Upekuzi101
JF-Expert Member
- Aug 28, 2020
- 477
- 1,017
Kwenye nchi ni lazima kuwe na watu ambao hata sisi tukipotoka wote bado wao watabaki kuwa tumaini letu kwa mawazo, ushauri, miongozo na kufanya maamuzi magumu kwa maslahi ya taifa. Maslahi ya taifa siku zote hushinda maslahi binafsi hivyo hivyo tunatambua kipi ni sahihi kwa kufanyika kwa sasa.
Kuna watu wamekaa na kujiaminisha kuwa wakimleta NCHIMBI eti anaweza kubadili hisia na mawazo kuhusu CCM na kukamata hisia za wananchi ila kiukweli watu Wana Imani na Makonda au hata Polepole kuliko huyu balozi ambaye kila mtu anamjua vizuri tangu zamani kwaiyo kwa karata hii you are doomed to fail, fikirieni tena.
Kosa lingine ni kuwa CCM inaenda kurudisha wazee, waliokwisha kutumikia hizi nafasi na wengine walishindwa hata kuleta maendeleo kwenye majimbo yao ila bila aibu na kwakua CCM ni shamba la bibi hata wale nyani wa zamani wanataka kurudi tena kula mahindi kwakua wanajua bibi kazeeka zaidi hawezi hata kurusha jiwe. Hii ni dharau kwa chama na wajumbe mkiwarudisha hawa ng'ombe wazee wenye uchu na madaraka mtafeli vibaya.
CCM cha maana mtakachofanya ni kuhakikisha damu changa ndo inapitishwa at least watakuwa na ushawishi kwa Gen Z hata kama hawatapigiwa kura za ushindi na wananchi lakini mtakuwa mmetengeneza muonekano mpya wa chama kwa kupumzisha wazee na vijana kushika hatamu. Wazee mmetutoa mbali ila hapa tulipofika inatosha mkitaka kuendelea hiyo ni tamaa na mtaongeza mpasuko mkubwa ndani ya chama ukizingatia hata ndani ya CCM vijana ndo wengi zaidi na ndo walitaka kura zipigwe kumchagua mgombea urais baada ya Kikwete kumpitisha mama peke yake bila makubaliano na wanachama wote.
Mzee wetu Kikwete naye ni Mzee wa mjini tu, mpaka leo anapambaniaga maslahi binafsi tu. Wazee wenye hekima tunawaona wakisimamia ukweli ni Warioba na Mzee Butiku. Rais mstaafu Hana cha kupoteza hasa anapoamua kuliponya taifa kwa ushauri, na msaada pale unapohitajika ila kuwa chawa, kushindwa kusema ukweli, na kujikosha ni fedheha kwa nchi kwa familia na taifa kwa ujumla ukizingatia JK analipwa, mwanae analipwa na mke wake analipwa.
Ifike mahali wazee warudiwe na hekima zao watoe muongozo kwa vijana na vijana watumie nguvu zao kuliongoza taifa ila wazee waking'ang'ania madaraka basi vijana wapo huru kuwatoa kwa nguvu hata kuwapumzisha kabla ya wakati