Nani amemdanganya Mkuu wa Kaya?

Kwa nyingeza kuna gharama ambazo ni lazima (fixed costs) ndege imepaa au la! Ndege imejaza abiria na mizigo au la!

Ati unanua roli na mtoto wake (tani 40) kubeba tani 5 ambazo zingebebwa na canter! Uchumi gani huo! Mtoa mada akajifunze uchumi kwanza "economies of scale"!
 
Mkuu,

1) Ikitokea tuseme kuna demand ya abiria labda 200 tu wa kwenda songea kwa Muda huo uliozungumzia huoni kama hesabu zako zitakinzana??
Manake Bombardier itahitajika kwenda trip mbili labda kwa mafuta ya hiyo 4mil total wakati Boeing mwendo ni uleule wa afuta ya 6mil (kwenda tu)??

2) Kama umeweza kufanya upembuzi ukagundua Si kweli kua Boeing inagharimu Over 26Mil bali only 6mil, mbona hukufanya upebuzi huohuo kwenye mafuta ya Bombardier? Huoni kama inawezekana aliedanganya kwenye mafuta ya Boeing atakua amedanganya pia kwenye mafuta ya Bombardier?? Huoni kama inawezekana hata hiyo 1mil per trip inaweza kua kubwa nayo kama ilivyokuzwa ile ya Boeing??
 
Yes Mkuu, na kwa kuwa hii aliyofanya ni comparative analysis, under ceteris peribus, basi hakutakuwa kutoa conclusion kwa derivative ya comsuption kwa boing against number of trips kwa bombardier, alitakiwa aweke analysis ya consumption ya hayo mapanga boi kwanza ndipo ajenge base ya hitimisho. Kifupi kafanya kazi nusu, kahukumu bila kumpa mshtakiwa wasaa wa kujitetea. Pangu Pakavu.
 
Mimi nadhani uamuzi wa kununua ndege ndogo kwa matumizi ya ndani, ni uamuzi sahihi kwa wakati huu kwa sababu kwa sasa watumiaji wa usafiri wa ndege ni wachache.

Lakini pia siyo kweli kwamba Dash 8 Q400 ndiyo ndege bora kuliko nyingine zote kwa mazingira ya aina zote. Kusema kuwa Q400 inatumia mafuta kidogo kuliko ndege nyingine zote nao ni uwongo pia. Matumizi ya mafuta kwa ndege hupimwa kwa kuangalia wastani wa matumizi ya mafuta kwa abiria mmoja kwa kilometa 100. Na kwenye kipimo hicho mpaka sasa Q400 is not the best.

Hapo unaongelea matumizi ya mafuta. Na matumizi ya mafuta siyo yanayoweza kulihakikishia shirika kupata faida. Faida hutegemea zaidi efficiency ya shirika.

Ni efficiency pekee ndiyo itakayolifanya ATCL isonge mbele au ianguke, wala siyo kiasi cha mafuta ndege zinachotumia au upya wa ndege tulizo nazo.
 
Hivi alichokisema raisi kuwa, bomberdia inatumia mafuta ya ml.1 mpaka songea ni kweli?
 
hii picha ina inazungumza mengi mambo si mambo umejifunza nini hapa.
View attachment 410241
swissme
Mkuu....
Hivi unayo hiyo milioni 7?
Yaani ukisoma hoja ya swali la mleta uzi ni kwamba.. NANI ANAMDANGANYA MKUU WA KAYA?
Alafu wewe ulipo weka picha ya Waziri mkuu na Mkuu wa kaya, maana yake ni kwamba huyo ndie anae mdanganya...[emoji15] [emoji15] [emoji15]
Ebu ngoja niishie hapa kwanza
[emoji124] [emoji124] [emoji124] [emoji124] [emoji124]
 
Hapa nazungumzia abiria 450 waliopo Dar na wanaenda Songea
 
Am much better, ndiyo maana nimeweka na link hapo ili udukue zaidi.
 
Kwani jamaa huwa anasikia la kuambiwa au kajidanganya yeye mwenyewe ?
 
we subiri atumbuliwe jicho maaana watamstukia tyuu TRA wa miaka hiii sio wa zama zileeeeeeeeee
 
Sasa mkuu abiria 450 wa kwenda songea siku moja unawatoa wapi?
Huko nyie mabasi tu yanawatosha.
 
Hoja yako inaweza kuwa na substance. Lakini jee tunao abiria 450 wa kupanda Boeing 777 kwenda Songea Kwa wakati mmoja? Nadhani walimshauri Mkuu wa Kaya waliangalia vigezo kadhaa ikiwemo ulichokijengea hoja.
Abiria 75 wa DAR - SONGEA pia itakuwa ni shida kuwapata.
 
Hoja hujibiwa kwa hoja, sio vioja. Njoo na mathrmatical formula ku prove kwamba fastjet inatumia mafuta ya milioni 28 kwenda Mwanza.
 
Mkuu umefanya analysis nzuri lakini hukumalizia ndio maana utapata critism nyingi. ungefanya kitu kimoja ungekata mzizi wa fitna

moja ungeafanya cost analysis kwa abiria mmoja ndege ikiwa imejaa (fully capacity), ikiwa na abiria (50% capacity) na ikiwa na abiria 25% inakuaje. hii itamaliza kabisa fitna yeyote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…