" akawa mzuri kuliko mwenye 4.5 ya Tanzania, hii ni kutokana na ulinganisho wa nchi katika ubora wa kiwango cha elimu na miundombinu ya kusomea iliyopo Harvard na aina ya wanafunzi aliosoma nao akiwa Harvard au Princeton kwa ujumla. Lakini UDSM vs Mzumbe, au SUA vs UDSM, kwangu sioni kama kuna tofauti kubwa
Watakaokwazika kwa maelezo marefu haya kidogo nawaomba msamaha; ni kutokana na uzito wa mada husika ambao unagusa maslahi ya nchi kwa upana wake.