MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,185
- 24,051
Na mwandishi Johnson Mbwambo
MPAKA sasa kila nikitafakari nashindwa kuelewa nini hasa kilikuwa kinaendelea katika vichwa vya viongozi wa juu wa Chadema hadi kukubaliana kuitosa ajenda ya ufisadi katika uchaguzi mkuu wa safari hii na kumchukua Edward Lowassa kuwa mgombea urais wake.
Mbali ya kumteua Lowassa kuwa mgombea urais wake, Chadema kilikwenda mbali zaidi hivi karibuni kwa kuiondoa kwenye tovuti yake ile orodha yake ya mafisadi papa (list of shame) ambayo huko nyuma kilikuwa kikiitumia kujenga hoja kuwa CCM ni chama cha mafisadi. Kwenye orodha hiyo Lowassa alikuwa Na. 9.
Hatua hiyo ya kuiondoa orodha ya mafisadi papa katika tovuti yake inathibitisha, pasipo shaka yoyote, kwamba vita dhidi ya ufisadi sasa siyo tena ajenda kuu ya chama hicho kikuu cha Upinzani nchini. Vyovyote vile; imani yangu ni kwamba baada ya matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 kufahamika, Chadema kitaishi na majuto.
Kitajutia kosa hilo kubwa la kiuongozi kililofanya ikiwa ni pamoja na lile la kuwapokea watuhumiwa wa ufisadi kutoka CCM na kuwapa nafasi za kugombea ubunge huku kikiwatosa baadhi ya makada wake wa miaka mingi walioshiriki kukiimarisha.
Nasema hivyo kwa sababu chama tawala CCM kimeidaka ajenda hiyo na kinaitumia vizuri katika kampeni, na sasa kila dalili zinaonyesha kitaibuka na ushindi Oktoba 25. Wakati kwenye kampeni Chadema kinahangaika kumsafisha mgombea urais wake, Edward Lowassa dhidi ya tuhuma za kuhusika na ufisadi wa Richmond, CCM kinasisimua maelfu kwa kauli za mgombea urais wake, John Magufuli kwamba ataunda mahakama maalumu za kuwashughulikia mafisadi na majizi!
Hivi ni nani aliyeidanganya Chadema kwamba kinaweza kushinda uchaguzi mkuu wa mwaka huu bila kujikita sana kwenye ajenda ya ufisadi ambayo kwayo kilipata umaarufu kilionao?
Hivi ni nani ndani ya Chadema asiyejua ya kuwa kwa miaka karibu 20 iliyopita hakuna ajenda kuu iliyotawala chaguzi mbili kuu zilizopita zaidi ya ile ya ufisadi? Hivi ni nani asiyekumbuka kwamba kwenye uchaguzi uliopita wa serikali za mitaa Chadema kilifanya vizuri kwa sababu kilitumia ufisadi wa Escrow Account kuipa kipigo CCM?
Hivi ni nani ndani ya chama hicho asiyejua kuwa ajenda ya ufisadi ina umri wa zaidi ya miaka 20 nchini, na kwamba huwezi kuitosa ghafla (kubadili gia angani kwa mujibu wa Mbowe), na kisha ukashinda uchaguzi mkuu?
Hakuna kitakachowezekana katika jamii hii mpaka hapo tutakapokuwa tumevaa njuga kupambana na uozo uliotufika shingoni. Ndiyo maana hatutakiwi kufanya mchezo katika kuchagua viongozi wetu. Kigezo cha kwanza cha kila mgombea kiwe ni uwezo wake na mwelekeo wake katika kupambana na uozo huu.
Ni ujinga kumchagua mtu kwa sababu ni rafiki yako, au anatoka unakotoka wewe, au ni wa kabila lako. Hali tuliyo nayo ni hali ya hatari kubwa kiasi kwamba hakuna anayeweza kutuhakikishia kwamba tutaendelea kuwa na amani. Bima pekee tunayoweza kununua ili tuwe na amani ni kujitosa katika mapambano dhidi ya uozo huu. Hayo si maneno yangu. Hayo ni maneno ya mwanasafu wa gazeti hili, Jenerali Ulimwengu. Yamo katika makala aliyoiandika katika gazeti la Rai zaidi ya miaka 20 iliyopita.
Ndugu zangu, hali sasa ni mbaya mara 20 zaidi kuliko ilivyokuwa miaka 20 iliyopita wakati Jenerali akiandika makala hiyo kulalamikia ufisadi uliokuwa umetamalaki nchini. Huo ndio ukweli mchungu!
Na ndo maana naishangaa Chadema kuitosa ajenda ya ufisadi. Huko nyuma nilishawahi kusema kwamba mtu akiniamsha usingizini saa nane usiku na kuniuliza ni tatizo gani moja kuu linaloiangamiza Tanzania yetu kwa sasa nitamjibu kuwa ni ufisadi na kuporomoka kwa maadili.
Ni kweli kuwa tuna matatizo mengi kuanzia ya ukosefu wa ajira, elimu duni, kilimo duni, huduma duni za afya, miundombinu duni, ukosefu wa maji safi na salama kwa watu wetu, demokrasia changa na utawala dhaifu nk.
Ni kweli pia kwamba wagombea wetu wakuu wa urais katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 John Magufuli na Edward Lowassa wamekuwa wakipita mikoani kwenye kampeni zao na kuahidi kuyashughulikia baadhi ya matatizo hayo.
Hata hivyo, ni mtazamo wangu kwamba hakuna atakayefanikiwa kwa kiwango cha kuridhisha kama hatapambana kwanza kuuondosha uozo huo; yaani ufisadi na kuporomoka kwa maadili.
Naamini hivyo kwa sababu juhudi zozote zitakazofanywa na rais wetu mpya (awe Magufuli au Lowassa) za kutatua matatizo ya ukosefu wa ajira, elimu duni, kilimo duni, huduma duni za afya, miundombinu duni nk, zitakwazwa na kutamalaki kwa ufisadi katika kila nyanja ya maisha yetu.
Ndugu zangu, Rais Kikwete alipotamka ya kwamba kuna mchwa serikalini wanaotafuna fedha za umma hakuwa anatania. Huo ndiyo ukweli. Kwa hiyo, adui mkubwa wa rais wetu mpya ajaye ni ufisadi.
Jenerali Ulimwengu ameandika katika makala yake hiyo ya zaidi ya miaka 20 iliyopita ya kwamba; kigezo cha kwanza cha kila mgombea urais kiwe ni uwezo wake na mwelekeo wake katika kupambana na uozo huu.
Mimi nakubaliana naye kwamba kigezo hicho kilikuwa muhimu miaka 20 iliyopita alipoandika makala hiyo, lakini nasisitiza kwamba bado kigezo hicho ni muhimu mno katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu; kwani tatizo limekuwa kubwa mara 20 zaidi kuliko lilivyokuwa zama hizo.
Na ndiyo maana, binafsi, nawapima Magufuli na Lowassa kwa kigezo hicho. Mwenye nafuu katika hilo huyo ndiye nitampa kura yangu Oktoba 25, na naamini inapaswa pia kuwa hivyo kwa wengine wote wenye mapenzi ya kweli na nchi hii.
Bahati nzuri (kama unaweza kuiita bahati nzuri) ukiwasikiliza wakihutubia mikutano yao ya kampeni ni vigumu kuwaelewa Magufuli na Lowassa wanaegemea upande gani katika siasa za dunia hii yaani Kushoto au Kulia au Kati au Kati Kulia au Kati Kushoto.
Hivi sasa wanahenya majukwaani na kutoa jasho wakiahidi kuwa watafanya hiki na kile wakiingia Ikulu. Mmojawao (Lowassa) wala hata hahangaiki kuwafafanulia wapiga kura ilani au sera za chama chake (Chadema) ambazo kwazo atazisimamia akiingia Ikulu.
Kwa hiyo, kwa kuwa hatuwaelewi wakiingia Ikulu wataielekeza Tanzania yetu upande gani katika siasa za dunia hii, na kwa kuwa pia wakiwa majukwaani hawazungumzii sana ilani na sera za vyama vyao, wanatubakishia kigezo kimoja tu kikubwa cha kuwapima nacho ni uwezo wao wa kupambana na ufisadi na mmomonyoko wa maadili.
Katika makala yake hiyo ya zaidi ya miaka 20 iliyopita, Jenerali ameandika: Ndiyo maana hatutakiwi kufanya mchezo katika kuchagua viongozi wetu. Nami nasisitiza leo - zaidi ya miaka 20 baadaye ya kwamba tusifanye mchezo katika kuwapima Lowassa na Magufuli. Natutumie kigezo hicho kuwapima.
Tukipuuza na kufanya mchezo na kushabikia ule ujinga wa baadhi yetu kwamba eti tufanye tu mabadiliko hata kama tunayemwingiza Ikulu ni shetani, tutakuja kujuta kwa sababu tutamwingiza Ikulu Bw. Changamkiatenda; yaani rais ambaye atataka kujichotea ten percent katika kila mradi mkubwa wa serikali uwe ni wa ujenzi wa barabara au ugawaji vitalu vya gesi asilia nk.
Kwangu mimi - kati ya hao wawili Magufuli na Lowassa, sipati taabu mno kumtambua ni nani anayeweza kugeuka kuwa Rais Mchangamkiatenda akiingia Ikulu.
Yule mwenye ugonjwa wa kupenda kujilimbikizia mali yule ambaye amejilimbikizia mali nyingi katika muda wake wa uongozi serikalini ndiye mwenye uwezekano mkubwa wa kugeuka Rais Mchangamkiatenda akiingia Ikulu!
Vyovyote vile, tusibabaishwe na ahadi zinazowatoka midomoni wakiwa majukwaani wakati wa kampeni; bali tupime na kuangalia iwapo maneno wanayoyatamka kuhusu vita dhidi ya ufisadi yanatoka kweli mioyoni mwao au ni usanii mtupu.
Vita dhidi ya ufisadi si jambo la kufanyia usanii hata kidogo. Matatizo makubwa yanayowakabili wananchi na taifa hili yangekuwa yamepungua kwa asilimia 50 kama taifa lisingekuwa linatafunwa na kansa hii ya ufisadi na kumomonyoka kwa maadili.
Nihitimishe safu yangu ya leo kwa kusisitiza tena kwamba wapimeni wenyewe Magufuli na Lowassa kwa kutumia akili zenu wenyewe za kuzaliwa na zile za kuambiwa, na kisha fanyeni uamuzi sahihi unaotokana na kuwajua vyema wote wawili.
Jiulizeni wenyewe ni yupi kati ya Lowassa na Magufuli anakidhi kigezo kile cha kwanza alichokizungumzia Jenerali yapata miaka 20 iliyopita.
Jiulizeni:Ni yupi ana uwezo, mwelekeo na dhamira ya kweli ya kupambana na ufisadi akiingia Ikulu? Ni Edward Lowassa au ni John Magufuli?
Jiulizeni hayo; maana itakuwa balaa kumsindikiza kuingia Ikulu Rais Mchangamkiatenda. Binafsi hata nitukanwe vipi kwa simu, sms na emails, siko tayari kumsindikiza Ikulu rais wa sampuli hiyo. Tafakari.
Makala kutoka RaiaMwema, toleo 23 Sep 2015.