Nani anastahili kufundisha chuo kikuu?

Nani anastahili kufundisha chuo kikuu?

Hiyo experience waipatie wapi sasa?
Labda useme wawekwe under management ya wenye experience kwa muda wa miaka mitatu.
Ata hiyo hiyo kaka. Ni aibu. Haiwezekani tunawakabidhi watoto watu wasiojua wanafundisha nin. Nakumbuka akati nasoma pale mliman miaka ya 2009's kulikuwa na mateacher wazeee wasumbufusumbufu. At that time nilijua wanazingua lakini kwa sasa nimejua kwanini walikuwa wasumbufu. Zamani ulikuwa hupewi kufundisha mpaka angalau uwe ushawahi kufanya kazi sehemu
 
Ilo la Tz tuu...
Google wenyewee wanasema 16% gpa hawaijui ni mdudu gani katika kampuni yao wanakula maisha dafi
 
Hapo watanzania ndo tunaharibu kabisa G.p.a haziwezi kuangaliwa ktk kujua ufanisi wa kaz ukweli daaah ukweli kama hatutaliangalia hili kwa jicho pevu tutakuwa na wakaririaji wengi sana kuliko wanaoelewa ndo maaana unakuta vyuo vingi wanafundisha kukelemua tu badala ya kuelewa.
 
Kama anaelewa vitu ameshindwaje kufauru na kuwa na GPA kubwa?

!
!
Kwa sababu sikariri ndio maana sina GPA kubwa. Lijitu linajesha kukariri vitu vilivyoandikwa kama vilivyo... Au huyu mwingine kuutwa kutoa papuchi, au ananunua mitihani..... Kimsingi gpa si chochote si lolote. Ingekuwa ni kitu vmcha maana huenda leo IFM wangekuwa wamekabidhiwa benki kuu.
 
Mmmmh!Hivi ni kweli ufanisi wa mtu upo kwenye GPA?
kwa kiasi lakini siyo kama tunavyotekeleza hapa nchini. Kuna daraja la kwanza (4.4-5), daraja la pili la juu (3.5-4.3), daraja la pili la chini (2.7-3.39) na ufaulu wa kawaida. Kiwango anachotakiwa kuwa nacho mtu anayetarajia kuwa mhadhiri hapa nchini kwa sasa ni wakia (G.P.A) ya 3.8 kwa digree ya kwanza na 4.0 na kuendelea kwa digrii ya pili. Unaweza ukakuta kuna mtanzania mwenye digrii ya pili au ya tatu na G.P.A YA 3.5 undergraduate anaachwa kwamba hafai huku serikali ikitoa vibali vya kuajiri wale wanaoitwa maexpert kwa vile wana 3.8. nafikiri tunakosea heri GPA zetu za 3.5 tunajua zinavyopatikana na si hizi za 3.8 ambazo hatujui hata wamezipatapataje. Nchi nyingine zinawatafutia wananchi wake ajira kwa udi na uvumba hivyo wakikuta chanzi kama hii wapo hata tayari kuwafojishia vyeti.
 
Kwa ushauri wangu naona kigezo cha gpa kingebakia pale pale. Ila waongeze na kigezo cha angalu experience miaka 3. Maana imekuwa aibu kubwa. Tutor anafundisha kitu asichowahi kukiona. Wapo wengi tu nakutanana nao makazini pindi wanapokuja kutembelea vijana wao wakati wa practical na field work. Ni aibu aibu hakuna mfano. Inakuwaje mwalimu anaulizia ata simple issue.
kwa experience naweza kukubaliana na wewe lakini kwa GPA bado kidogo, ni ukweli usiopingika kuwa hamna tofauti kubwa kiuelewa au hata kiutendaji kati ya 3.5-5. Tutaweza kuwapata wenye uwezo zaidi kati ya tofauti hii ya GPA kwa interview. Nafikiri ndio kazi ya interview. kuna kijana alipata sponsor ya PHD nakumwacha mwenye first class baada ya interview lakini kama angeenguliwa kabla ya interview wangepoteza jembe na kuchukua kihiyo.
 
