Nani anagharamia matumizi ya Lema, Msigwa na Mbowe huko Nairobi?

Hivi unategemea mtu kama Lema aliyesaidiwa kwa hali na mali na Tundu Lissu hadi akarejeshewa ubunge wake leo ashindwe kuishi Nairobi kwa gharama zake binafsi za kula kulala na kusafiri kwenda hospitali? Wala hashindwi! Yule kule Nairobi anaishi kwa gharama zake na vilevile mchango anatoa. Msigwa yeye alikuwa miongoni mwa wabunge wawili walioondoka na mgonjwa na hawezi kurudi yeye wala Mbowe mbali na kwamba wanatumia gharama zao binafsi.

Mimi mwenyewe naelekea huko na sitashindwa kuishi kule hata kwa mwezi mzima kwa gharama zangu na michango ya matibabu naenda kutoa. Roho ndogo kama hiyo muachie Magufuli mkuu, wewe hutakiwi kuwa nayo!
Msamehe bure mkuu maana wengine hapa ndio wanatafutia Kiki kupata udc
 
Najua hashindwi wala sijasema anashindwa lakini juhudi na upendo wake umedhihirika katika anga la Tanzania lakini kwanini asirejee nyumbani na hizo fedha akaziwekeza katika kuokoa maisha ya Lissu? Huoni kama atakuwa amefanya kitu Positive zaidi?
Sijui ni busara kumpangia mtu matumizi ya pesa zake,mhe zitto,mhe nyalandu ambaye amerudi kwa mara ya pili na wengine wengi wanaoenda huko kwa nini nao usiwajumuishe katika hili la kupunguza gharama na pesa zao zitumike kama mchango
 
Najua sio masikini lakini kwanini hizo fedha wasichangie kwenye matibabu kuliko kukaa huko Nairobi bila sababu ya msingi?
Mbona hukuuliza michango ya tetemeko huko bukoba ilenda wapi?ebu tutolee akili za kishirikina weww
 
Kuna mtu kaingia madarakani akiwa na moyo wa chuki na kinyongo na ameambukiza ugonjwa huo wengi katika chama chake. Mmegoma kumgharamia, watu wenye mapenzi mema wameamua kujichanga kidogo kidogo walicho nacho na bado hata michango yao nayo mnataka kuhoji?
 
Sasa unataka mgonjwa aachwe kule Hospital mwenyewe ili kuokoa gharama? Mkuu naona unashindwa kujua umuhimu wa uwepo wa watu karibu na mgonjwa! Kumbuka kuwa Lissu alishambuliwa na wanaosadikiwa kuwa ni wa mhimili mrefu hivyo ni lazima kuhakikisha kuwa kunakuwepo na ukaribu wa watu wanaoweza kujitoa pale patakapokuwa na hatari! Lissu bado hayuko salama mkuu. Twende zetu Nairobi tukampe faraja mzalendo wetu wasiye mnafiki na asiye na chuki wala roho ndogo kama ya "Bwana yule"
Wanataka Lissu abakie pekee yake ili lile neno litimie
 
Anae hoji kuhusu Lema na Msigwa,kuishi Nairobi,huwenda ni sehemu ya wauwaji:kwahiyo uwepo wa Lema na Msigwa Kyle Nairobi kunampa wakati mgumu kwenda kumalizia misheni yao,tusiipuzie

Sent from my itel S11 using JamiiForums mobile app
 
Kwani wakiwa kwao wanatumia pesa za nani? Na unasema nairobi maisha ni ghali kwani kula ya cku moja ni kiasi gani? Ach ubwege wewe unatakiwa upambane na hali yko mkuu
 
Habari Wanajamvi,

Kwanza natanguliza pole na kumtakia mema Kamanda wetu Tundu Lissu. Lakini najaribu kufikiri kwanini Msigwa na Lema bado wako Nairobi?

Kwa gharama za nani? Kama za kwao kwanini wasirudi nyumbani kisha hizo fedha wachangie kwenye matibabu?

Wewe ni nani hata uwapangie matumizi! Hela ni yao waache watumie watakavyo.
 
Mkuu ngoja kwanza Lissu apone halafu haya mengine yote tutajua tu, kama wanatumia michango yetu au hela za chama au za kwao binafsi itajulikana tu
Then ukishajua ndo utachukua hatua gani wakati fedha zitakuwa zishateketea! Prevention is better the cure
 
Baasi kwa taarifa yetu tu huyu Mbowe anakuja hapa Hai kilimanjaro na kurudi Nairobi karibia kila siku na safari ya hapa kilimanjaro to Nairobi ni kama masaa matatu tu
 
Huo ndio mchango wako kwenye mjadala?Nani anayegharamia sasa?hebu jibu wewe ******!
8d269d8477ece6e56be87a22b1c45632.jpg
 
Hivi kweli umeshindwa kutumia akili kujua kwamba wale walioko kule ni wabunge na mshahara wao wa mwezi unatosha kuishi kule wao na familia zao?


Sent from my GT-I9505 using JamiiForums mobile app
Nimetumia akili nikaona ni vyema wangeitumia hiyo mishahara yao kuchangia matibabu na si kushinda wakipuyanga huko Ughaibuni
 
Baasi kwa taarifa yetu tu huyu Mbowe anakuja hapa Hai kilimanjaro na kurudi Nairobi karibia kila siku na safari ya hapa kilimanjaro to Nairobi ni kama masaa matatu tu

Hizo gharama za safari zingesaidia kupunguza mzigo wa gharama za matibabu
 
Then ukishajua ndo utachukua hatua gani wakati fedha zitakuwa zishateketea! Prevention is better the cure
Kwani hata sasa hivi wewe unaweza kuzuia kama wanatumia fedha ulizochanga?

Watu wanachanga kwa ajili ya mgonjwa na kama wakija na mchanganuo usieleweka then wafuasi wataelewa wana viongozi wa namna gani. Kama ambovyotulielewa Bukoba. Ikitokea tatizo siku nyingine twaweza tumia mfumo mwingine wa kuchanga.

Ila kwa sasa tusubiri mgonjwa apone kwanza.
 
Lissu hawezi kufanya kitu chochote kwa kutumia mikono yake na hata miguu yake hivyo basi watu waliopo huko Nairobi wanasaidia yeye kufanya chochote anachohitaji kifanyike kwa wakati so ukitaka apewe hela tu na kuondoka basi msaada wako utakuwa ni bure kabisa. Hongera wote waliojitoa kumsaidia Lissu pale Hospitali MUNGU awabariki sana kwa wema wenu na upendo wote mliouonesha kwa watanzania wenzenu kwa ndugu yetu Lissu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom