Nani Ana Haki Hapa?

Stevemike

Senior Member
Mar 12, 2011
117
15
Waumimi wa dhehebu A(jina limehifadhiwa) walijenga jengo la ibada kwenye kiwanja cha mmoja wa waumini. imefikia hatua wameamua wote kuhamia dhehebu (b) akiwemo na mwenye kiwanja.

Viongozi wa juu wa dhehebu (a) wanadai kama wamebadili dhehebu watoke kwenye jengo hilo maana ni mali ya dhehebu (a). waumini wamegoma wakidai dhehebu (a) hawana haki na jengo hilo. nani ana haki na jengo hili kisheria?
 
Kwanza inabidi tujue hilo dhehebu a lilifanya transfer of title kama walifanya basi huyo muumini aliyetoa eneo anachake ila kama hilo dhehebu a alikufanya transfer dhehebu imekula kwao
 
Kwanza inabidi tujue hilo dhehebu a lilifanya transfer of title kama walifanya basi huyo muumini aliyetoa eneo anachake ila kama hilo dhehebu a alikufanya transfer dhehebu imekula kwao

dhehebu a hawakufanya lolote. muumini mwenye kiwanja ndiye ana hata ya kijiji inayomtaja yeye na sio dhehebu a. viongozi wa dhehebu a hawana document yoyote kuhusiana na eneo hilo. je, dhehebu a wana haki kisheria kudai jengo hilo?
 
maana ya ardhi kwa mujibu wa sheria ya ardhi ya mwaka 1999 hususani katka kifungu cha pili pamoja na ile shelia ya ardhi ya vijiji zinasema ardhi ni jumla ya tabaka la juu la udogongo na vitu vyote vilivomo nani na juu yake hutegemea na kiwango cha kujishikiza kwa vitu vilivyopo juu yake mjumuiko huusishi madini,gesi na mafuta. Kwa
maana hyo mmiliki halali aliye na hati halali ndo mmiliki halali wa hcho kiwanja na kilichopo juu yake na kutokana na hakuna transaction yeyote iliyofanyika kati ya mmiliki na hayo makanisa kama sija kosea kwenye kesi ya metsula nyagaswa mahakama iliamua kwamba haiwezi kumlamisha mmiliki wa kiwanja kununua nyumba hliyo jengwa kimakosa na mtu ambaye sio mmiliki wa kiwanja kwa hyo ko kanisa A imekula kwao au watalazimika kuondoa hl6 kanisa
 
Kwa hiyo ndugu fugees, waumini hawa wana uwezo wa kufanya ibada kwenye jengo hili maadam mwenye kiwanja hana shida nao chini ya dhehebu b bila kubugudhiwa na na uongozi wa juu wa dhehebu a?
 
Kwa hiyo ndugu fugees, waumini hawa wana uwezo wa kufanya ibada kwenye jengo hili maadam mwenye kiwanja hana shida nao chini ya dhehebu b bila kubugudhiwa na na uongozi wa juu wa dhehebu a?

endapo kama wanakataa kuondoa kanisa lao.kwa mana kwamba wao cio kama waliojenga wataomba wapshe au kuondoa kanisa ila kama hawatak wanahaki ya fufanya ibada
 
Jamani Hata mungu wao ameshindwa kuwaamua ? kwa maana mwananchi akiwa na tatizo kama hilo wanamwambia njoo kanisani kwetu uombewe sasa inakuwaje wanarumbana?

tukirudi kwenye swali mimi nadhani mambo mengi yanafanywa na wananchi mitaani bila kutumia taratibu za kisheria lakini wakati wananchi hawa wanafanya mambo haya huwa wanaweka maandishi ya kumbukumbu juu ya kile kinachofanyika hivyo kama walifanya mikutano au vikao ambavyo wanakumbukumbu zake zinaweza kusaidia kuonyesha walichokubaliana na kina nani walishiriki.

kwa haraka inaonekana kanisa ni mali ya dehehebu A kwa maana michango na kiwanja walivyovitoa hawa watu zilikuwa ni sadaka kwa kanisa na walipoteza umiliki wake tu pale walipoamua kuvitoa kusaidia kanisa.

hakuna mtu anayehama kutoka katika dhehebu alafu akadai kurudishiwa sadaka zake zote alizowahi kutoa katika kanisa hilo.

lakini hilo linaweza kubadilika iwapo waumini hawa "wote" waliohusika katika ujenzi wa kanisa hili wanaamua kuhama kwa maana ni sawa na kanisa zima kuamua kubadili jina la kanisa lao je wanapoteza umiliki wa mali walizokuwa nazo au na mali zinahamia katika jina hilo la pili?

maana yake ni kuwa kama waumini hawa walijenga kanisa hili ili wapate mahali pa kuendeshea ibada yao lakini baada ya kuomba sana wakaona hawapati majibu wakaamua kubadili dhehebu kwa lengo lilelile la kuboresha ibada yao basi nadhani kanisa ni mali yao huko walikokwenda. bado katika mtizamo huu wa pili kama kuna muumini yeyote ambaye amebaki katika hilo kanisa bila kuhama basi kanisa linabaki A.

ila hivi makanisa haya yanaanzishwa kwa kutumia katiba na kama katiba ya kanisa A ipo basi hiyo inaweza kuwa na jibu la kitendawili hiki.

reference ni "thumb rule"

Waumimi wa dhehebu A(jina limehifadhiwa) walijenga jengo la ibada kwenye kiwanja cha mmoja wa waumini. imefikia hatua wameamua wote kuhamia dhehebu (b) akiwemo na mwenye kiwanja.

Viongozi wa juu wa dhehebu (a) wanadai kama wamebadili dhehebu watoke kwenye jengo hilo maana ni mali ya dhehebu (a). waumini wamegoma wakidai dhehebu (a) hawana haki na jengo hilo. nani ana haki na jengo hili kisheria?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom