Nani aliwaloga wajita??

Majita

JF-Expert Member
Jan 13, 2008
609
190
Ni kama utani fulani hivi ninapoandika habari hii.Lakini baada ya fujo na vurugu za jana kwenye uchaguzi wa UVCCMAGAMBA nimefualitia kwa karibu sababu ya kuanza kwa makonde ya vijana hao.Wachangiaji wengi wanaonyesha "ulalafu" wa hawa wajita katika mkoa wao.Wachangiaji Wako sawasawa kabisa.Mie najiuliza swali nani kawaloga wajita au who bewitched the "yegos".
 
bado hawajazinduka usingizini,wako karne ya 5.na usiombe ukuta na trafiki mjita atakuuliza mpa kitambulisho cha kupigi kura.
 
SIdhani kama ni tatizo la Wajita, tatizo la CCM na utamaduni wa posho-rushwa za ki-Nape Nape. Mbona sijasikia wapigane kugombania SADAKA?
 
Kuna mila zinaona mwanaume kupigana ni sifa usikute na wenyewe wamo
 
Mimi ni Mjita tatizo letu nini kwani mbona hamtuambiee tujue.
Naomba nijue kwani tuhuma hizi za jumla jumla si nzuri.
Kabla sijaenda mbali ebu nijulishe tatizo letu wajita.. Baadae tuingie kwenye reality tuzingatie Integrity na mambo kama hayo..
 
WAjita wanalalamikia umiliki wa vyeo na madaraka yote mkoa ule kuchukuliwa na Wakurya na jamii nyingine zinazoelewana nao. Vyeo vyote vya kuchaguliwa pale mkoani vya kiserikali na ki-CCM vimekamatwa na Wakurya na jamii zao. Hakuna Mbunge Mjita; hakuna mwenyekiti wa CCM, UVCCM, UWT, TAPA, wa Mkoa ambaye ni Mjita. Kumbuka Wajita pia ndio jamii yenye watu wengi pale Mara ikizidiwa kidogo sana na Wakurya.

Njia kuu na nguvu kubwa za kiuchumi pia zinamilikiwa na Wakurya na jamii zao pale mkoani na wilaya zote.
 
N .Wachangiaji wengi wanaonyesha "ulalafu" wa hawa wajita katika mkoa wao.Wachangiaji Wako sawasawa kabisa.Mie najiuliza swali nani kawaloga wajita au who bewitched the "yegos".

Usiwaonee Wajita. Mkoa wa Mara una makabila mengi sana. Kuna Waruri, Wakwaya, Wasimbiti, Waisenye, Wakiroba, Wasweta, Wajaluo, Wakurya, Wazanaki, Waikoma, Wangoreme, Waisenye, Wajita na wengineo. Ajabu na Wajita tu wanaotuhumiwa kwa rabsha hizi. Kulikoni?
 
Basi nimejua tatizo, Kwa taarifa yako usiwalinganishe wajita na Wazalamo ni kosa kubwa sana. Mimi sio CCM ila ni Mjita kwa kitendo cha Wajita kujitambua inaonyesha mwisho wa siasa za Rushwa na Ukabila. Mambo yamebadilika watu wameelimika na Uelewa ni mkubwa kwa kuwa wamelitambua hilo wakiacha CCM watafute sehemu itakayowafaa. Haina maana kupigania vyeo kwenye chama ambacho Wajita wanajua hawatapata uongozi. Na Uongozi kwa Mkoa wa Mara ndo sehemu ya Maendeleo. Sasa basi CCM si Mama ya WAJITA ni muda Muafaka wakiame chama hicho na kutafuta mmbadala.
NINACHOPINGA NI SWALA LA KULINGANISHA WAJITA NA WAZALAMO, HAPANA TUWATENDEE HAKI KWANI KUTOPENDA KUFANYA FUJO SI UDHAIFU BALI NI UUNGWANA.
 
mie mjita niwe mzalamo wa Musoma , Hii sio sawa!!. Wajita sio wanasiasa bali watendaji kwa mtazamo wangu.
 
