Nani Anakumbuka Hii

Bora hiyo bongo ilikua unaomba simu kwa operator wa ttcl asubuhi unakuja kupata line jioni
 
Tena imefungiwa na kufuli, unachoweza kukifikia kwa urahisi ni kile cha kupokelea tu ili uweze kuongea lakini sio upande wa namba ili upige.....
 
Duh ilikuwa nouma sana enzi hizo, kama dingi yupo ilikuwa hakuna kukimbilia coz ilikuwa ni lazima asikilize yeye,
kama hayupo sasa ndo vita kila mtu anataka apokee ..
Duh tumetoka mbali sana..
 
Hii mi naona ndo kwanza nipo chekechea na stori yake ni hii ni kuipata kwake tu ni shurubu na ukishaipata tu basi hapo mtaani ni wewe tu mfalme na kuhishimika sana na kerro la hodi hodi na hapo tena ni kuitia kakufuli kadogo hapo mama tena anachagua wale mashoga zake tu
 
Tena imefungiwa na kufuli, unachoweza kukifikia kwa urahisi ni kile cha kupokelea tu ili uweze kuongea lakini sio upande wa namba ili upige.....

Ahahahahaaa bado tulikuwa tunaiba mkuu, mfano Namba 87356 unachofanya unanyanyua receiver halafu unafanya kama unakata kutafuta line, unaanza na nane unakata mara nane haraka haraka hiyo saba hivyo hivyo hadi unamaliza namba zako ukimaliza inaanza kuita unaongea hadi nje tulikuwa tunapiga, bill ikija anabaki analalamika TTCL wamembambikiza hawezi kuuliza mtu wakati funguo zote wameficha wao
 
Alikua hafati statement ya orodha ya simu zilizopigwa?.
 
tumetoka mbali
Saana sana tu tumetoka mbali aisee! nakumbuka kwa bibi yangu ndio kulikuwa na bomba moja la maji tu sasa kuna visichana vilikuwa vinakuja kuomba maji yaani namkumbuka mmoja alikuwa na sweta la kufuma na mkono alafu limefumuka kuanzia kwenye mikono huyo alikuwa kiongozi wa kuiba maji! ha ha haaaaaaa kalikuwa kajanja kama sungura!
 
Aiseee enzi hizo ukisikia inaita hata kama upo msalani unasitisha zoezi
 
ha ha ha ha huyo namjua nitamwambia sasa hivi amekuwa bonge wa sista du ujue
 
Mimi mwenyewe sijawahi kutumia hiyo kitu
 
Watoto wa Professor Kikwete!

Mkuu sio hivyo....mimi binafsi nilikuwepo kipindi hicho ila nyumbani hutukuwa nayo....kule shamba tulikuwa tunaishia kuzisoma tu kwenye vitabu.
 
Alikua hafati statement ya orodha ya simu zilizopigwa?.

Hiyo mkuu ilkuwa inaonyesha kila kitu, hata aende TTCL bado statement itakuwa ni ile ile, nani kapiga na wamebana na kufuli funguo wanazo wao? hata akilalamika itabidi alipe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…