kakuruvi
JF-Expert Member
- Sep 2, 2009
- 770
- 259
Mwisho wa wiki iliyopita nilisafiri nje ya Dar na kwenda vijijini huko Korogwe, kuna mahali tulifika nikajisikia kula muwa. Basi tulisimama barabarani karibu na daraja moja la mto Rwengela kwenye mashamba ya mkonge Magoma Estate.
Wakaja vijana tukawaagiza miwa kwani hapo ndio mashambani kwao, waliporudi walionekana kwenye malumbano fulani, hatukujua mpaka tulipowauliza kulikoni? Kumbe walipoondoka walijihisi haja kubwa wote kwa pamoja, mmoja akajisaidia mtoni, mwengine pembeni ya mto.
Ubishi ulikuwa, mmoja anamlaumu mwenzake kwa kujisaidia pembeni ya mto kwani atawatesa wote watakaopita pale kwa harufu ya kinyesi, mwingine anamlaumu mwenzake kwa kujisaidia mtoni kwa kuwa atawalisha uchafu wote wanaotegemea maji ya mto huo huko kote utakakopita.
Wana JF tuambie madhara yatakayosababishwa na mazingira ya uchafu wa kila mmoja, nani ana afadhali kati ya hawa wawili?