Nani anafaa kushika dodoki kumsafisha Lowassa ndani ya CHADEMA na wananchi wakamwelewa?

lizon

Senior Member
Jul 29, 2015
126
89
Ndugu Watanzania wenzangu, kwa takribani miaka kumi sasa tumeshuhudia vyama vya upinzani hususani CHADEMA wakitumia muda wao mwingi na rasilimali nyingi kupambana na ufisadi hapa nchini Tanzania.

Wamezunguka nchi nzima wakiwahubiri watu juu ya adhma yao hiyo nzuri ya kupambana na mafisadi.
Wametumia kila aina ya operation na mikutano kuwaaminisha Watanzania kuwa wao na ufisadi ni sawa na paka na panya. Bungeni wamekuwa vinara wakufichua mafisadi na hata kushinikiza wawajibishwe.

Wamekuwa na ujasiri mpaka wakuwataja baadhi ya mafisadi papa hapa nchini (rejea list of shame2007 by Dr. Slaa).

Edward Ngoyaye Lowassa ni miongoni mwa Watanzania waliokuwa wakitajwa kwa kina na upana sana na upinzani kama nguli wa ufisadi nchini Tanzania (rejea mikutano mbalimbali ya chadema). Wakathubutu kusema kuwa hakupaswa kuwa uraiani saizi bali jela au amenyongwa kabsa. Wakailaumu serikali kuwa inalinda wezi na mafisadi.

Watanzania tukawaamini Chadema, tukaamini kuwa Chadema wana nia ya dhati ya kupambana na ufisadi, tukawashangilia kila kona, tukaamini kuwa watatuletea mabadiliko, mabadiliko yaliyoshindwa kuletwa na CCM.

Katika harakati zote hizi, Chadema walikuwa pamoja, viongozi wote mpaka na wanachama, wakipinga ufisadi na udhalimu wa CCM.

Leo wamebadilika, yule mtu waliyekuwa wakimsema na kumtaja kwa kina na upana kabsa kuwa fisadi nguli na hatari Tanzania wamemkarbisha kwenye chama chao, tena akiwa na siku mbili tu wakampa nafasi ya kugombea urais, tena bila kupingwa, pasipo hata kumchunguza. "Samaki na ndege leo wameoana sijui wataishi wapi". Sasa nauliza swali...

NANI ANAFAA KUSHIKA DODOKI KUMSAFISHA LOWASSA CHADEMA WATANZANIA WAELEWE?

BY
SOLOMON
 
Mbona aliisha safishwa ndani ya mkutano wa NEC wa CCM baada ya kuimba ule wimbo wa:
"Tunaimaani na Lowaaasaa hoyaaa hoyaaa"
Kwani baada ya wimbo huo wananchi nao kwa umoja wao wanaendeleza wimbo huo
"Tunaa imaani na Lowaaasaa hoyaaaa hoyaaaaa"
 
mtoa mada lowasa kanunua chama cha chadema akina mbowe vibaraka na wasiwasi lowasa katumwa na ccm kuimaliza chadema
 
lizon

hawana ushaidi kama kweli fisadi ndio maana wamemkalibisha.
 
Last edited by a moderator:
...hatuhitaji dodoki, nape apelekewe jiwe ka kumsugua na waliomtuma kumchafua Rais wetu lowasa...

Panya akingia kwenye mtungi wa maji...huvunji mtungi kumtoa...unainamisha MTUNGI taratibu akitoka unakata kichwa --- Nape .....done done done done Panya keshakatwa kichwa......
 
Ndivyo mañana wana ccm wakamkata hatuna Haja nae ni uhuni kuwawaona wanaonchi woote niviziwi
 
Wewe ndugu usipotoshe hii nchi si ya ccm hii nchi ni ya Watanzania so mtu yeyote awe FISADI awe MWIZI awe MCHAWI, kama ni mchapa kazi we dont care sio ccm iliyojaa mafisadi NCHI Nzima ufisadi kila kona sasa basi muhimu hapo tunataka mtu mchapa kazi atakae wadhibiti mafisadi wasiwe wengi sana. N a ni LOWASA pekee ataiweza hiyo kazi maana anajua mbinu zote na pia pesa anayo yeye nia yake nikusaidia kuweka nchi sawa mabadiliko.
 
Mkuu nadhani 10B alizobeba Mbowe awajibike mwenyewe kununua sabuni na kumsafisha el.

Bilioni kumi wakati anapewa mbowe takukuru walikuwa wapi ? Na zilipitia benki gani ccm mpaka leo ikaiacha salama hembu acheni kulishwa maneno.
 
Endeleeni na ujinga wenu hivyohivyo wenzenu walimuona Lowassa ni tishio kwao na endapo CCM wangemfanya kuwa mgombea wao hakuna mpinzani ambaye angeweza kufurukuta.

Wapinzani walichokifanya ni kuwachomekia CCM kuwa mtu wao ambaye wanakusudia kuwa mgombea wao ni fisadi,mwizi na mtoa rushwa,CCM bila hata ya kutumia akili wamejikuta wamewekwa kati na wapinzani baada ya kutetemeshwa na wapinzani,wamemtosa mtu wao ambaye angewafanya wakapata ushindi wa kishindo.

Sasa wapinzani wamemchukua mtu ambaye alikuwa tishio kwao,hakuna cha ufisadi wala cha mama yake na fisadi,hata CCM wenyewe wanajua kuwa Lowassa siyo fisadi ndio maana hawakumpeleka mahakamani na hawajahi kusema popote pale kuwa Lowassa ni fisadi tangu akiwa mwanachama wao,tunachosubiri ni CCM wawaeleze watanzania kama Lowassa alikuwa fisadi ni kwa nini hawakumpeleka mahakamani?Je Lowassa amekuwa fisadi baada ya kuhamia upinzani?.

Zaidi ya hapo CCM waendelee kutia maji pengine yatawasaidia kuwapunguzia maumivu pindi Lowassa atakapo anza kuwanyoa,safari hii hakuna cha kunyolea mkasi ni mwendo wa kunyolea chupa tena chupa yenyewe ni butu.
 
Hiv hwa wanaoshupalia lowasa ni fisadi ni kina nan?? Ccm hakuna msafi wote wachafu mgombea..wao makufuli mchafi ,ila lowasa juz kaweka wazi , mkataba wa richmond alitaka uvunjwe ila mwenye kaya akagoma kabisa.......njoo na cd nyingine hiyo imesha chja......
 
lizon

Ni afadhali kumsafisha Lowasa kamaa Lowasa kuliko kuisafisha ccm yote maana ni kazi kuisafisha ccm nzima kuliko mtu mmoja.
 
Last edited by a moderator:
Nimevunjwa moyo na siasa za bongo kutufanya mazuzu tusiokumbuka chochote nakutugeuzia maneno kila uchwao,
 
  • Thanks
Reactions: nao
Back
Top Bottom