Nani amemroga Profesa Palamagamba Kabudi?

Nani amemroga Profesa Palamagamba Kabudi?

AMARIDONG

JF-Expert Member
Joined
Jun 24, 2010
Posts
2,501
Reaction score
189
Alipoingia kwa mara ya kwanza darasani kunifundisa Family Law niliamini kweli niko chuo kikuu na ninafundishwa na GURU mwenye uwezo mkubwa, na baada ya kufundishwa nae kwa muda mrefu sikuamini kama kuna mtu Tanzania ambaye anaweza kuwa na uwezo mkubwa katika maswala ya sheria za familia kwa wakati ule zaidi yake.

Naikumbuka sauti yake kali na maelezo yake yasiyobabisha nakumbuka pia wanafunzi wengi waliopendelea kukaa viti vya mbele walilalamika kuwa Palmagamba alikuwa ananyesha sana, yaani akiongea anatoa mate huku na huku hilo sikulishuhudia kwani nilikuwa napendelea kukaa nyuma kama ilivyo mila yetu kuwa kijana wa kichaga unakaa nyuma ya familia ili kuilinda na kuhakikisha familia inakuwa salama sio uhuni kukaa backbencha.Siamini mtu mahiri ambaye mara zote darasani aliiponda serikali na kuwaponda watendaji wake

Mwalimu ambaye hakuna hata siku moja laiyowahi kusema zuri juu ya serikali na katiba yake,kila siku akijadili katiba alionyesha mapungufu makubwa juu ya katiba iweje leo ausifie mswada mbovu LAZIMA AMELOGWA na huku ni kulogwa kwa kununuliwa na SHILINGI.

Alipoingia kwenye siasa za kinafki na kuanza kuchambua hoja ya mgombea binafsi kinafki bila kusema ukweli kwa wananchi niligundua kuwa mwalimu wangu sasa ana njaa ,na ameamua kutafuta umaarufu mwingine zaidi ya ule uliotukuka aliokuwa nao.Nilifikiri labda anajiandaa kugombea ubunge sehemu fulani au ameahidiwa Uanasheria mkuu.

Wiki iliyopita nilishangaa sana kumuona mwalimu huyu wa Family law akiungana na adui yake mkubwa Jaji wa zamani wa mahakama Kuu kitengo cha biashara kwa kuteatea mswada mbovu wa katiba unaopelekwa bungeni kwa nguvu ya mafisadi na serikali isiyosikiliza maoni na matakwa ya watu waliowapeleka madarakani,""hii si sawa na ni lazima itambulike kuwa wanasiasa nyie ni watanzania pia na huu mswada unawahusu zaidi nyie"" Haya ni baadhi ya manene yaliyomtoka Guru wa sheria za kifamilia na kunifanyua nijiulize ni nani aliyemloga Guru huyu??

Naomba kumshauri mwalimu wangu kuwa kwa sasa amebaki peke yake mtaalamu na msomi anayeitetea CCM,aangalie sana isije ikawa mwaisho wa wema wake unafikia kuwa mwanzo wa ubaya wake.

Mabadiliko tunayoyataka ni lazima yaje kwa nguvu au kwa hiari Mkapa alisema HAKI HAIOMBWI INADAIWA NA IKISHINDIKANA INAPIGANIWA, tutaidai haki yetu hata kwa kuipigania.
 
umesahau watu wanauzwa na kununuliwa pia? (sio miili tu mpaka na fikra zao)
 
...........toka alipoungana na serikali kupoka haki ya uraia wa mtanzania (ugombea binafsi) na kwenda kinyume na mawazo ya baba wa Taifa kuhusu haki ya uraia ambayo ni haki ya kuchagua na kuchaguliwa, nilijua kuna kitu kimemtokea Prof. lakini sijui ni kitu gani, ni suala la wakati tu.
 
Prof. Palamagamba kabudi

images


Hii ndo SOurce ya NENO GAMBA
 
Mkuu huyu jamaa nilikuwa namkubali sana...lakini kwenye semina ya wabunge siku ya Jumamosi lol!! alimwaga uharo mbele ya watu............
 
Huyu Profesa kanisaidia sana Jana, sababu sasa ninaanza kumsikiliza kila professional kwa macho mawili.
1. Professional eye
2. Personal Interest eye.

Huyu Professa, ameweka pembeni kabisa usomi wake na kuangalia maslahi binafsi, ndio maana
sikumsikia akitoa any technical advice zaidi ya siasa mwanzo mwisho.

Kanunuliwa huyu
 
Mtu mwenyewe anaitwa Magamba,ameshanunuliwa huyo,hata siku ile walipompa gamba kikwete aliongea pumba eti kwenye mswada watu wasiongee kuhusu muungano!!anatafuta maslahi AKILI ZA MBAyUWAyU CHANGANYA NA ZAKO
 
PALAMAGAMBA KABUDI alikuwa msomi aliyebobea na alikuwa mbali system pale UDSM, pesa ni kitu kibaya sana, baada ya VC rafiki ya JK kuingia wakaanza kumvuta karibu hadi kapewa ukuu wa kitivo cha SHERIA UDSM. Maoni yake mengi pamoja na yule wa siasa BANA BENSON ni ya wachumia TUMBO fool shame on them.
 
Pesa sabuni ya roho, ila tuendako pesa itakuwa sabuni ya kaburi, wadanganyika wameanza kuamka, mkianza kufikiri kila kitu ni CDM nchi itawashinda, angalieni watu wanataka nini, kama ni CDM nendeni na nyie muanzishe jukwaa la katiba mseme huu mswada safi sana muone moto wake
 
Sikuwa mwanafunzi wa sheria UDSM,lakini kila nilipokuwa namwona prof Kabudi akichambua mada za kisheria, nilimkubali sana. Imani yangu kwake ilinitoka baada ya kutoa ushauri wa ajabu akiwa rafiki wa mahakama katika kesi ya mgombea binafsi. Nafikiri bila ushauri ule sasa hivi tungekuwa na mgombea binafsi.
 
Back
Top Bottom