Nani aliidangaya CHADEMA?

Nani aliidangaya CHADEMA?

Hizi propaganda za Johnson Mbwambo ni simulizi nyepesi zisizo na mashiko. Kwanza, kupitia kwa magazeti yake, Mbwambo ana maslahi na CCM hasa hiki kipindi cha kampeni hivyo haishangazi kuwa anapuliza zumari kulingana na matakwa ya mlipaji wake. Hilo liko wazi. Pili, kiuhalisia, Chadema/Ukawa hawajaachana na agenda ya ufisadi (soma Ilani yao!). Tatu, kinachomsumbua Mbwambo (na wenzake) ni hatari ya wazi ya CCM kung'oka katika uchaguzi huu kutokana na Chadema kuachana na siasa nyepesi za kiuanaharakati na kuendesha kampeni yenye dhamira ya kweli ya kuuondoa utawala wa wezi (KLEPTOCRATIC rule) wa CCM madarakani (ambao wananufaika nao). Walichokua daima wanataka ni kuiona Chadema, kama chama kikuu cha upinzani, kinaishia tu kuimba majukwaani: "Ufisadi! Ufisadi!" bila kuwa mkakati wa dhati wa kuing'oa CCM (ambayo ndio mhimili mkuu wa ufisadi) madarakani. Hakika sasa Chadema wameamua. Hawadanganyiki!!

Huyu Mbwambo kama wengi mlivyosoma uzi wake mrefu mtamwelewa ni wazi anakishabikia chama gani na ni kati ya wale wanaosemekana kulipwa kwa kueleweka udhaifu wao. Hawezi kudanganya popote kuwa mgombea wa chadema kwa maana ya ukawa hanadi sera za chama chake kila afanyapo mikutano ya kujinadi. Wote tunaona,kusikia na kusoma pia.Hivyo hivyo hawezi kusema chadema wameachana na kukemea ufisadi na wizi wa hela na rasmali za taifa na lipo pia katika ilani yao aisome na kuacha kuwaaminisha wananchi uongo. Hawezi pia kudai chadema inashabikia ukanda vinginevyo yeye ndie anaefanya hivyo kwani mgombea anaemshabikia wa chama chake wanatoka kanda moja pia. Hatuelezi ni kwa nini mgombea wake anakwepa kujinadi kwa jina la chama chake huku akijua yeye kama yeye hamiliki nchi na ametumwa na chama chenye usajili wa kudumu. Awaeleze watanzania mgombea wao atakavyotekeleza anayowaahidi watanzania ndani ya chama chake kwa mfumo walio nao ambao hana ubavu wa kubadilisha lolote na akabaki salama. Yote anayoeleza majukwaani yanaweza kutekelezwa na chama kilicho nje ya mfumo wao waite wapinzani au kama tungekuwa na mgombea binafsi na sio chama kinachoongoza nchi na serikali kwa sasa yaani ccm. Labda atuambie ccm yake kwa sasa imejiandaaje kulipa IPTL fedha zao kwani toka May mwaka huu wameshaleta barua ya kutaka kulipwa hela za tegeta escrow acc walizogawana eti sio za serikali. Tumeisoma wote humu humu Jf jukwaa hili hili. Naomba wananchi wenye uelewa na wanaotaka maendeleo ya nchi na mwananchi mmoja mmoja wampuuze huyu bwana na ushawishi wake usio na mwelekeo. MABADILIKO UKAWA UKAWA MABADILIKO.
 
Ajabu kweli. Sasa kama mlikuwa mnachukia ufisadi kwa dhati, mbona hamkuisaidia hiyo CHADEMA kwa miaka yote hiyo 20?? Slaa amepiga kelele hamkumuelewa. Ni kinini kingewafanya sasa mumuelewe?? Ni unafiki!!!!!!! Unajifanya unajua mema na mabaya sasa! Hukujua zamani! Ulikuwa mtoto??

Mtu yeyote mwenye akili atabadili mada kama kwa miaka 20 imekuwa kama kumpigia mbuzi gitaa, hakuna anayeelewa somo, mafisadi mwendo mdundo, wanazidi kuchaguliwa alafu wewe unakamia; mafisadi! mafisadi! Mafisadi! Lakini hakuna anayeitika. Busara inaonyesha Mtanzania hashtushwi na ufisadi. In fact, anaupenda ufisadi maana miaka yote wamerudi madarakani! Wa EPA, wa rada, wa Richmond, wa... wooooote wanarudishwa madarakani. Nyoka wooote wa makengeza wanarudi madarakani. Sasa kwa nini unaitaka Chadema ibaki na wimbo huo huo. Watakuwa insane; doing same thing, same way na kutegemea matokeo tofauti!

Na sio kweli kuwa Chadema walifanya vizuri uchaguzi uliopita!! Kwa kashfa kama ya escrow ingekuwa kwa nchi makini ingeangusha serikali. Sasa kwa impact ndogo kivile, hivi unategemea ufisadi upi tena? Kama unategemea mwingine mkubwa, Nakuhakikishia, hutajakaa uone ufisadi mkubwa kuliko ule.

Tena waambie mwenye kampuni yake ya IPTL ameshaitwanga serikali barua toka mwezi wa tano mwaka huu kutaka hela zake na faida zilizokuwa escrow account au awafikishe mahakamani.Zile fedha walimlipa Sigh kwa kuamini documents za kufodge na kisha kuzigawana mafisadi wote wakidai hazina mwenyewe. Kesi hii IPTL wanashinda asubu na mapema na walipwe gharama za kuendesha kesi.Watanzania fumbueni macho mkidanganyika na hadaa za Magufuli majukwaani mtataabika kwa miaka yote kumi atakayoongoza kwani kwa mfumo wa ccm hana ubavu wa kubadili lolote wala kutekeleza anayowaaminisha majukwaani kwa sasa.
 
Ujinga ni mwingi na Mara nyingi mjinga huona karibu nakubali kweli wana ukawa wengi ni watu wenye ufinyo wa mishipa ya kufikiri
 
Kamwe hukuwahi kuipenda na kuiunga CHADEMA ilipokuwa ikiibua hoja za ufisadi; iweje uipende na kuionea huruma ghafla leo inapopambana kuleta mabadiliko tuyatakayo nje ya ccm..??
Kwani CHADEMA ya zamani haikuwa inapambana kuleta mabadiliko?
 
Kura yangu kwa magufuli...wana ukawa lazima wajue kuwa lowassa hakuondoka ccm kwa kuwa ni mbaya. Ni kwa kuwa walimkata tu. Tatizo akili za nyumbu
 
Kinachokupa jeuri ya kuandika hivi ni hizo tafiti uchwara. Ila usisahau goodluck jonathan tafiti zilimpa 70%
Hiyo ni Nigeria brother, siyo tz ,- Tanzania na watanzania wanafahamu nani kiongozi na nani mpiga deal. Tarehe 25 ipo Karibu kura yangu kwa Magufuli mzee wa push up
 
Naiunga Mkono Makala Kwa 100%.Mimi Natamka Wazi Kuwa Lowassa Ni Fisadi Na Hafai Kwenda Ikulu.Mimi Binafsi Yangu Nimeshaamua Kura Yangu Kwa Magufuli.Tunataka Raisi Mchapakazi Sio Mchezadili
#hapakazitu
Plain and simple Lowassa hafai kuwa Rais wa Tanzania.
 
Back
Top Bottom