Hebu fafanua kidogo hapo kama hutojali
siku za nyuma baadhi ya vyuo kama SUA, MUST na MZUMBE walikuwa wanaajiri kiwango cha chini cha GPA ya 3.5 na vyuo kama UDSM, IFM, NM-IST ilikuwa ni 3.8. Sasa utumishi wakaja na mpango wakuwa na kiwango kimoja cha ufaulu kwa vyuo vyote vya umma na sifa za kupandishwa vyeo zinazofanana. Hivyo kiwango cha kuanzia kikawa ni 3.5 kwa vyuo vikuu vya umma. Hiyo ndiyo kwa ufupi sana lakini andiko lipo ukigoogle utalipata.
 
Wakati tukiwa na vyuo vikuu vichache kabisa hapa nchini kiwango cha ufaulu cha TUTORIAL ASSISTANT kilikuwa si chini ya GPA 3.8 sawa sawa kabisa na ASSISTANT LECTURER, na LECTURER. Kutokana na ukosefu wa wanataaluma baadhi ya vyuo kama SUA na MZUMBE wakawa na kiwango chao cha GPA ya 3.5 wakiungana na baadhi ya taasisi nyingine za elimu ya juu chini ya NACTE.Hili nilifikiri ni sahihi kuhakikisha kazi wanazoweza watanzania wanajengewa mazingira ya kuzifanya Sidhani kama vyuo vilivyokuwa na wahadhiri wenye GPA za 3.5 walikuwa na ufanisi kidogo katika kazi kiasi cha kuamua KUWAACHA katika soko hili la ajira na kuwapa wageni ambao hata hizo GPA zao hatujui uhalisia. HARMONIZATION SCHEME YA WANATAALUMA WA ELIMU YA JUU imeharibu kila kitu na inajenga mazingira ya TANZANIA kuwa soko la wahadhiri kutoka mataifa mengine bila kuwa na ulazima huo. Vyuo kama Nelson Mandela, UDOM, UDSM, KAMPALA UNIVERSITY wanaidadi kubwa ya wageni wanaohudumu kama visiting lecturers kwa post ambazo watanzania wangeweza kuzifanya kama huu ukiritimba utaondoka. Haiingii akilini nafikiri serikali inahitaji kuchunguza zaidi.
SUA
Minimum 3.8 hacha uongo. Pia vyuo vya NACTE havina GPA hiyo ya 3.5 hata 3 unafanya kazi. Huyo ni sera ya TCU kuwa lecturer lazima undergrads use na 3.5 na masters 4. Japo chuo kinaamua kuweka grade yake. Hii jamii forum mbona inakuwa kama Facebook huku.UDSM haina visting lecturers kiasi kikubwa hivyo zaidi ya wantanzania wenye ufaulu unaoaminika.
 
Hapq hata mimi hupataga ukakasi...utakuta lecturer anajisifu gpa kubwa lakini kwenye kufundisha ziro kabisa yani hana kabisa kipaji cha kuinstruct...linatia usingizi tu na wakati kuna watu wanajua hasa kutema madini lkn ndo ivo gpa imewapiga kofi.
Hawakufundishwa teaching methology husimlaumu.
 
!
!
Na ndio maana wavumbuzi wa vitu vipya sio maprofesa.
Hapa umepiga chumvi mzee. Wasomi ndo wavumbuzi worldwide. Sema kibongo bongo wasomi hatuoni chochote ila unyamwezini uvumbuzi unaibuliwa na wasomi brah! Hata hao unaowasikia wameshine (kina Steve Jobs, Bill Gates and the likes) matechnocrats wao ni wakali wa MIT, Havard etc
 
Kesho TCU ikibadili vigezo vya ufaulu katika kuajiri wahadhiri, 90% humu mtarudi hapa na kuanza kuponda kwanini wanafunzi vyuo vikuu wafundishwe na vilaza.

Overall GPA ni kigezo kimoja kati ya vigezo kadhaa ambavyo hutumika kumpata mhadhiri, ikiwemo GPA kwenye somo husika atakalofundisha, uwezo wa kujieleza kwenye usaili, sifa za chuo alichosomea kabla.

Interviewees hupewa mtihani wa kuandika na baada ya hapo wale watakaofanya vzr hufanya oral interview. Hizi interviews hufanywa na professors na Drs na maswali huwa ni technical (course based and classroom based). Haya hufanywa kwenye vyuo ambavyo hufanya usaili vyenyewe na si kupitia UTUMISHI.

Pia baadhi ya vyuo wanaajiri wahadhiri waliosomea taaluma ya ualimu. Vyuo vingine ambavyo wahadhiri hawakusoma education, huandaliwa workshop za teaching methodology ili waweze kujiandaa vizuri kabla na wkt wa kufundisha.

Kuna baadhi ya vyuo tutorial assistant haruhusiwi kuingia darasani kufundisha kwakuwa hii ni learning post, bali hutakiwa ku understudy seniors wake hadi hapo atakapomaliza masomo ya master's. Ila kwa sababu ya uhaba wa wahadhiri, baadhi ya vyuo hulazimika kuwatumia kufundisha.

Kuna vyuo ambavyo hutangaza nafasi za kazi na kurudia kutangaza lakini hawapati watu. Akipatikana mtu wa nje, hutakiwa ku "certify" vyeti vyake TCU kabla ili aweze kuajiriwa. Haya ni machache tu ambayo nimeyaona mwenyewe.
 
hizi GPA inategemea ni masomo gani!... kwa wale wa medicine GPA doesn't mater at all... "experience matters , as u practice more , ndivyo unavozidi kuwa mzuri ... katika tiba na kufundisha pia " ... ingekuwa madactari wanaangaliwa GPA basi kusengukuwa na madactari kabisa ...

ila hizi kozi nyingine inabidi muangaliwe GPA kwakweli ....
 
kwa kiasi lakini siyo kama tunavyotekeleza hapa nchini. Kuna daraja la kwanza (4.4-5), daraja la pili la juu (3.5-4.3), daraja la pili la chini (2.7-3.39) na ufaulu wa kawaida. Kiwango anachotakiwa kuwa nacho mtu anayetarajia kuwa mhadhiri hapa nchini kwa sasa ni wakia (G.P.A) ya 3.8 kwa digree ya kwanza na 4.0 na kuendelea kwa digrii ya pili. Unaweza ukakuta kuna mtanzania mwenye digrii ya pili au ya tatu na G.P.A YA 3.5 undergraduate anaachwa kwamba hafai huku serikali ikitoa vibali vya kuajiri wale wanaoitwa maexpert kwa vile wana 3.8. nafikiri tunakosea heri GPA zetu za 3.5 tunajua zinavyopatikana na si hizi za 3.8 ambazo hatujui hata wamezipatapataje. Nchi nyingine zinawatafutia wananchi wake ajira kwa udi na uvumba hivyo wakikuta chanzi kama hii wapo hata tayari kuwafojishia vyeti.
Formula za kukokotoa GPA katika vyuo vyote zinafanana?au ndo ukichukua maksi za huku ukaweka Kule GPA inabadilika?
 
!
!
GPA za kwenye vyeti si kitu kabisa. Ni vilaza tu sema kwa sababu moja au nyingine walifaulu mitihani yao. GPA si kitu, muhimu ni uelewa wa vitu. Lijitu linakariri tu linafaulu baadae na lenyewe linakuja kukaririsha watu. Na ndio maana wavumbuzi wa vitu vipya sio maprofesa.
Tutajuaje kama unauwezo kama ulifeli. Wasio na akili ndio hukimbilia kusema GPA si kitu. Halafu Hakuna professor asiye na mchango kwenye field yake
 
Mmmmh!Hivi ni kweli ufanisi wa mtu upo kwenye GPA?
Kwahiyo unataka hata watu waliofeli wapewe uhadhiri. GPA inaweza isiwe kipimo madhubuti cha ufanisi ila ndio kipimo bora so far. Kama mtu alifeli utampa Kazi ya uwalimu kwa kigezo gani?
 
Hapo watanzania ndo tunaharibu kabisa G.p.a haziwezi kuangaliwa ktk kujua ufanisi wa kaz ukweli daaah ukweli kama hatutaliangalia hili kwa jicho pevu tutakuwa na wakaririaji wengi sana kuliko wanaoelewa ndo maaana unakuta vyuo vingi wanafundisha kukelemua tu badala ya kuelewa.
Either ulikariri au ulielewa nakufaulu ina maana GPA yako ni nzuri. Kama ulishindwa vyote wewe ni failure. Unaweza kuwa na vigezo zaidi vya kurecruit wahadhiri ila huwezi toa kigezo cha GPA. Unataka failures ambao GPAs zao sio nzuri ndio wawe walimu? Utawapa Kazi kwa kigezo gani sasa?
 
Hapa umepiga chumvi mzee. Wasomi ndo wavumbuzi worldwide. Sema kibongo bongo wasomi hatuoni chochote ila unyamwezini uvumbuzi unaibuliwa na wasomi brah! Hata hao unaowasikia wameshine (kina Steve Jobs, Bill Gates and the likes) matechnocrats wao ni wakali wa MIT, Havard etc
Watanganyika wengi wavivu wa kusoma na hawapendi elimu hivyo wanatafuta kila njia kuhalalisha failure zao smh. Sielewi wanawezaje kusema mtu mwenye GPA asiwe muhadhiri halafu aliyefeli ndio afundishe
 
siku za nyuma baadhi ya vyuo kama SUA, MUST na MZUMBE walikuwa wanaajiri kiwango cha chini cha GPA ya 3.5 na vyuo kama UDSM, IFM, NM-IST ilikuwa ni 3.8. Sasa utumishi wakaja na mpango wakuwa na kiwango kimoja cha ufaulu kwa vyuo vyote vya umma na sifa za kupandishwa vyeo zinazofanana. Hivyo kiwango cha kuanzia kikawa ni 3.5 kwa vyuo vikuu vya umma. Hiyo ndiyo kwa ufupi sana lakini andiko lipo ukigoogle utalipata.
Kuhusu SUA sio kweli hata kidogo.... si tu zamani bali hata sasa!! SUA hawana shida ya Walimu pale coz' wana monopoly ya agricultural universities. Hivi nyuo vingine lazima wawe na uhaba manake kila chuo kipya kikianza, utasikia LLB, Accounts and the like..... na vyuo vyooooooooooooooooote, unakuta same courses matokeo yake wanakosa walimu wenye sifa.

Mi nimesoma SUA, kwa hiyo miaka ya nyuma unayosema hata hayo mambo ya tutorial assistant mwenye ONLY bachelor degree sikupata kuyaona achilia mbali kuyasikia EXCEPT, kwa miaka mitatu ambayo mimi nilikuwepo, teaching staff mwenye bachelor alikuwa anafundisha somo la BIOMETRY/STATISTICS na bila shaka unaweza kupata jibu kwanini waliweza kumchukua hata mtu mwenye bachelor!! Kwanza kwa wakati ule, hata wahitimu wenyewe wa Statistics walikuwa wachache sana na hilo somo kwa SUA lilikuwa just a back up subject ingawaje lilikuwa na CR hours nyingi.

Kwenye kozi yetu, wenye elimu ndogo walikuwa wawili na kila mmoja alikuwa na MBA and the reason behind, ile kozi yetu ilikuwa na miaka isiyozidi mitano kwahiyo haikuwa na staffs wa kutosha lakini ukirudi kule kwenye kozi ambazo ni pure agriculture; hata kama utaona tangazo na wakakuwekea hiyo 3.5 basi itakuwa ni formalities na wala huwezi kupata coz', usisahau, watu walikuwa wakimaliza pale SUA shahada ya kwanza, wana-fight kusoma shahada ya pili ili kuukwepa ubwana shamba na kwenda vijijini! Na mtu mwenye masters angekuwa tayari kufanya kazi kama tutorial assistant kuliko kumwambia akawe agricultural extension officer na ndio maana ilikuwa ni very rare kukuta mtu mwenye bachelor as a member of teaching staff. Lakini hata kwa miaka ya karibuni, last year nilituma application ya T.A ya dogo na walikuwa wanataka at least GPA ya 3.8.
 
Back
Top Bottom