Nani aliidhinisha Ujenzi wa Stendi Mpya ya Nyegezi? Viongozi Hawaoni tatizo?

Hii stendi naona watu wanasifia, na kuna wakati Waziri Mkuu alie da kukagua maendeleo ya Ujenzi, Ila tulinyimwa akili au zipo ila Uchwa umetuzidi.

Swali ni Je Hakuna Idara ya Intelijensia ya kuweza kugundua kwamba pale ni uhuni na pesa zimepotea bure na itahitajikantena kuja kujengwa stendi mpya?

Ile Stendi imejengwa katikati ya makazi na ile eneo liko very congestion, ni mara 200 ile stendi ya Nyamhongolo sijui kama nimepatia speling.Il stendi ilipaswa kutafutiwa eneo kubwa sana ambalo lingekuja kuzidiwa baada ya miaka hata 50 na sio hii ya miaka 4

Stendi ya Nyegezi naipa miaka 3 kutoka sasa wataanza kutafuta eneo jingine kwa ajili ya ujenzi wa stendi Mpya, Pale hamna maisha, ni pesa zisha pigwa za ujenzi na wakati wanatafuta eneo jipya wahusika wa sasa watakuwa my be walisha hamishiwa maeneo mengine kuendeleza upigaji.

Cha kustajabisha viongozi hawaoni kabisa kwamba eneo lile ni dogo sana na licha ya udogo ni eneo limejaaa, na lina Jam za kutosha na baada ya miaka minne halitafaaa kabisa itabidi litafutwe eneo jipya.

Hii nchi ni kawaida kufanya mambo kwa projection za miaka 4 tu mbele baada ya hapo tuna vunja au tunabomoa na kujenga tena.

Walio jenga au kuruhusu Ujenzi wa stendi ya Ubungo walipaswa kuwa jela kwa sasa kwa kulisababishia Taifa hasara ya kujenga stendi baada ya Muda inavunjwa inaenda kujengwa kwingine.

Wakati wenzetu Project zao huwa zinaangalia miaka 100 ijayo za kwetu ni miaka 4 ijayo. Na hii iko hadi kwemye Majengo ya Serikali.

Angali Majengo ya shule zinazo jengwa sasa na linganisha na zilizo jengwa na Kanisa au Wakoloni na baadae Nyerere akawanyang'anya kanisa. Shule kama Karatu Secondary wale watu wali project miaka 100 mbele hadi 200.

Angalia sasa shule zetu za kata projectiin ni miaka 3 hadi 4 mbele.
Wewe ni Mmoja wa watu waliodhani stendi itajenga Usagara mkakimbilia kununua viwanja pale. Nyegezi stendi Iko pale hata miaka thelathini ijayo.
 
Wakati wenzetu Project zao huwa zinaangalia miaka 100 ijayo za kwetu ni miaka 4 ijayo. Na hii iko hadi kwemye Majengo ya Serikali.
Mimi sipendi kupingana nawe kuhusu uliyo andika hapa. Ni kwelikabisa eneo ni dogo; lakini udogo ndiyo hoja kuu kweli.
Huwezi kupanua wigo kidogo ukaona hata maendeleo katika ufanisi wa kiteknolojia kuweza kuruhusu udogo huo kwa ufanisi.
Kuna sababu zozote zinazolazimisha, kwa mfano, gari (Bus) likae stendi hapo zaidi ya saa moja nzima kabla halijaondoka na kuacha nafasi kwa wengine?
 
Yupo sahihi sana mleta mada.

Eneo la stand ya Nyegezi ni dogo ssna. Baada ya muda mfupi itabidi ihamishwe tena. Itapelekwa mbali zaidi na mji kuliko kama wakati inajengwa hii, wangetafuta eneo kubwa, labda huko Nyashishi. Miaka 4 baadaye, hata Usagala, hawataweza kupata eneo kubwa.
Kwani standi ya mabasi ni lazima iwe moja? Mji kama huo wa Mwanza, ambako ni kama mwisho wa nchi, wanaweza kuwa na stendi kuu mbili au tatu. Kwa mfano, haiwezekani kujenga stendi nyingine ikitokea maeneo ya barabara iendayo Mara, na kuunganisha stendi hiyo na barabara kuu iendayo Shinyanga na kuelekea Dodoma hadi Dar?

Sijawahi kuona katika miji yote mikubwa duniani yenye stendi yenye eneo kubwa sana. Usafiri wa reli utakapokuwa mzuri, na ndege zikawa nafuu kwa raia wengi, uhitaji wa mabasi utapungua sana. Raia wengi watakuwa pia na usafiri wao binafsi.
Hali hii ya sasa ni mpito tu, mambo yatakuja kubadilika sana muda siyo mrefu, kama Samia na CCM yake hawatatuchelewesha zaidi.

Na zaidi ya yote hayo, picha tunayojengea hoja hapa kuhusu usafiri wa mabasi hautumiki tena sehemu nyingi duniani.
Kampuni ya mabasi, kama 'Greyhound' huwezi kukuta mabasi yake yamerundikana mahali pamoja tu mjini. Haya yana vituo mbalimbali sehemu nyingi ya miji yanapopitia. Hayakai kituoni kwa muda mrefu; yaani ni 'network', yanapokezana wasafiri wanaokwenda sehemu mbali mbali za nchi.
 
Kwani standi ya mabasi ni lazima iwe moja? Mji kama huo wa Mwanza, ambako ni kama mwisho wa nchi, wanaweza kuwa na stendi kuu mbili au tatu. Kwa mfano, haiwezekani kujenga stendi nyingine ikitokea maeneo ya barabara iendayo Mara, na kuunganisha stendi hiyo na barabara kuu iendayo Shinyanga na kuelekea Dodoma hadi Dar?

Sijawahi kuona katika miji yote mikubwa duniani yenye stendi yenye eneo kubwa sana. Usafiri wa reli utakapokuwa mzuri, na ndege zikawa nafuu kwa raia wengi, uhitaji wa mabasi utapungua sana. Raia wengi watakuwa pia na usafiri wao binafsi.
Hali hii ya sasa ni mpito tu, mambo yatakuja kubadilika sana muda siyo mrefu, kama Samia na CCM yake hawatatuchelewesha zaidi.
Umemaliza mkuu
 
Back
Top Bottom