Usiwaonee Wajita. Mkoa wa Mara una makabila mengi sana. Kuna Waruri, Wakwaya, Wasimbiti, Waisenye, Wakiroba, Wasweta, Wajaluo, Wakurya, Wazanaki, Waikoma, Wangoreme, Waisenye, Wajita na wengineo. Ajabu na Wajita tu wanaotuhumiwa kwa rabsha hizi. Kulikoni?
Kwangu mimi niliyekaa sana kule Mara ungeniuliza ningekwambia MAKABILA halisi ya Mkoa ule ni matatu tu. mengine haya ni koo tu za makabila hayo matatu:
-WAKURYA, humo utawakuta Wazanaki, Wangoreme, Wasimbete, Waikoma, Wanata, Waisenye, Wakabwa,...;
-WAJITA, humo utawakuta Waruri, Wakwaya, Wakerewe,...;
-WAJALUO.
Wazaramo wa Musoma ni Wakwaya na Waruri kidogo ambao sasa wamenyang'anywa ule mji wa Musoma na Wakurya kama Wazaramo wanavyotimuliwa Dar sasa.
 
Ni kama utani fulani hivi ninapoandika habari hii.Lakini baada ya fujo na vurugu za jana kwenye uchaguzi wa UVCCMAGAMBA nimefualitia kwa karibu sababu ya kuanza kwa makonde ya vijana hao.Wachangiaji wengi wanaonyesha "ulalafu" wa hawa wajita katika mkoa wao.Wachangiaji Wako sawasawa kabisa.Mie najiuliza swali nani kawaloga wajita au who bewitched the "yegos".

Hii ni dharau kubwa mno, kwanamna nyingine ubaguzi wa hali ya juu. hivi Tz bado mnaongelea makabila, no wonder 2015 JK atawachagulia Rais mwingine.
 
Usiwaonee Wajita. Mkoa wa Mara una makabila mengi sana. Kuna Waruri, Wakwaya, Wasimbiti, Waisenye, Wakiroba, Wasweta, Wajaluo, Wakurya, Wazanaki, Waikoma, Wangoreme, Waisenye, Wajita na wengineo. Ajabu na Wajita tu wanaotuhumiwa kwa rabsha hizi. Kulikoni?

Hizo zingine ni koo tu au sub-tribes....in the end kuna WAKURYA, WAJITA, WAJALUO, WAIKIZU na WAZANAKI tu..........kama UCHAGGANI kulivyo na WAROMBO, WAMACHAME nk etc
 
Hii ni changamoto kwa jamii ya Wajita inabidi kuanzia hapa jamii hii ijitathmini.Maana ya Michango iliyotolewa kwenye mada hii ni kiashirio tosha kuwa kuna tatizo ambalo kwa muda mrefu halijawahi kuongelewa.
 
Definetely kuna tatizo ambalo halina nafsi tena kwa WAJITA. NOTE: Kama Udini umepewa kipaombele na UKABILA lazima sasa UTAMALAKI. Waasisi wa haya yote ni CCM na serikali yake na wameshatufikisha pale ambapo hatukutalajia ( UKABILA).
 
WAjita wanalalamikia umiliki wa vyeo na madaraka yote mkoa ule kuchukuliwa na Wakurya na jamii nyingine zinazoelewana nao. Vyeo vyote vya kuchaguliwa pale mkoani vya kiserikali na ki-CCM vimekamatwa na Wakurya na jamii zao. Hakuna Mbunge Mjita;

Ukimtoa Kangi Lugora hakuna mjita mwingine ambae ni mbunge,DC,mkuu wa mkoa,mwenyekiti ktk kada zote kuanzia ngazi ya wilaya,mkoa na Taifa,au niseme kwa cheo cha kuteuliwa.
Mimi hapo real am puzzled.Shida ni nini
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom